Njia rahisi ya kujilipua Abroad, (Risk Takers & Wapambanaji tukutane hapa)

Bastille

Member
Sep 7, 2018
12
46
Hopefully wote tupo njema tukiendelea kupambana na hali zetu. Kutokana na hali ya tz kubana sana kumekua na harakati mbali mbali za raia kujaribu kupeperuka na kusaka maisha sehemu tofauti tofauti (Nje ya nchi).

Risk takers, Wazee wa kujilipua na watafutaji njooni tukutane hapa tupeane uzoefu jinsi ya kupasua huko mbele. Nitaelezea taarifa zote ambazo nazifahamu hatua kwa hatua, Kuanzia jinsi ya kupata Passport mpk mwisho, Then wenye ujuzi na uzoefu zaid watatusaidia kujazia. Lets Go.!!

Kuna njia tofauti zinazotumika ili kutoboa nje ila zinatofautiana ki gharama na risk. Hapa nitazungumzia njia ambayo ni less expensive (Haina gharama sana) na less risk (hatari yake ni ndogo), Hapa nazungumzia njia ya kwenda Kusoma either (Diploma, Bachelor, Masters and Post-Graduation).

Mainly nitaongelea Germany kwa kuwa nchi hii elimu ni bure vyuo vingi vya public kwa ngazi ya Degree & Masters. Mwanafunzi atachangia Semmester fee ambayo atalipa mara moja pindi anapoanza muhula na hii ina cover ticket fees ndan ya mji uliopo(chuoni) na nyingine inaenda kwa students services inategemea na mipango ya chuo na hii fee inaanzia €50-€350 kulingana na chuo, vyuo vingi vya miji mikubwa ndio vina semmester fee kubwa.

Pia utajihudumia gharama za kimaisha nwenyewe hapa nazungumzia Accomodation, Health insurance, Food , Books Entertainments(sio lazima). Tukianza ktk Accomodation unaweza tafuta students halls za chuo husika kama zipo.
Hizi huwa ni nafuu zaid kuliko kupanga appartment/flat za nje....students halls zinaweza kuanzia €150-€400 per month na flats /appartments nyingi huanzia €200-€600 per month hii pia inategemea na mji uliopo..miji mikubwa kama Berlin, Frankfurt am main, Hamburg, Munich na Dusseldorf maisha ni ghali ingawa ina nafasi nyingi za ajira.

Hapa sasa umeshapata mwanga jinsi maisha yatakavyokua na umejipanga vipi mambo ya tiketi nadhani yanajulikana.

Wanafunzi wengi wanatamani kupata hii nafasi ila wanakwama kutokana na sababu mbali mbali kama
1. Mitihani la Lugha IELTS na TOEFL
2. Lugha ya KIJERUMANI
3. Bank Statement/Sponsorship hii ni wakati wa kuomba VISA.
Hizi sababu haziwezi kukukwamisha still bado una nafasi kubwa tu ya kutusua, nitaelezea what i know na nilichokiona kwa watu wa pembeni.

1. JINSI YA KUPATA PASSPORT

Siku hizi zoezi hili limekua simple atleast sio kama zaman mpk utumie vishoka, cha kufanya ni kutimiza Vigezo vyote vinavyohitajika kama vile.

i) Kitambulisho Cha Taifa
Lazma uwe nacho bila hiki huwezi kukamilisha zoezi so hapa ni muhimu.

ii) Cheti cha kuzaliwa
Hiki pia muhimu kama unacho fresh no prob..kama huna fuatilia au jiongeze kwa wajanja. Kwa wale ambao wamezaliwa 1980 kurudi nyuma wanaruhusiwa kutumia affidavit km hawana vyeti, hii affidavit utalipa elfu 10 then watakupatia pale pale Immigration.

iii) Barua mbili. Moja ya maombi ya passport na nyingine ya mzazi kuthibitisha ombi lako hii utaambatanisha na kitambulisho chake cha kupiga kura au cha utaifa.Barua zote hizi zinapatikana stationary pale nje ya uhamiaji.

iv) vyeti vyako vya masomo, hivi vinajulikana.
Hapa utakua upo good to go..make sure umefuata taratibu za ujazaji form online umelipia na ushaprint..hii haina shida utasoma kwenye site yao watakupa maelekezo its simple. Baada ya wiki utakua ushapata passport yako.

2.KUTAFUTA VYUO.

Germany kuna intake mbili kwa mwaka, kuna Summer Semmester na Winter Semmester.
Winter semmester hii naiita semmester kubwa kwa kuwa vyuo vingi sana vinafunguliwa muda huu huwa inaanza August/September/October kulingana na ratiba ya chuo husika, Summer semmester hii inaanza March/April. So utaangalia kama utapata course yako stahiki kwa semmester ipi.
Hapa tunacho angalia ni vyuo ambavyo utapata course wanayofundisha kwa lugha ya kingereza tuu ili tukwepe gharama za kuhangaika kusoma kozi za lugha ili kupata cheti chao, Tumia Sites zifuatazo kupata unachohitaji
1. daad.de
2. study portals
Ukichagua course angalia je wanatoza ada? Vp requirements zao? ni mji gani chuo kipo ili kujiandaa na gharama za kuishi, jaribu ku contact na chuo kupitia E-mail ili kupata taarifa zaidi. Nashauri kuchagua chuo chenye requirements nyepesi ili kujiongezea nafasi ya kupata admission.

Kuhusu kigezo cha IELTS au TOEFL usiwe na shaka kuna vyuo haviitaji u submit hivi vyeti kama elimu yako umeipata in English, hapa wa TZ hatuna shida Elimu zetu ni kingeereza so we are good to go, au kama umefaulu sana somo la English pia ni advantage.

So baada ya kupata vyuo kinacho hitajika ni wewe kuandaa Documents zako muhimu kama vile

i) vyeti vyako vya masomo

ii) C.V

iii) Motivation Letter( hii utaelezea kwann wakupe nafasi hapo chuoni, jitahidi kuwashawishi)

iv) Passport

v) Extra curricular activities ( kama kuna internship uliwahi fanya unaweza attach).

3. KUFANYA APPLICATION

Hapa ndio kuna mambo yenyewe, kuna njia mbili za kufanya application ambazo nazifahamu.

i) kutumia UNI ASSIST.

ii) kutuma maombi Direct chuoni(Online Portal)
Hii njia ya kwanza vyuo vingi vinatumia ili kuweza kuwasaidia international students ambao hawajapata high school education in Germany, hivyo basi Uni Assist watakusaidia ku Convert Grade zako ziende kwa mfumo wa kijerumani. Njia hii ni nzuri ila ina gharama.
Kwa application ya kwanza utalipia €75 then kwa kila application inayofuata utalipia €30. Unachohitaji ni kujisajili na utaingia utachagua chuo chako then utajaza details zote ulizonazo.
NB: bado sijaitumia njii hii hivyo basi wanaoijua kwa kina wanaweza kutusaidia mpaka mwisho jinsi ya kuzituma.
Njia ya pili, hii ya kufanya application direct chuoni. Sijajua kama kuna vyuo vinakubali ufanye application kwa vyeti vya hapa Tz ila wapo watu waliokwenda Embassy ya Germany na wakasaidiwa vyeti vyao vikawa converted to Germany grades then wakafanya application.

NB: hapa pia kunahitaji ujaziaji kwa wale waliofanya application kwa njia hii.
Nitaweka list ya vyuo vinavyo fundisha baadhi ya course in English (Undergraduate) lakini pia masters ni nyingi zaidi.

NB: vyuo hivi nimeweka kwa wale ambao wanataka ku apply summer semmeater najana ndio wameanza kupokea maombi mwisho ni 15 january na kuanza masomo ni 1March/April. Hivyo basi kuna vyuo vingi sana ila vingine ni Winter semmester yani kuanza masomo October 2019 kwa wanaovumilia watasubiri pia, usajili wake ni May-July .

1. HTW Berlin
2. Worms University
3. Deggendorf Institute of Technology
4. Johannes Guternberg University
5. University of Tubingen
6. Technische Hoschule Nurnberg
7. Leuphana University
8. University of Bamberg
9. Hildeshein University
10. Koblenz University.

Wenye ujuzi na experience zaidi watatusaidia zaid katika kufanya maombi.

4. VISA Application

Hapa ni sehemu ya kuomba mungu sana uwe na bahati lakini pia ujipange haswa katika pande mbili, moja uwe mkamilifu wa documents zote zinazohitajika na ziwe za uhakika ili kuepusha mvurugano wakianza kukuulizaaswali. Pili ujipange kiakili kujibu maswali kama utafanyiwa interview.

Requirements muhimu wame orodhesha katika site yao hivyo utaziandaa kwa student hakuna nyingi na hazipo complicated but main issue inakua jinsi gani utakua funded. Wengi wetu humu tunaenda ku hustle kule kupata maisha hivyo uhalisia ni kwamba hatuna pesa, je tutapita vipi hiki kipengele.?

Ipo hivi tafuta bank statement ya mtu yeyote ambaye unafaham ana mzunguko mkubwa wa pesa almost 20m is enough au zaidi will be much better. Then utasema huyu ni sponsor wako ambaye ni ndugu wa karibu kama haweza kuhudhuria kwenye interview basi uende mahakamani ukawekewe muhuri wa kiapo cha kuthibitisha ni kwl anakudhamin. Then wanaweza wakampigia simu kumuuliza maswali mawili matatu so ni vizur ukaweka namba za mtu ambaye umempanga vizur na anajua nn cha kujibu. Nadhani ukipita kipengele hiki utakua ktk nafasi nzuri

Tuhamie upande wa Interview kama utafanyiwa wengine hawafanyiwi kabisa kutokana na ukamilifu wa documents zao. Kuna maswali ambayo ni Common na ukijibu vizuri basi una nafasi kubwa ya kupata VISA yako. Maswali ni kama yafuatyo:-

1. Jina lako na Taarifa za msingi

2. Kwanini umechagua kozi hiyo?

3. Kwanini huwezi kusoma hapa hapa tz?

4. Kwanini sio U.S or Canada?

5. Utafanya nn baada ya Elimu yako?

6. Una ndugu au jamaa huko?

7. Umejipanga vipi na safari yako?

8. Nani anakufadhili na uhusiano wenu?

9. Unajua nini kuhusu Ujerumani?

Nadhani kutakuwa na majibu tofauti tofauti kulingana na upana wa uelewa wetu, kikubwa ni kutoa majibu sahihi na kuonyesha kuwa utarudi na confidence ni muhimu sana.

Mpaka hapa nimejitahidi kuweka taarifa ambazo nazifahamu so kama kuna sehemu nimeyumba wajuzi zaidi na wenye uzoefu watanisaidia kuongeza au kurekebisha.

Usikate tamaa kila kitu kinawezekana despite of challenges zilizopo ktk kila stage just focus on the main Goal.

Lets meet there.....!!!

Best Regards,

Bastille.
 
sina mpango wa kujilipua ila ahsante sana Mkuu kwa uzi huu
Binafsi nashauri kutumia UNI ASSIST na sio kuapply mwenyewe(hawa jamaa wana uzoefu na watakusaidia sana)
Nina imani umewasaidia wengi
MAISHA POPOTE
 
Shukran Chief
 
Heko kwa kufafanua vizuri mkuu. Ila Naomba nikuongezee kitu Muhimu zaidi walichofanya wajeremani ili kuziba mianya ya mabaharia wazamiaji kwenye hili Kwani wahindi, wapakistani, wabangladeshi, wanigeria walitaka kufilisi social welfare benefit ya mjeremani kwa kujifanya wanaenda masomoni kumbe walikuwa wanataka kuzamia tu.

Inajulikana wazi kwamba German education is dirty cheap with excellent infrastructure and world class facilities hivyo iliatract watu wengi kutaka kusoma German but wazamihaji wa kutaka kuishi na kuhaso tu walikuwa wengi kuliko Wakusoma. Hivyo wakaintroduce system moja makini sana ya kuziba mianya ya wazamihaji kupenya kiwepesi.

System hii iliwataka wanafunzi wote wenye vigezo kufungua kwanza "online blocked bank account" wakiwa nchini mwao ambayo hawatakua na total control nayo yenye jumla ya million kama 22 hivi za kibongo ambapo mwenye account anapewa access ya kutoa €650 kwa kila mwezi. Kwa hiyo mwanafunzi alitakiwa kubalance asitumie zaidi ya Euro 650 kwa mwezi. Na hiyo account unaifungulia online unadeposit hiyo pesa kwenye Deutsche Bank ya Germany then inablockiwa na unakuwa huna access na control ya moja kwa moja sababu awali wanaigeria walikuwa wanaazima hela kwa Mtu wanaingiza kwenye Deutsche Bank then wanapewa visa kirahisi afu wanazitoa hela zote na kurudisha walikozikopa na kwenda kuishia mitaani huko Berlin na kusumbua serikali ya ujeremani kwenye welfare support.

"By mandate, a student planning to study in Germany is supposed to prove that he/she can afford his/her stay in Germany for at least the first year of study. For this, the government has decided on a particular sum. As per the Federal State, a student is required to prove that he/she have access to at least 659 euro per month for the first year, or 7,908 euro total. This, in turn is done by means of opening a blocked account."

Pale embassy hawana shida wakipatiwa hii document from Germany Deutsch bank ikithibitisha mkwanja ushatumwa na umeblockiwa kitu ni fasta tu unapewa visa yako. Na hapa ndipo ugumu unapokuja kwenye kusoma Germany lazima uwe na mkwanja wako au wa mdhamini alisi na alietayari kukudhamini afu wao ndio waushike ndio usome bure unless husomi kwa mjeremani na utaendelea na kusoma VETA.

Hivyo tu!
 
Aisee
 
Back
Top Bottom