Nitaunga mkono endapo Mwakyembe atalifungia gazeti LA Mtanzania kwa uongo huu

Leo gazeti LA Mtanzania limechoza na kichwa cha habari ambacho kimewekwa kama habari kuu kikiuarifu umma kuwa " SERIKALI YATANGAZA AJIRA 52436" ukisoma undani Wa habari wameandika kuwa waziri akijibu swali bungeni alisema kuwa serikali inakusudia kuajiri 52436 kwa mwaka Wa fedha 2017/2018. Sasa kwa haBari hii ni wapi serikali imetangaza Ajira kama siyo uandishi Wa kikuda na Wa kupotosha watu ili wavutiwe kununua gazeti hilo.? Huu uongo Wa kibiashara haukubaliki, ninashauri waziri mwakyembe alichukulie hatua gazeti hili ili wajifunze kuadnika habari vizuri. Gazeti hili lifungiwe maisha au kwa miaka kadhaa ili iwe funzo kwa magazeti mengine na waandishi uchwara

magazeti yote siku hizi yamekuwa ya kidaku tu.
 
Nakumbuka niliwahi kutoa mada kuwa baada Jukwa la Wahariri kupitia kwa Neville Meena kutangaza kususa habari za Mkuu wa Mkoa ktk Media mauzo yamepungua sana mitaani na return ni kubwa ya magazeti kwa sasa.

Nikapingwa sana,ooh leta data, sijini nini!! Sasa nadhani kwa Habari kama hii inaonyesha kuwa ni ya kuuzia Gazeti kabisa na kama kweli ni ya uwongo basi ni uthibitisho mzuri wa nilichosema kuhusu kuporomoka kwa mauzo ya magazeti.
 
Kilichoandikwa ni sawa kabisa, ajira zilizotajwa ni za 2017/18 ajira hizo ni kwa bajeti ya mwaka wa fedha unaoanza Julai. Kosa la mwandishi ni nn kuripoti matarajio ya Serikali, ambayo yametamkwa na Serikali yenyewe?
 
Sasa wangeandika "Serikali inatarajia kutangaza ajira 52436 kwa mwaka wa feza 2017/2018" ungenunua gazeti? acha kuingilia biashara za watu.
 
" SERIKALI YATANGAZA AJIRA 52436" ukisoma undani Wa habari wameandika kuwa waziri akijibu swali bungeni alisema kuwa serikali inakusudia kuajiri 52436 kwa mwaka Wa fedha 2017/2018.
Sioni tatizo katika hii habari, bado kama miezi mitatu mwaka mpya wa fedha uanze na kama waziri kaahidi basi ndo ajira zenyewe, tatizo liko wapi, au labda ungetupa mbadala wa heading ambavyo ingepaswa kuwa, tatizo ni pale kama waziri anaudanganya umma, na kufungia sio suluhu, tuachane na kasumba za kidikteta
 
Back
Top Bottom