Nitazungumza na Watanzania kuomba ridhaa ya kuwania Urais

Status
Not open for further replies.
Nitazungumza na Watanzania kutoka Makao Makuu ya Nchi-Dodoma, Mazungumzo yangu nanyi yatajikita kuomba ridhaa ndani ya Chama ya Kugombea nafasi ya Uras wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tukiwa tunaianza safari ya Kuelekea Miaka 50 tena ya Taifa letu, Naomba usipitwe na Mazungumzo yangu yatakayokuwa LIVE kupitia Redio na Televison Mbalimbali hapa Nchini.

Siku ya Jumapili, Saa 9 Alasiri hadi 12 Jioni, Chuo Cha Mipango Dodoma.

Ukumbi: Mwl.Nyerere Hall "

WAKATI NI SASA,MABADILIKO KWA VITENDO"

Ngoja tukisikilize mkuu. Lakini pia uje utuambie yale maoni yaliyotolewa na Wananchi yakatupwa wakati wa Bunge maalum, ukipewa nchi utayarudisha?

By the way hongera na kila la heri.
 
Mwigulu nchemba alikua safi hapo mwanzo,tatizo kilichomharibia ni kipindi kile anaongea ovyo bungeni,ndo mambo yaliyomharibia cv yake na mwonekano wake ktk jamii hii ya watanzania!

cku zote unapofanya jambo focus na mbele!
Mtu gani hana hata busara na uvumilivu kwa wengine kisa tu wanatofautiana kimtazamo,mtu na heshima zako unachukua hotuba ya wapinzani unaitupa huku watanzania wote wanaona halafu sasa hivi "........nitaomba ridhaa kwenu....." kina nani? Hao Watanzania uliokuwa unawaonyesha madharau ya kijinga mchana kweupe.Give us a break dude!
 
Mwigulu Nchemba

Haaa , Duh na wewe unataka kugombea urais, kweli nimeamini ''kwenye msafara wa mamba hata kenge wanakuwepo''.
 
Last edited by a moderator:
ufisadi unaofanywa na TRA bandarini+ shilingi yetu kushuka thamani+kumbambikia kesi Rwakatare,bado unajiona unafaa kuwa Rais?!!Labda Raisi wa FM academia
 
Je tukikupa urais utapata muda wa kuja hapa JF na kujibu maswali yetu?

kwani ameshawah kujibu maswali ya wanaJF mefuatilia profile yake sijaona reply yake nikagundua yuko vizuri kwenye kuanzisha topic ila kujibu 0. Duuh! kwa mara ya kwanza leo ndo naona uzi wa kiongozi mkubwa humu Jf nadhani wengi wanaogopa changamoto
 
Mwigulu Nchemba

Nchi imeishiwa viongozi wa kuiongoza. Hata wewe unautaka urais?

Tuambie ukweli, jina lako ni Madelu au Mwigulu? Nani alipanga ugaidi wa Lwakatare? Nani alimmwagia Musa tindikali, nani alifumaniwa Ugoni Igunga, nani alipanga bomu la Soweto na nani aliwatuma vijana wa CCM kuganya fujo ndaga kwenye mkutano wa Mnyika?

Kama ukiwa naibu katibu mkuu CCM ulihujumu elimu ya uraia kwa wanyiramba wakati dkt Slaa akiwa Iramba kwa kupeleka timu ya simba, ukipata uraisi si utaigeuza TZ China, yaani viongozi wa upinzani si utawanyonga ?

In short uraisi sio hadhi yako na hutopitishwa na chama chako na ikitokea ukapita, basi Tanzania inachukua kombe la dunia

Tulimsikia wote akidai kwamba CHADEMA walijipiga bomu wenyewe Arusha. Mwinyi was right: Tanzania imekuwa kama kichwa cha kichaa. Yaani kila mtu, hata wale wenye historia za kutisha wanadhani wao wanatakiwa wawe Rais!

I am greatly amused that Mwigulu thinks that he is presidential material!
 
Wizara ya fedha umeshindwa kulinda thamani ya shilingi ya Tz, utaweza urais?
 
Tulimsikia wote akidai kwamba CHADEMA walijipiga bomu wenyewe Arusha. Mwinyi was right: Tanzania imekuwa kama kichwa cha kichaa. Yaani kila mtu, hata wale wenye historia za kutisha wanadhani wao wanatakiwa wawe Rais!

I am greatly amused that Mwigulu thinks that he is presidential material!

Hawa ndio team Lowassa walioandaliwa ili baadae aje aseme najitoa kumwachia EL
 
Umeshindwa kuipigania shilingi mpaka imeporomoka je kuongoza nchi utaweza wewe!
 
Hongera sana Mwigulu.

Tuna imani na wewe, hakika ni wakati wa mabadiliko kwa vitendo, tuanzie hapa..
 
Mwigulu Nchemba
...Maswali yangu kwako kabla ya kutangaza nia hiyo jpili:

1. Hazina mnaiacha na reserve kiasi gani?

2. Mifuko ya jamii mnakokopa (kwingine mnachukua tu)fedha za kuendesha serikali mnailipa lini?

3. Sisi kama nchi tuna hifadhi ya dhahabu (gold bullion) kiasi gani kule BoT?

4. Wewe kama waziri(naibu) umefanya nini kupambana na wezi wa escrow account money?

5. Nani wahusika/wamiliki wa Simba Trust iliyokwapua sehemu ya hela ya escrow?

6. Nani walichukua hela ya escrow kule stanbic bank?

7. Je nyie kama serikali mmetekeleza maazimio ya bunge dhidi ya wezi wa escrow kwa kiasi gani hadi sasa?

8. Ni kwa kiasi gani wewe kama waziri umeshiriki kupunguza deni la taifa?

9. Wewe kama kada wa chama unaridhika na zoezi la uandikishwaji wapiga kura kupitia BVR?

10. Wewe kama kada wa ccm una maoni gani kuhusu katiba mpya na kura yake ya maoni?...

11. Ukiwa kiongozi umepambanaje na ufisadi katika taifa hili hadi leo?

12. Umechangiaje kama waziri kupunguza madeni ya waalimu ktk taifa hili?

13. Nini umefanya hadi leo ukiwa waziri kutufanya tukuamini kuwa rais??....

Ukinijibu maswali haya na kumridhisha kila mtu humu JF basi unastahili kuwa rais ajaye TZ.....kinyume chake wala usijaribu kugombea maana hutotufaa....
 
Last edited by a moderator:
Kila la kheri brother

Kwa hivi sasa, hakuna mtu mwingine kuivusha CCM zaidi ya wewe na kwa mbali sana Membe na Magufuli. Achana na wengine wamekaa kama magugu na sangare yakisongasonga mazao shambani.

Kumbuka kuwa Watanzania hawataki uhafidhina wa kichama, nena na tenda kwa kuweka maslahi mazima ya mama Tanzania. Kipindi baada ya kuteuliwa kuwa Naibu katibu mkuu wa CCM ulipotoka sana lakini ulijirudi sana baada ya kuwa Naibu waziri. Na hapa ndipo Watanzania walipokuona kuwa unafaa kuwa rais wa Tanzania siku moja na huenda hiyo siku mmoja ndio mwaka huu.

Kila kheri.
 
Mwigulu,umefanya vema kuthubutu kujitokeza,ila bado kidogo kwa nafasi unayoiomba.

TANZANIA INAHITAJI KIONGOZI MAKINI,ALIYEJULIKANA KWA MUDA MREFU NA KUONWA UWEZO WAKE KTK KUKABILI HALI HASI NA CHANYA.

BADO HATUJAKUPIMA,BADO HAUJAPITA KTK MOTO,BADO HATUJAKUJUA.
 
Mwigulu Nchemba

Hizi ni hadithi za kina Lowassa,mtu unajifanya kuomba ridhaa kwa wananchi kugombea urais,wakati umeshajipa ridhaa mwenyewe,halafu unajifanya kuomba ridhaa kwa wananchi,si mkae kimya muone kama wananchi watakosa kupata rais.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom