Benny
JF-Expert Member
- Jun 6, 2014
- 3,275
- 5,403
Mkuu kwa ushauri huu lazima nkurunzinza aachie madaraka
Hahaha...
Mkuu kwa ushauri huu lazima nkurunzinza aachie madaraka
Hwaambie wasilete mgonjwa la sivyo utajinyonga mkose wote...
Ushauri kutoka kwa mdau huyu ndo wa kuufuata,,, akuna cha kuongeza. Biashara tuifungie apa,,,,Kuna vitu vinatokea kama lesson katika maisha.
Suala la ugonjwa hakuna mtu anayepanga, vivyo hivyo suala la kupona.
Zamani walikuwa wanaamini kila mtoto anazaliwa na riziki yake. Yawezekana msemo huu ni kweli kwasababu hakuna anayeweza kubashiri kwamba huyu ndie president ajaye.
Point yangu ni kwamba; ongea na mzee wako nafasi uliyonayo kwa kumwelewesha kuwa, kama mgonjwa wanataka aje, basi ukoo uchange pesa hata kwa kuuza mashamba ili nauli na pesa ya matibabu ipatikane.
Suala la kufa au kutokufa sio kazi yako. Ikitokea amekufa mikononi mwako basi Mungu atakuwa ameamua kukupa somo, na nakuhakikishia hautakosa msaada au namna ya kuhandle hilo jambo. Ila kukataa kwamba asiletwe kisa huna nafasi sio busara na hakuna jamii itakuelewa.
Comment yako ulivoiwekea manjonjo, nimecheka kwakweliKuhusu kifo usihofie! Kwa ninavyowajua wa tz, hawakusaidii ugonjwa lkn msiba watakupa msaada! Tena utashangaa pesa zinatoka wapi, wanaunda kamati ya mazishi, msosi, kina mama nao dk0 wamevaa madera ya sare wote! Yaani utashangaa masuala huwa fasta fasta
Hilo nalo neno maana wasije wakaja na lundo la wasidizi.Jambo la msingi mgonjwa asije na jeshi la uhamiaji ili kupunguza gharama, huenda neema yaja kupitia mgonjwa huyo na ukimkataa utakuwa umeifunga. Chukulia chanya kila jambo, simama imara, amini kwamba kuna njia mbadala katika kila jaribu, piga moyo konde ili ubongo ukuonyeshe njia ya kumudu jambo gumu na siyo kukupa woga ambao unatafsirika kirahisi.
Ukimpokea mgonjwa aidha atakufa au atapona na hayo yatasahaulika lakini kidonda cha kumkataa nduguyo hakitapona haraka katika mioyo ya wazazi na ndugu zako. Usiogope kumpokea mgonjwa na kumlisha sembe kwa matole, ogopa kumkataa mgonjwa ili ulinde bajeti ya wali samaki. Mtoto wa kiume hulia ndani ya moyo wake, huna hali ngumu kama unavyojidhania...wenye hali ngumu wapo na bila shaka hujawaona.
Dah!mkuu hii imekaa vibaya mpaka nakuhurumia-pole sana.Wadau,
Ukoo upo kwenye vikao na maandalizi ya mwisho kabisa ya kumsafirisha baba yangu mkubwa kuja Dar kwa matibabu zaidi baada ya ugonjwa wake kushindikana katika hospital ya mkoa.
Ukoo wamepanga afikie kwangu na mimi ndie nishughulike na masuala ya Muhimbili na hiyo rufaa kwa ujumla, baba amenipigia simu kunijulisha kuhusu mgonjwa kufikia kwangu, hakutaka majadiliano, ni kama amri vile, mzee wangu ni mkoloni hakuna mfano.
Kinachotutisha ni hali ya mgonjwa ilivyo, chances za kupona ni very slim, watotoa taarifa wameniambia kwanza akifika hai Dar basi mungu mkubwa, hivyo nikamgomea mzee kuwa haiwezekani hatuna nafasi.
Mzee akasema tutaona, kwamba anajua ni mke wangu ndio kakataa, sababu anawajua wanawake, hivyo akadai atamsafirisha mgonjwa hivyo hivyo tupende tusipende, akampigia na wife simu akamfokea sana.
Wadau, tunalikataa suala hili kwa sababu wote mnajua hali ilivyo kwa sasa, posho za vikao zimefutwa, mianya yote ya deals imefungwa hapo kazini, naishi kwa mshahara tu ambao nao nilishaukopea hivyo hauji kama ulivyo, sasa kwa hali hii nije nipate msiba hapa which is more likely, maana mgonjwa sasa amevelop kwiki kwiki isiyokatika muda wote.
Gharama za kusafirisha msiba kwenda mkoa wetu kwa coaster ni karibu 4 million, na mimi sina watu kihivyo hapa mjini, haya, bado gharama za hospital, tuseme Mungu ametenda muujiza akafika akalazwa najua gharama zote za hospital wataniachia mimi, maana wanaendelea kufikiria nina hela kama zamani
Wanampigia mke wangu simu na kumtisha kuwa watamtoa kwenye hii ndoa kama mgonjwa akifa, baba kila saa ananipigia simu nitume hiyo nauli ya ndege mgonjwa asafirishwe haraka mimi nakua namchenga.Sasa jambo hili limekua kubwa katika familia na limeleta mzozo mkubwa.
Msaada wenu wa mawazo unahitajika haraka sana.
Mkuu Ambamba!Mkuu zingatia ushauri wa kwanza,
Wauze hata ngo'mbe nk. na wachangishane, ili kukupiga tafu.
Ni kweli hali ni mbaya sana kwa watumishi kwa sasa, maana wengi walichukua mikopo bank wakitegemea deal mbalimbali kuwapiga tafu lakini sasa hali ngumu sana