Nini maana ya hiyo picha.

...Kwa maoni yangu ni mshangao tu kwa hao watoto kumuona huyo bwana mkubwa anang'aa akiwA ameweka vitu kwenye uso wake....nahisi hilo eneo hakuna mtu mwenye mwili unaong'aa kama huyo mtu aliyembele yao it tells from sura za watoto unaowaona sielewi kama weusi wao ni kutokana na ukosefu wa maji au vipi???? But pia yawezekana hata huyo mtu mng'aavuna amevaa vitu usoni anashangaa kama katika dunia hii kuna mahali kwenye watoto wenye afya na mtazamo uliofifia kama wale akifananisha na watoto wake nyumbani (angalia sura ya mtoto wa pili toka kushoto mbele).....Ni jukumu la nani kuwafanya watoto hawa warudishe matumaini tena????? HUYU MTU MNG'AAVU MWENYE VITU USONI ANATAKIWA KUTOA MAJIBU....

Mkuu Kipanga, hapo umepigilia kwenye ukweli. Mie niliyeweka hiyo picha nilikuwa nina mtazamo kama wako. watoto wanaonekana hata maji ya kuoga huko hayapatikani. Haiwezekani watoto karibia wote wakawa na mwonekano uleule. Naamini hawa wototo wanawakilisha moja ya matatizo luluki yanayowakabili watanzania.
 
Duh!! jamaa kawiva lakini watoto choka mbaya sana. Sijui anajisikiaje akiona watu choka mbaya namna hii huku yeye akitalii dunia kwenye G-5.....

Nyani Ngabu,
Hiyo kweli ni aibu sana kwa Taifa letu. Na sina hakika Mh. JK baada ya kutembelea eneo hilo alitoa maoni yoyote kuhusu matatizo ambayo hao watoto waliwakilisha.
 
Mkuu Kipanga, hapo umepigilia kwenye ukweli. Mie niliyeweka hiyo picha nilikuwa nina mtazamo kama wako. watoto wanaonekana hata maji ya kuoga huko hayapatikani. Haiwezekani watoto karibia wote wakawa na mwonekano uleule. Naamini hawa wototo wanawakilisha moja ya matatizo luluki yanayowakabili watanzania.

Usikute wanaoga ila wanaogea maji ya kisimani yaliyochanganyika na matope na taka taka nyingine. Sabuni wanayoogea usikute ni mbuni au dizaini kama hiyo. Wanajisugulia madodoki. Usikute lotion hawapaki badala yake wanapaka mafuta ya YU....Lol. Oh well, Miafrika Ndivyo Tulivyo na anayebisha na abishe lakini ukweli utabaki vile vile tu.
 
Kwa wanaojua body language wataweza kuona kwamba JK anawazuga tu watoto lakini mawazo yake hayako nao, hata aliyempa mkono amempa kizugaji tu, amempa mkono lakini hata hamwangalii, anaweza kuwa analia lakini JK hawezi kujua, moreover inaonekana anaangalia past vichwa vya watotot kama vile anasema "Sijui tutamaliza saa nhapi suluba hii nijiondokee".

Unfortunately this is poignantly depicting his entire presidency, he does not have empathy or a care for his people and at this point he cannot wait to be an ex president.

Pundit, heshima Mkuu.
Everything U said it true. I can't comprehend what kind of Prezidaa we have.
Sijui jamaa kama huwa anapata nafasi ya kuangalia picha ambazo hupigwa huko anakopitia. Na hata kama hapati huo mwanya, yeye mwenyewe anaona hali halisi ya Watanzania, sijui anajisikiaje kuona hali ile huku wengine akina Chenge, Rostam, Lowassa, Karamagi , yeye mwenyewe na wengineo wakiendelea kupeta na pesa zetu. That's insane.
 
Kwikwikwikwikwikwiiiiiiii!Sasa hicho kipilipili chenyewe kichana hakipiti do you expect wave itashika?Huyu anahitaji chakula bora nadhani Kikwete angevalia njuga suala la chakula bora mashuleni hawa wanafunzi wangekuwa hata na sura za kuvutia.

Mwezi Aprili mwaka 2007 nilisikia kuna mtu alikuwa amepewa tenda ya kutoa maziwa kwa shule zote za msingi
Tanzania. Lengo likiwa ni kutoa some Vitamins kwa wototo wa shule. Sina hakika kama huo mradi ulikuwa ni Richmond nyingine au vipi. Kuna mtu yeyote ambaye ana Data kuhusu usambazaji wa Maziwa mashuleni? Weka Data hapa.
 
watoto wanawakilisha wananchi wa tanzania: choka mbaya, wamepauka, wana kiu na njaa, hopeless, powerless and confused nk

Rais anawakilisha mafisadi: wamewiva (jua la bongo linawachoma kwa nadra hao), smiling faces, shibe na afya toka utosini hadi nyayoni, ubabe uliochanganyika na unafiki nk
 
Poor Tanzanians! Sijui tunaelekea wapi!!!!
 
Poor Tanzanians! Sijui tunaelekea wapi!!!!

Hukujua tunakwenda RIVASI sasa. Ule mfumo wote kuanzia Ujima hadi hapa tulipo tunaanza kurudi kinyume nyume hadi tutakapoanza kuvaa magome ya miti.
 
Ila naona kama watoto wengi hapo hawana taimu na Kikwete, bali wanajisogeza wasije wakapewa adhabu shuleni; nadhani walilazimishwa kwenda kushikana mikono na JK ili kumkamilishia ziara yake. Hebu angalia, yule wa kwanza anasema ".... hivi huyu msanii naye amekuja hapa kufanya nini na kunikosesha masomo ya leo?" Yule wa nne baada ya aliyeshikana mkono na Kikwete anasema anasema " ....hebu niondolee ujinga hapa msanii wewe." Tena unaona watoto hawa wameweka ndita kweli kweli kuonyesha wasivyofurahia kitendo cha JK kuwapo pale.
 
Nadhani hiyo ndita inatokana na rumba kuwa kali. Wee angalia, hao ni watoto wadogo lakini wanaonekana tayari wameshaanza kuzeeka....gademu!!!
 
Usikute wanaoga ila wanaogea maji ya kisimani yaliyochanganyika na matope na taka taka nyingine. Sabuni wanayoogea usikute ni mbuni au dizaini kama hiyo. Wanajisugulia madodoki. Usikute lotion hawapaki badala yake wanapaka mafuta ya YU....Lol. Oh well, Miafrika Ndivyo Tulivyo na anayebisha na abishe lakini ukweli utabaki vile vile tu.

Si mpaka wawe na hizo sabuni za mbuni na YU. Mkuu inaonekane hujapita mitaani kitambo kidogo, hali ni mbaya kuliko maelezo, tena naona hapa walimchagulia palipo bora kwa standard zetu. Nikawaletea picha za nani, mbona itabidi mfunge hiki kijiwe!
 
Mwenzio huwa naishia Dar tu siku hizi. Huko mikoani sikuwezi tena.
 
Its perfectly simple!!!! Chekechea wakutana na shule ya Msingi!! "Mungu Ibariki Tanzania",Je! Unaukumbuka ule Wimbo??
 
Si mpaka wawe na hizo sabuni za mbuni na YU. Mkuu inaonekane hujapita mitaani kitambo kidogo, hali ni mbaya kuliko maelezo, tena naona hapa walimchagulia palipo bora kwa standard zetu. Nikawaletea picha za nani, mbona itabidi mfunge hiki kijiwe!

halafu watoto waliambiwa kesho lazima kuoga, kusugua meno na kuja shule na unifomu safi.... ukiwaona ktk hali ya halisi unaweza ukajitwika mikono kichwani na kuangua kilio
 
Nimesikia tetesi kwamba walimu wa shule za msingi hawajalipwa mishahara yao. Huyu mkuu, kweli matanuzi yote anayoyafanya, si hizo pesa wawalipe walimu?

JK anasikitisha sana, lakini tulikuwa tunategemea nini toka kwa mtu ambaye jimbo lake la ubunge liko hoi bin taabani kwenye kila kitu?

Tujifunze, kiongozi bora anaonyesha ubora wake kuanzia kwenye familia yake mpaka juu.
 
Anajua popularity yake ipo below average that is why he is travelling alot to boost it up.He is a loser and on the verge ya collapse.
 
Fungua hiyo attachment hapo chini kisha toa maoni yako kulingana na hiyo picha.

Watu wa ikulu wameshindwa kazi, kila anapokwenda jk lazima kuwepo picha jk amepiga na watoto, hizo ni cheap politksi!! wanataka public sympathy, eti pamoja na shutuma nyingi na kuonekana kashindwa kazi ya kuongoza taifa kwa ujasiri, wanataka kuwaonyesha watu wa vijijini waone labda jk anasingiziwa tu, mbona yuko karibu na watu!! hii ndiyo maana yao.

Achen kulazimisha ukarimu hata pasipostahili, jk ana mambo mengi makubwa ya kufikiri na kushughulikia zaidi ya kusalimia watoto, ambao yeye mwenyewe ameshindwa kuwatengenezea mazingira bora ya kuja kufurahia utanzania wao!
 
Back
Top Bottom