Mr nobby
JF-Expert Member
- Aug 25, 2023
- 254
- 516
UT ANIMA P. FRANCISCI TUUS REQUIESCAT"
"MAY YOUR SOUL REST IN PEACE POPE Francis'
"Kaka na dada wapendwa ni kwa huzuni kubwa kwamba sina budi kutangaza kifo cha Baba yetu Mtakatifu Francisko. Saa 01.35 asubuhi ya leo, (Jumatatu 21 Aprili 2025),Askofu wa Roma, Francisko, alirejea nyumbani kwa Baba. Imesikika sauti ya huzuni kutoka kwa Kardinal Farrell"
Mwandishi Revocatus J Ng'oja
Katika historia ya ulimwengu, vifo vya viongozi wakuu wa dini vimekuwa tukio la mshtuko na majonzi makubwa kwa waumini wao.
Lakini linapokuja suala la kifo cha Papa wa Kanisa Katoliki, tukio hilo linakuwa zaidi ya majonzi.
Ni mchakato mzima wa kihistoria unaofuata taratibu za karne nyingi zilizopita.
Sasa hebu tafakari hili, Papa Francis amefariki Leo baada ya kulazwa muda mrefu Toka mwanzoni mwa mwezi Feb. Alikuwa anapumulia mashine, hali yake ilikuwa mbaya sana na dunia nzima ilikua inafuatilia kwa ukaribu huku waumini wa Katoliki zaidi ya bilioni 1.5 wakimwombea.
Lakini baada ya kufariki Leo akiwa na miaka 88, unajua kitafanyika?
Baada Papa kufariki mchakato maalumu unaanza ,Tena ni mchakato wa kihistoria ambao umefuatwa kwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita.
Mara tu baada ya kifo Vatican imeingia katika kipindi kinachoitwa Interregnum,ni kipindi ambacho Kanisa Katoliki linakuwa bila kiongozi mkuu.
Mchakato huo unaanza na uongozi wa Vatican kupitia ofisi maalum inayojulikana kama Camerlengo.
Camerlengo inafanya nini?
- 1- Kuthibitisha kifo cha Papa.
Kiongozi wa Vatican humuita Papa mara tatu kwa jina lake rasmi. Ikiwa hataitika, basi kifo chake kinathibitishwa rasmi na ndicho kimefanyika kabala hawajatangaza kifo chake na baadaye ndipo wakatangaza.
Hata hivyo zamani,taratibu zilihusisha nyundo ndogo ya shaba kupigwa kidogo kwenye paji la uso la marehemu, lakini desturi hii ilisitishwa mwaka 1963.
- 2-Kutangaza Kifo Hicho Kwa Dunia,
Habari za kifo cha Papa hutangazwa rasmi kwa kutumia chombo cha mawasiliano cha Vatican. Ndivyo ilivyofanyika.
Makanisa yote hutangaziwa na kengele maalum hugongwa kama ishara ya maombolezo.
3-Kufunga Ofisi ya Papa,
Vitu vyote vya ofisi ya Papa hufungwa rasmi. Pete ya Papa na muhuri wa Fisherman's huharibiwa, kuashiria mwisho wa utawala wake.
- 4-Kuandaa Mazishi,
Mazishi ya Papa lazima yafanyike kati ya siku nne hadi sita baada ya kifo chake. Kisha, kanisa huingia katika siku tisa za maombolezo rasmi.
Baada ya kifo chake, Papa huzikwa katika makaburi ya St. Peter’s Basilica, isipokuwa kama aliacha wosia wa kuzikwa sehemu nyingine.
Baada ya maombolezo na mazishi, Kanisa linaingia katika hatua muhimu zaidi, kumchagua kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki.
Mchakato huu unaitwa CONCLAVE.
- 5-Conclave Inavyofanyika,
Ndani ya siku 15 hadi 20 baada ya kifo cha Papa, Makardinali wenye umri chini ya miaka 80 hukusanyika Vatican.
Makadinali Hawa wanajifungia ndani ya Kanisa la Sistine,na hakutakuwepo na simu, waandishi wa habari, hata mawasiliano na dunia ya nje hayatakuwepo.
Makadinaki Hawa watapiga kura kwa siri, wakirudia mara kadhaa hadi mmoja wao atakapopata 2/3 ya kura.
Baada ya kura, kinachofuatia ni cha kusisimua zaidi, Kila baada ya mzunguko wa kura, makaratasi yanayotumiwa katika uchaguzi huchomwa moto.
Moshi mweusi ukitoka, inamaanisha hakuna maamuzi bado. (Makaratasi ya kura huchomwa pamoja na kemikali maalum zinazozalisha moshi mweusi.
Kemikali zinazotumika mara nyingi kitaalamu huitwa Sulphur na Resin, ambazo huleta moshi mzito na mweusi unaoonekana kwa mbali).
Moshi mweupe ukitoka, inamaanisha Papa mpya amechaguliwa! (Makaratasi ya kura huchomwa pamoja na kemikali zinazozalisha moshi mweupe.
Kwa kawaida, kemikali hizi ni potassium chlorate, lactose, na pine resin, ambazo husaidia kuchoma karatasi kikamilifu bila kutoa moshi mweusi).
Mara baada ya Papa mpya kuchaguliwa, anatangazwa kwa dunia kwa maneno haya maarufu.
" HABEMUS PAPAM "( Tuna Papa mpya!)
Hapo ndipo ulimwengu mzima husherehekea na safari mpya ya Kanisa Katoliki huanza upya.
Licha ya kifo cha Papa kuwa pigo kubwa kwa waumini wake, mfumo wa Kanisa Katoliki umejengwa kwa namna ya kipekee inayohakikisha kuendelea kwa uongozi bila mgogoro.
Na hiki ndicho kinachokifanya Kanisa Katoliki kuwa moja ya taasisi imara zaidi duniani.
Kwa hivyo BAADA YA kiti Cha Papa Francis kutagzwa rasmi na Vatican Leo , dunia haitasimama. Kanisa litaomboleza, lakini taratibu zake zitahakikisha mrithi wake anapatikana na Kanisa linaendelea kusimama.
Huo ndio uzuri wa historia, taratibu na imani vyote vikifanya kazi kwa usawa.
LIDUMU KANISA TAKATIFU KATOLIKI LA MITUME.
" SANCTAM APOSTOLICAM CATHOLICAM VIVAT"
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WAMILELE UMWANGAZIE PAPA FRANCIS APUMZIKE KWA AMANI.
REQUIES AETERNA DA SIBI DOMINE, AC PERPETUA LUMINIS PAPAE FRANCISCI REQUIESCAT.