Nipo tayari kukosolewa: Rais Magufuli kama kawaida ameongozwa tena kwa chuki, hasira na pupa!

Nilivyomuona Magufuli jana alikuwa na kitabu ambacho kina evidences walizokuja nazo hawa maprofesa. Wewe unampinga kwa kutegemea porojo za mjini na hear says, hiki ndio kiwango cha ujinga kama nchi tulichofikia. Pia kumbuka ilichotamka tume ndicho wengi tuliaminishwa. Hans Pope na wataalam wengine walituaminisha kuwa hatuna umeme wa kuweka smelter na pia gharama ya smelter ni dola bilioni moja, kumbe kuna hadi Mini Smelters. Nchi hii imefikia wakati wataalam wanapotosha ukweli ili wapate hela ya mboga na kuweka rehani ajira na matibabu ya wananchi
Hataki tuwaamini hao wataalam waliochunguza hilo sakata. Ni ngumu sana kutetea majambazi
Acha tu ndugu yangu, nchi imeliwa mno.
 
9f81bebc15b7043319c34c46c0bf516b.jpg

Wakati unaunga mkono tamko la jana hukufikiria kwa kina.!
aksante mkuu idawa ungemwambia neno moja tu ukiwa muongo uwe na kumbukumbu!
 
Yaan nyie watu ni mijib.wa kabisa, mambo ndo kwanza yameanza kakurupuka kwa lipi? hayo mambo ya sheria kwani kamati ishawasilisha taarifa za utafiti wao juu ya hili swala? mnatia hasira sana.
 
Mkuu wenzio wamefanya utafiti na wameleta majibu kwa Umma wa tanzania....wewe utafiti umefanya lini? kwa hiyo unataka kusema hiyo mikata ndio inasema kuwa kwenye documents waandike dhahabu kwenye mekanika ziko 0.03 wakati ziko 38%? mikataba inasema wadanganye?
Hebu kwanza tukumbushe report ya Hostel za Dares-salaam imefikia wapi?
 
Hiyo report ya Prof.Mruma ni sawa na ile ya Wilson Mukama ambaye alijiandikia 'presentation' ya kupata Ukatibu Mkuu wa CCM badala ya kuandika utafiti wa kuikwamua CCM na ujinga ujinga wao...matokeo yake aliupata ukatibu mkuu wa CCM but he was a total failure...

Ningetamani sana kumsikia Prof.Muhongo akisema chochote lkn bahati mbaya yeye siyo kama Nape Nnauye atakufa na tai shingoni and he will not speak..

Li Magu lina roho mbaya sana ya visasi na chuki huo moyo wake uliojaa chuki namwombea tu Mungu asije akapatwa na maradhi mabaya ya moyo...ukiwa mtu huwezi kuishi na binadamu wenzio ukiwatendea mabaya hivi, halafu unamlinda Bashite???
 
Kwa hili sina mjadala wasuse tu.lakini madini yetu yanaibiwa.
Hautakiwi kuwa mganga ndo ulijue hilo.maslahi yetu yameguswa sana.hatuwachukii wawekezaji.wala hatuwafukuzi.ila kuwe na mikataba yenye faida kotekote
 
Rais Magufuli tangia akiwa waziri wa ardhi na nyumba, ujenzi na hatimaye uvuvi kabla ya kurudi tena ujenzi, hajawahi kamwe kufanya maamuzi magumu na hatimaye yakafanikiwa. Katika enzi hizo Kikwete ndiye alikuwa mhimili wake mkuu na chombo kikuu cha kumuongoza.

Rais Magufuli ndiye pekee waziri ambaye viongozi wake wakuu (waziri mkuu na baadaye rais mwenyewe enzi hizo akiwa waziri ) walitoka hadharani na kumkosoa mbele ya umati kwa matendo yake ya pupa, hasira na chuki. Hili kwangu lilikuwa jambo la kushtua.

Lakini nilishtuka zaidi pale nilipolala nikaota kuwa Magufuli ndiye rais wa Tanzania. Nilishtuka tena zaidi pale nilipoamka na kukuta ndoto yangu niliyoota kumbe lilikuwa ni jambo la "live" Magufuli sasa ndiye rais wa Tanzania.

Kwa dhati kabisa naunga mkono kuwa mikataba ya madini waliyoingia Chenge na Mkapa ilikuwa mibovu sana. Ubinafsishaji wa mashirika ya umma, viwanda vya serikali waliofanya Chenge na Mkapa ulitia aibu taifa. Mwaka 1997-98 ulikuwa mwaka wa laana kwa Tanzania. Kiwanda kikubwa chenye eneo kubwa na mashine za kisasa kama TPI kuuzwa milioni kadhaa za kitanzania ni uwenda wazimu wa aina yake!

Tukio la jana: Hili ni tukio ambalo litaleta "total failure" kwa rais Magufuli na watanzania. Pengine litakuwa tukio tutakalokuja kukumbuka huko baaday kama tunavyokumbuka leo ya mwaka 1997-98.

Jambo linalofanywa na mtu mmoja (kama Magufuli) ama watu wawili (kama Chenge na Mkapa) nje ya mamilioni ya wataalamu ni la kuogopwa sana! Siyo jambo sahihi katika tu mwanzo wake.

Jana nilimsikia Profesa Mruma akisoma ripoti yake kwa hasira nikajiuliza, huyu si anasoma Alichofanyia utafiti? Hasira za nini? Nikamsikia Magufuli akitamka maneno "Upumbavu" na "Profesa Muhongo, profesa mwenzako ameku-prove wrong" Kisha nikamfananisha na Mruma nikajikuta nikisema mbona kama Magufuli amemteua mtu wa aina yake kwenye hili? Tutaupata ukweli na uhalisia?

Hatimaye haraka haraka Muhongo akaliwa kichwa na watendaji wengine. Hilo kwangu siyo shida.

Shida yangu ni je documents halali ambazo copies zake zipo kwa wanasheria na mahakama za kimataifa zinasemaje? Hawa wawekezaji wanafuata sheria zipi kwenye hayo mambo?

Kuna wakati nilimsikia rais Magufuli akisema kuwa hawa wawekezaji wakishachukua mchanga wanaenda kuwauzia wenye Smelters kisha wao biashara yao inaishia hapo? Kiongozi mkuu kuongea jambo ni lazima uwe na documents halali za kukupa support. Je Magufuli anazo?

Rais Magufuli ajue kuwa, na awe makini sana kuwa, sasa yeye ni kiongozi na atakaloongea ama kufanya anafanya kama kiongozi. Asije akadhani kuwa ataharibu kisha atokee Kikwete mwingine wa kumrekebisha. Akishaharibu yeye ni Tanzania imeharibu. Leo tunalia juu ya Bilionea Chenge na Mkapa. Tusije baadaye tukalia tena juu ya Magufuli na Masaju!

Zipo taarifa kuwa Muhongo alimuelekeza rais Magufuli ukweli wote kuhusu hili sakata la mchanga na madini. Akampa paka sheria zinazotubana pia akamtahadharisha tutakapokwamia endapo kama tutaamua kama tulivyokuwa jana. Lakini baadaye Mruma akaipindua akili ya Magufuli na ndipo ikawa vile.

Mimi huwa naamini kuwa jambo lolote lile linalofanya na mtu mmoja nje ya wataalamu mamilioni kwa mamilioni kama alichofanya Magufuli siyo jambo sahihi. Jambo lolote lile linalofanywa na watu wawili kama alivyofanya Mkapa na Chenge siyo jambo sahihi. Ndio maana kukawepo na bunge. Hilo ndilo hasa linaloweza kuja na jambo sahihi kwakuwa linahusisha mijadala huru. Bunge ndiyo mwanzo wa kila kitu. Huko kwingine hata sikuamini. Naisubiri kwa hamu ripoti ya bunge juu ya hili. Ninaunga mkono kuwa Mkapa na Chenge walituletea janga na hata jana nilisema hilo kuwa kwa Magufuli ninachounga mkono ni kuwajibishwa kwa Mkapa na Chenge watueleze ni kwa nini aliamua hivyo. La jana bado nalitafakari ila nikitambua kuwa Magufuli huyu tuliye naye leo ndiye yule waziri wa jana. Umakini mkubwa juu ya maamuzi yake ni lazima uhitajike na hasa tukiielewa vyema historia yake ya pupa na hasira. Kazi ni yetu sisi wa Tanzania kwakuwa Magufuli atapita kama alivyopita Mkapa aliyesifiwa kipindi hicho na sasa analaumiwa kweli kweli. Chanzo ni maamuzi ya akili moja! Bunge likiwekwa kando ni lazima ukwame tu.
Kwakweli wewe ni COWARD!!!! Liwalo na liwe wacha ulimwengu ujue tunavyofanywa maskini. Ni bora tuwekewe vikwazo kama Zimbabwe kuliko kuendelea kuibiwa angali tumeshajua wanavofanya. Ni bora Rasilimali zilizobaki ikiwemo madini zibaki kama zilivyo kwakuwa mpaka sasa hazina msaada kwa mwanachi wa hali ya chini na kwa watanzania waliowengi ukiacha hao madalali wachache wanaofaidi. To hell with them. Unaongea pumba. Look at Chile today they've been very strong huko nyuma for establishing the foundation of strong institutional and today is the only Latin American country to be member of OECD. Wewe kalaghabao! Ale chikuona!!!sandeni sana du.
 
Mfumo wa uongozi aliouweka Rais
fumo wa uongozi aliouweka Rais Magufuli awamu hii ndio utakaoliingiza taaifa hili pabaya. Magu amejitahid na amefanikiwa kuweka mfumo wa watu kuwaona wote wanao-challenge mawazo yake ni wezi, wapiga deal, mafisadi, wala rushwa au wamepewa chochote kile wamkosoe. Huu utaratibu ni mbaya na naona taratibu unaanza kulitafuna taifa. Ss hv ukiongea tofaut na mawazo ya Rais au Serikali yako basi ww utaonekana ni moja ya watu hao niliowataja hapo juu. Kuna vitu vingi tu ss hv Mh. Rais anachemka lkn watu (wataalam) wanapiga kimya kwa kuogopa kuonekana hawaitakii mema nchi hii au wamepewa hela (wamehongwa). Hii ni mbaya sana kwa taifa. Ku-challenge (kuhoji) maamuz au mawazo ya Rais (au Seikali) sio usaliti kwa nchi, ni njia nzuri ya kufanikisha mambo yaende, hatuwez kufanana mawazo au mitazamo naukiona mnafanana kwny kila jambo basi ujue anguko lenu limekaribia.

Kwny taarifa ya jana kuna vitu vimepotoshwa /vimekuzwa lkn watu hawawez kuviongelea kwa kuogopa km nlvyosema hapo juu. Mkulu anaposema kwa makontena yale 277 serikali ilkuwa inapoteza mapato kati ya Bil .... na Trilion ..... ya dhahabu sio sahihi. Hizi ni true value (thamani halisi) ya dhahabu iliyopo kwny makontena ambayo ikiuzwa, serikali kupitia TRA itachukua kodi/tozo/mrahaba wa 3% kwa sheria ya ss hv. Kwahiyo hiyo hela yote sio ya kwetu, sisi tuna % tu ya hela hiyo iliyotajwa. Tatizo lililopo ni kuwa kulingana na taarifa ya tume, thamani halisi ya dhahabu ni ndogo kuliko iliyotajwa hapo mwanzoni. Sasa hili tumelikuza na kuwaaminisha wanatanzia tumeibiwa kati ya Bil .... na Trilion ..... wakati si kweli chetu pale ni 3% ya true value (Bil ..... to Tril .....)
Ni km kwny biashara zingine tu za uzalishaji, utazalisha soda utauza zile soda, baada ya mauzo halisi ya soda zile kwa thamani sahihi ya soda, ile hela iliyopatikana (gross revenue) itapigwa % kadhaa kama kodi/tozo na mzalishaji atabaki na chake baada ya kodi/tozo (net revenue). Sasa jana tumeaminishwa ile gross revenue baada ya kuuza zile dhahabu ni yetu yoteee. Hili tulikosea jana na kuleta tahaaruk kubwa ya kuonuesha kuwa tunaibiwa sana. Ni kweli tunaibiwa lkn tuepuke kukuza mambo.
.
 
Back
Top Bottom