Hivi nini ambacho raisi huyu amekifanya cha kukufanya uamini kuwa amechukua maamuzi mazito na magumu yanayoweza kuhatarisha usalama wake kiasi kwamba sisi wananchi tumuombee.
Je, ni haya?
1.Kubomoa nyumba za masikini?
2.Kufukuza/kusimamisha watumishi wa umma?
3.Kuwapa grace period wafanyabiashara wakubwa wasiolipa kodi?
4.Kutuoa kauli kali kwa Mawaziri,Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa?
Jamani nisaidieni labda kuna ambayo kaagiza/kayafanya ambayo pengine mimi mwenzuni siyajui kama vile;
1.Kukamata na kufungulia mashitaka wanasiasa wakubwa(vigogo) kwa matumiza mabaya ya madaraka.
2.Kuzuia maslahi ya vigogo
3.Kutishia maslahi ya mataifa makubwa yaliyowekeza hapa nchi kama vile kuagiza kupitia upya mikataba yao na serikali au kuisitisha mikataba hiyo
4.Kuagiza mikataba hiyo ipelekwe bungeni mara moja
5.Kuondoa kinga ya raisi kutoshitakiwa
6.kuagiza uchunguzi mpya juu ya kashifa za Escrow, Kagoda, EPA, Meremeta, n.k.
Mwenezuni sielewi labda kaagiza na haya yafanyiwe kazi ndio maana anaomba tumuombee kwa mungu.[/QUOTE
Muombee afanye hayo unayotaka... . ingekuwa ameshafanya asingesema tumuombee so muombee tu hayo unayoyataka yatatekelezwa.. Pia muombee tu maana yaonekana ni adui yako Na Mungu ameagza muombee adui yako aishi miaka Ming..... Kwahyo ndugu huna budi kumuombea tu