Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,752
- 34,057
- Thread starter
- #41
Coronavirus: Ni kina nani walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu?
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Zaidi ya nchi 50 zimethibitisha kupata visa vya coronavirus
Watafiti wanafikiria kwamba kati ya visa 5 na 40 vya coronavirus inakisiwa kwamba watu 9 kati ya 1,000 au asilimia 1 huenda wakaaga dunia.
Lakini inategemea na mambo kadhaa: umri, jinsia na hali yako ya afya na mfumo wa afya kwa ujumla.
Kwanini ni vigumu kufahamu idadi kamilia ya vifo vinavyotokea?
Hata kuhesabu visa vya ugonjwa huo vinavyotokea ni mtihani.
Visa vingi vya Coronavirus havihesabiwi kwasababu watu hawaendi kwa daktari wakiwa na dalili ambazo bado hazijajitokeza vizuri.
Idadi tofauti tofauti ya vifo vinavyoripotiwa kote duniani huenda ni kwasababu nchi mbalimbali ama zina uwezo mzuri au bado hazina uwezo wa kubaini dalili za mbali za virusi hivyo, kulingana na utafiti uliofanywa na Imperial College.
Lakini pia inachukua muda kabla ya maambukizi kusababisha kifo au mgonjwa kupona.
- Walio katika hatari ya kupata Coronavirus ni kina nani?
Katika utafiti wa kwanza mkubwa wa visa zaidi ya 44,000 kutoka China, idadi ya waliokuwa ilikuwa mara 10 zaidi kwa wazee ikilinganishwa na watu wenye umri wa makamo.
Idadi ya waliokua na umri wa chini ya miaka 30 ilikuwa chini - kulitokea vifo vinane peke yake kati ya visa 4,500.
Na idadi ya vifo ilikuwa angalau mara tano zaidi kwa watu wenye ugonjwa wa kisukari, shinikizo la juu la damu au matatizo ya moyo ama ya kupumua.
Pia idadi ya wanaume waliokufa kwa Coronavirus ilikuwa ya juu kidogo ikilinganishwa na wanawake.
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Watu karibia 621 waliambukizwa Coronavirus katika meli ya Diamond Princess nchini Japani
Je hatari iliyopo kwa watu wa eneo fulani ni ipi?
Kundi la wanaume wa miaka 80 nchini China huenda wakawa na vigezo tofauti na wanaume wa umri sawa na huo Ulaya ama Afrika ambavyo vinaweza kuwaweka katika hatari ya kupata coronavirus.
Pia matumaini ya kupona yanatgemea tiba utakayopata.
Hilo linategemea na tiba iliyopo na kiwago cha mlipuko.
Iwapo mlipuko utatokea ghafla basi huenda mfumo wa afya ukakumbwa na visa vingi.
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,
Wagonjwa wa Coronavirus Uingereza wakitibiwa katika kituo maalum katika hospitali ya Royal Free London
- Je ugonjwa huu ni mbaya zaidi kushinda mafua?
Kwahiyo ni vigumu kutambua kuna visa vingapi vya mafua au virusi vyovyote vipya kila mwaka.
Lakini bado mafua yanauwa watu wengi Uingereza kila msimu wa baridi.
Ushauri wa Shirika la Afya Dunia (WHO) ni kwamba unaweza kujilinda kutokana na virusi vya vinavyosababisha maradhi ya matatizo ya kupumua kwa kunawa mikono wako, kuepuka watu wanaokohoa, chemua na kujaribu kutogusa masikio, pua au mdomo wako.
Pia unaweza kutazama:
Maelezo ya video,
Namna sahihi ya kuosha mikono kuzuia Coronavirus
Ni nani anayepaswa kujitenga?
Unahitaji tu kujitenga kama umeambiwa ujitenge na maafisa wa afya.
Kwa kawaida wanaoambiwa wajitenge ni wale ambao''wamekua karibuni ama wako karibu'' na watu binafsi ambao walithibitishwa kuwa na virusi- waliobainika kukaa dakika 15 katika umbali wa mita mbili kutoka alipo mtu alieambukizwa.
Inakua ni lazima kujitenga na watu hususan kama umesafiri katika maeneo ya ndani ya China, Thailand, Japan, Korea kusini, Hong Kong, Taiwan, Singapore, Malaysia au Macau katika kipindi cha siku 14 zilizopita na una dalili kama vile kikohozi, homa ya mwili na kushindwa kupumua vizuri.
Katika hali kama hii, usiende kwa daktari au kituo cha afya.
Badala yake kaa nyumbani.
Unashauriwa kuwasiliana mara moja na maafisa wa afya au hopsitali ili kupata usaidizi wa haraka wa matibabu.
Coronavirus: Ni kina nani walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu? - BBC News Swahili
Kwa sasa kukisiwa kwamba uwezekano wa Coronavirus kusababisha kifo ni asilimia sio kwa kila mmoja
www.bbc.com