Nini cha kuzingatia ukitaka kununua gari kwa mtu (used)?

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
25,079
71,164
Wakuu.

Mbali na kuagiza gari kutoka nje ya nchi, au kununua showroom kuna option ya tatu ya kununua gari ambalo Mtanzania mwenzako analitumia.

Hii inaweza kua njia salama zaidi lakini pia ya hatari zaidi usipokua makini.

Sasa kuna vitu vya kuzingatia unavyotaka kununua, tutaviweka kwenye hatua kumi (10), ila sio zote za msingi.

1. Panga budget ya kununua na service.

Lazima uwe na budget ya kununulia gari usiseme tu nataka gari fulani. Budget yako ikumbuke na gharama za matengenezo baada ya kununua.

Mfano una top million 10, unaweza tafuta gari la million 8.5 max na kutenga mil 1.5 kwa service ndogo ndogo.

Kumbuka, usimtajie budget yako muuzaji. Yeye atataja yake na ww utaangalia window ya kunegotiate.

2. Kua na option za magari na wauzaji

Hapa naongelea unataka sedan, basi uwe na option ata ya sedans tatu mfano Mark X, Honda Accord au Crown, hii itakusaidia usipelekeshwe na muuzaji.

Au kama unataka Crown tu, basi uwe na options za wauzaji ata wawili au watatu.

Wauzaji wengi wa magari private tunawapata Facebook groups, ila tegemea watu wa aina mbalimbali kwenye social media kuanzia madalali hadi mawinga uko.

3. Nenda kakague gari na fundi

Ukishafanya selection ya wauzaji, nenda na fundi au mtaalamu kukagua gari.

Wewe utakagua muonekano, ndani, chini, rangi, kutu, leakages, nk vitu ambavyo rahisi kuona kwa macho.

Fundi muachie afanye utaalamu wake, kwa kuangalia vitu vyake na akiwa na kifaa cha diagnosis machine itakua safi zaidi.

Ukiona dalili zozote za kufichwa madhambi kama vile kusafisha engine kwa mafuta, kupaka rangi, kunyooshwa bodi, airbag kulipuka basi achana nalo.

4. Gari inakaguliwa asubuhi

Usikague gari mchana au eti anasema tukutane sehemu flani nakuja na gari ukague. No. Weka appointment.

Nakuja Jumamosi saa 1 asubuhi kukagua gari.

Hapa tunaenda test cold start. Gari likiwa na engine ya moto linaficha mengi sana. Hakikisha kabla hamjawasha gari funueni bornet afu angalia engine kama ya moto. Kama ya moto itawadanganya.

Pia gari likiwa limepark muda mrefu ni rahisi kuona leakages za oil, ATF au coolant, ata kama ni ndogo sana.

5. Test drive wewe mwenyewe

Natumai unajua kuendesha. Basi weka ata wese la elfu 10 hafu endesha, tafuta sehemu zenye kilima kirefu utaona gari kama inaangaika na pili tafuta sehemu iliyonyooka urmdeshe angalau 80 km/h.

Kwa mfano, kwa Dar uwa napendelea kilima cha kwenda UDSM kutokea geti maji au kwenda UDSM kutokea Msewe. Vinanionesha jinsi gari linavyoangaika kwenye mlima kubadirisha gear. Mishtuko ikiwa mingi ni redflag.

Kuna magari yakifika speed 60+ km/h yanaanza kutetemeka, sababu zinaweza kua nyingi, ila nalo litanipa redflag.

6. Kagua documents

Ukiridhia na ivyo vya juu, check documents kama zinaendana na gari mfano chasis no (VIN no) rangi ownership etc.

7. Malipo yafanyike bank

Usifanye cash. Ni salama kwako na kwa biashara yenu. Akupe account ukalipie. Akileta story za cash kataa.

8. Mkataba na ID zenu kwaajili ya kubadirisha card

Hii ni final stages mtakua na mkataba wa mauziano ambao utakusaidia wakati wa kubadirisha umiliki wa gari. Usisahau ID esp NIDA au leseni kubadirishana copy.

9. Fanya service kubwa

Ukishamiliki gari, sasa chukua ile pesa uliotenga ufanye service.

Badirisha oil, ATF, pia akague fundi vimiminika vingine kama vilainishi vya steering, brek fluids, coolant nk.

Pia kagua breki, sunspensions nk. Unaweza fanya wheel balance and alignment sio bei sana.

Na mwisho, ipeleke carwash kubwa watoe uchafu na gundu zote.

10. Record kila unachofanya kwenye gari

Kama utaweza unaweza kua na service & maintenance log book kwaajili ya kurecord vitu unavyoifanyia gari lako na gharama zake.

Itakusaidia kutrack gharama za uendeshaji wa gari na kujua ni muda gani wa kufanya service.

Unaweza kutumia ata baadhi ya Apps kwenye simu zinaweza record.

Additional:

  • Usinunue gari ambalo linatatizo hafu muuzaji akakudanganya eti iki kutengeneza laki 2 tu. Yaani usijaribu kabisa. Muache atengeneze yeye.

  • Kama ni gari lako la kwanza jipe muda. Mawazo yakija leo ya kununua, take time ata miezi minne kabla ya kufanya maamuzi.

  • Pia ata kwa wazoefu, gari kununua sio kitu cha haraka. Si wengine waoga, kununua simu tu research week nzima, sasa imagine gari.

  • Na pia kwa wanunuaji wa kwanza, fikiria issue ya parking, nayo sio jambo dogo.

Vipi izo, anaeweza kuongezea zaidi karibu.

Poleni kwa uzi mrefu. Pamoja!
 
Hivi shida hua ni nini? Kuna prado hapa inafanya hivyoo 65km kwenda 70km/h inatetemeka halafu ukivuka 75 inakua safi tu
Kuna uwezekano happ 65-70 kuna kubadirika gear. Angalia mshale wa RPM ukifika hapo unabehave vipi?

Kama issue ni iyo hapo kuna issue kwenye gearbox ila sio kubwa wala ndogo, nisikutishe, unaweza anza kwa kubadirisha ATF.
 
Utest kwa kuendesha gari ambayo hujalipia?? Wakati utakapoendesha ikitokea ajali utanunua screpa au itakuaje? Hebu wajuvi mnieleweshe nijifunze jambo pls
Gari ina bima. Mbona iko wazi. Labda muuzaji awe anaficha kitu ila ukimuonesha leseni kwann asikuruhusu.
 
Wakuu.

Mbali na kuagiza gari kutoka nje ya nchi, au kununua showroom kuna option ya tatu ya kununua gari ambalo Mtanzania mwenzako analitumia.

Hii inaweza kua njia salama zaidi lakini pia ya hatari zaidi usipokua makini.

Sasa kuna vitu vya kuzingatia unavyotaka kununua, tutaviweka kwenye hatua kumi (10), ila sio zote za msingi.

1. Panga budget ya kununua na service.

Lazima uwe na budget ya kununulia gari usiseme tu nataka gari fulani. Budget yako ikumbuke na gharama za matengenezo baada ya kununua.

Mfano una top million 10, unaweza tafuta gari la million 8.5 max na kutenga mil 1.5 kwa service ndogo ndogo.

Kumbuka, usimtajie budget yako muuzaji. Yeye atataja yake na ww utaangalia window ya kunegotiate.

2. Kua na option za magari na wauzaji

Hapa naongelea unataka sedan, basi uwe na option ata ya sedans tatu mfano Mark X, Honda Accord au Crown, hii itakusaidia usipelekeshwe na muuzaji.

Au kama unataka Crown tu, basi uwe na options za wauzaji ata wawili au watatu.

Wauzaji wengi wa magari private tunawapata Facebook groups, ila tegemea watu wa aina mbalimbali kwenye social media kuanzia madalali hadi mawinga uko.

3. Nenda kakague gari na fundi

Ukishafanya selection ya wauzaji, nenda na fundi au mtaalamu kukagua gari.

Wewe utakagua muonekano, ndani, chini, rangi, kutu, leakages, nk vitu ambavyo rahisi kuona kwa macho.

Fundi muachie afanye utaalamu wake, kwa kuangalia vitu vyake na akiwa na kifaa cha diagnosis machine itakua safi zaidi.

Ukiona dalili zozote za kufichwa madhambi kama vile kusafisha engine kwa mafuta, kupaka rangi, kunyooshwa bodi, airbag kulipuka basi achana nalo.

4. Gari inakaguliwa asubuhi

Usikague gari mchana au eti anasema tukutane sehemu flani nakuja na gari ukague. No. Weka appointment.

Nakuja Jumamosi saa 1 asubuhi kukagua gari.

Hapa tunaenda test cold start. Gari likiwa na engine ya moto linaficha mengi sana. Hakikisha kabla hamjawasha gari funueni bornet afu angalia engine kama ya moto. Kama ya moto itawadanganya.

Pia gari likiwa limepark muda mrefu ni rahisi kuona leakages za oil, ATF au coolant, ata kama ni ndogo sana.

5. Test drive wewe mwenyewe

Natumai unajua kuendesha. Basi weka ata wese la elfu 10 hafu endesha, tafuta sehemu zenye kilima kirefu utaona gari kama inaangaika na pili tafuta sehemu iliyonyooka urmdeshe angalau 80 km/h.

Kwa mfano, kwa Dar uwa napendelea kilima cha kwenda UDSM kutokea geti maji au kwenda UDSM kutokea Msewe. Vinanionesha jinsi gari linavyoangaika kwenye mlima kubadirisha gear. Mishtuko ikiwa mingi ni redflag.

Kuna magari yakifika speed 60+ km/h yanaanza kutetemeka, sababu zinaweza kua nyingi, ila nalo litanipa redflag.

6. Kagua documents

Ukiridhia na ivyo vya juu, check documents kama zinaendana na gari mfano chasis no (VIN no) rangi ownership etc.

7. Malipo yafanyike bank

Usifanye cash. Ni salama kwako na kwa biashara yenu. Akupe account ukalipie. Akileta story za cash kataa.

8. Mkataba na ID zenu kwaajili ya kubadirisha card

Hii ni final stages mtakua na mkataba wa mauziano ambao utakusaidia wakati wa kubadirisha umiliki wa gari. Usisahau ID esp NIDA au leseni kubadirishana copy.

9. Fanya service kubwa

Ukishamiliki gari, sasa chukua ile pesa uliotenga ufanye service.

Badirisha oil, ATF, pia akague fundi vimiminika vingine kama vilainishi vya steering, brek fluids, coolant nk.

Pia kagua breki, sunspensions nk. Unaweza fanya wheel balance and alignment sio bei sana.

Na mwisho, ipeleke carwash kubwa watoe uchafu na gundu zote.

10. Record kila unachofanya kwenye gari

Kama utaweza unaweza kua na service & maintenance log book kwaajili ya kurecord vitu unavyoifanyia gari lako na gharama zake.

Itakusaidia kutrack gharama za uendeshaji wa gari na kujua ni muda gani wa kufanya service.

Unaweza kutumia ata baadhi ya Apps kwenye simu zinaweza record.

Additional:

  • Usinunue gari ambalo linatatizo hafu muuzaji akakudanganya eti iki kutengeneza laki 2 tu. Yaani usijaribu kabisa. Muache atengeneze yeye.

  • Kama ni gari lako la kwanza jipe muda. Mawazo yakija leo ya kununua, take time ata miezi minne kabla ya kufanya maamuzi.

  • Pia ata kwa wazoefu, gari kununua sio kitu cha haraka. Si wengine waoga, kununua simu tu research week nzima, sasa imagine gari.

  • Na pia kwa wanunuaji wa kwanza, fikiria issue ya parking, nayo sio jambo dogo.

Vipi izo, anaeweza kuongezea zaidi karibu.

Poleni kwa uzi mrefu. Pamoja!
Dah hapa safi saana naendesha gari mwaka wa tano sasa ila nimejifunza vingi na hii n kwasababu boss anamaliza kila kitu mwenyew mm n ufunguo stater pedo twende mdundo
 
Hahaha tosha kabisa iyo mbona.
 
11. Kabla ya kununua jaribu kufuatilia gharama za uendeshaji za gari husika, bei ya gari isikuchanganye.

Kuna gari zinauzwa mkononi kwa bei kitonga sana, ila ukija kufuatilia kiundani gharama za uendeshaji kama vile spea, mafuta n.k ni kubwa. Sasa bei ya gari inakuchanganya unaenda pupa.
 
Brevis....
 
Back
Top Bottom