SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,683
- 12,707
Huu uzi nautoa kama tahadhari ili kama kuna sehemu ya kusafisha ifanyike haraka. Sitaenda kumnyooshea mtu kidole wala kumlaumu mtu bali ninachotegemea ni wahusika kuangalia mambo kwa jicho la tatu.
Baada ya gemu ya Dodoma Jiji kuahirishwa, Simba ililazimika kukaa siku kadhaa zaidi ya timu nyingine bila kucheza na hili gepu likaiwezesha Yanga kurudi kileleni na kukaa mpaka sasa. Game ya Simba iliyofuata ilikuwa ni dhidi ya Namungo.
Ukiweza kaangalie tena ile game na performance ya mchezaji mmoja mmoja, sijawahi kuona wachezaji wa Simba wote kwa pamoja, mmoja mmoja, wakiwa na game mbaya msimu huu kama game ile. Watu wanalaumu kiwango cha Ngoma kwa game ya jana dhidi ya Azam ila kwenye game ya Namungo alikuwa hovyo kupita maelezo. Asilimia kubwa ya mipira yake ilipotea katika ile game. Hiki hapa chini ndiyo nilichosema wakati game ya Namungo inaendelea.
Kiujumla, performance ya mchezaji mmoja mmoja kwenye mechi na Azam ilikuwa bora kidogo zaidi ya ilivyokuwa mechi na Namungo, ukiacha labda Ngoma na Kibu ambaye touch zake hazikuwa nzuri, ila kilichokuwa hovyo kupita maelezo ni uchezaji wa timu nzima kwa pamoja.
Yaani beki ilikuwa inakatika kupita maelezo, watu hawarudi nyuma kukaba, pumzi ilikata, eneo la kati na pembeni lilikuwa na mapengo, ungeweza kudhani Simba ilikuwa inacheza na wachezaji 8 uwanjani. Fadlu naye akajisahau "kumaliza mchezo" baada ya kupata goli la pili. Msimu huu hii ni mara ya kwanza hafanyi sub wakati ndiyo mechi ya kwanza ya Simba msimu mzima ambayo timu ilionekana kukata moto. Hii inafikirisha sana.
Swali langu, nini kimeitokea timu ya Simba baada ya kuahirishwa ile mechi dhidi ya Dodoma Jiji? Mbona kama kuna kitu kimedrop ghafla.

Kwenye game ya Azam ndiyo kabisa, niliona muendelezo wa poor performance ya Ngoma kama ilivyokuwa dhidi ya Namungo na pasi yake mbovu ndiyo ilizaa goli la kwanza la Azam.Hii mechi imewakataa Ngoma na Janshalewa. Wakiendelea na hii game, Simba itapata shida.