Nini cha kufanya pale tu unapoingia katika soko la ajira

BWANA WANGU

JF-Expert Member
Jul 10, 2018
332
770
Hii nakala nime copy kutoka moja ya mitandao ya kijamii.

MWANDISHI: Iddy Makengo, 11 Sep 2017.

NINI CHA KUFANYA PALE TU UNAPOINGIA KATIKA SOKO LA AJIRA!

Miaka kama nane hivi iliyopita nilikua katika soko la ajira, ingawa sikusumbuka sana kwa maana ya kukaa muda mrefu bila ajira lakini nafahamu kazi iliyopo katika kutafuta ajira. Ni kazi ngumu hasa katika kipindi hiki ambacho ajira ni chache na nyingi hutolewa kwa kujuana, kuna wasomi wengi mtaani kuliko unavyodhani hivyo kama msomi mbali na cheti chako unapaswa kufanya kitu cha ziada ili kuhakikisha unaajiriwa.

Kuna mambo ambayo sikuyajua kipindi hicho, ambayo naamini kama ningeyajua yangenirahisishia kupata kazi, hivyo katika makala hii nitafundisha nini cha kufanya unapoingia katika soko la ajira? Hapa siangalii elimu yako, siangalii kile ulichosomea lakini kama umeingia kwenye soko la ajira, ndiyo unaingia au ulishakaa muda mrefu na bado unahangaika na bahasha ya kaki naamini mambo haya yatakusaidia kuajirika mapema.

(1) Amua Unataka Kufanya Nini; Hiki ndiyo kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kukifanya, kuna watu wapo kwenye soko la ajira lakini bado wanataka kufanya Biashara, bado hawajui kama wanataka kuendelea na masomo na mambo mengine kama hayo. Hatua ya kwanza kabisa ya kupata ajira ni kuamua kua unataka kuajiriwa, ni kitu ambacho unatakiwa ukiseme, ukiwaze na kikae akilini kwako, kwamba ujione kama wewe ni kuajiriwa tu.

Najua ni vizuri kuwaza na biashara, kuwaza kujiajiri, lakini kuna wale watu ambao wanaona huko sio kwao na lao pekee ni kuajiriwa. Sasa hembu fanya maamuzi hayo sasa, uko kiwenye soko la ajira, amua kama unataka kuajiriwa, kujiajiri au kurudi kuendelea na masomo, acha kuwa mguu nnje mguu ndani, ni rahisi kukata tama kama hujui uantaka nini!

(2) Amua Unataka Kuajiriwa Wapi; Najua utashangaa, ajira zilivyo ngumu hivi nipange pa kuajiriwa, watu wengi wakikuomba uwaunganishe kupata kazi ukiwauliza wanataka kazi gani utasikia kazi yoyote tu, wamesomea kitu flani lakini wanatafuta kazi yoyote.

Hili ni kosa la kwanza unalolifanya, kutokujua unataka nini. Nikweli unatakiwa usichague kazi kama nitakavyofafanua mbeleni, lakini nilazima uwe na vipaumbele vyako.
Sasa kama uko kwenye soko la ajira, hembu orodhesha sehemu kama tano hivi ambazo unatamani kufanya kazi, unatamani wakuajiri na pia orodhesha kama unataka kuajiriwa kama nani?

Kwamba kozi uliyosomea inaweza kuwa inakupa mwanya wa kufanya mambo mbalimbali, chagua. Mfano sema nataka kuwa mhasibi wa TRA, Banki X, Kampuni Y na nyingine, tafuta tano ambazo unaona kweli unaweza kupata ajira, hapa usijali kama wametangaza ama la, wewe tafuta tu.
Nikitu chako ambacho unajiwekea kwamba mimi nataka niajiriwe sehemu flani, ujue kabisa, na kama unaona sehemu husika ni ngumu kupata ajira, orodhesha nyingine na nyingine.

Ninachotaka hapa ni wewe kujitambua, kujua unataka nini ili iwe rahisi kukipata unachokitaka. Ujue unataka kuwa nani na sehemu flani, suala la kuipata hiyo ajira ni jingine lakini kwanza ujue unaitaka.

(3) Angalia Mfumo Wao Wa Uajiri/Fanya Utafiti; Baada ya kuorodhesha sehemu ambazo unatamani kuajiriwa, hembu sasa angalia mfumo wa uajiri katika sehemu hiyo. Hapa nikimaanisha kwamba kuna wakati mwingine unaweza kutaka kufanya kazi sehemu lakini ukakuta kuwa uajiri wao ni wa baada ya miaka flani hivyo huwezi kupata, ni mgumu au unahusisha mlolongo mrefu hivyo huwezi kupata kwa urahisi.

Kwa mfano, serikali na mashirika mengi ya umma huajiri kwa kutumia Bodi ya Ajira, nafasi zake hutangazwa jumla na ni mpaka zitangazwe, hivyo kwa kujua hivyo basi hutapoteza muda kusubiria sana huko mpaka pale zitakapotangazwa. Lakini kuna taasisi ambazo huajiri kupitia makao makuu, nyingine katika matawi na vitu kama hivyo.

Hembu pitia ile orodha yako, ingia Google, uliza watu, wafanyakazi, katika mitandao ujue hivi nafasi za kazi katikia makampuni hayo zikoje. Acha kuwa mtu wa kusubiri mpaka zitangazwe, kuna kampuni nyingi tu ambazo hazitangazi, kama ukijua basi unaweza kuomba moja kwa moja bila kusubiri matangazo na kupata. Lakini kuna wengine huajiri watu wanaojitolea tu, hivyo ukijua wanaajiri vipi nirahisi kufanya kama wanvayotaka na kuajiriwa nazo.

(4) Tafuta Uwezekano Wa Kujitolea Unapotaka Kuajiriwa; Kama huna ajira, upo kwenye soko la ajira hembu acha kukaa nyumbani, si ushaamua kuajiriwa basi hembu anza kutafuta nafasi za kujitolea. Iko hivi wakati mwingine kampuni haziajiri si kwasababu hazihitaji watu hapana bali kutokana na uwezo, hivyo kama ukiamua kujitolea, bila kulipwa basi unaweza kupata nafasi kuliko kuomba kuajiriwa.

Unapojitolea sehemu ni kama kulazimisha usahili kwani nirahisi kukuajiri kama wakiona una tija kwao. Hata kama hakuna nafasi lakini watakutafutia na hapa ndiyo inakuja kwanini mwanzoni nilikuambia uamue kama unataka kuajiriwa au la, unapojitolea watu wengi hufanya hivyo wakiatafuta pesa za kujikimu, hapana kujitolea kunapaswa kuwa kujitolea kwamba hutaki malipo labda wakiamua wao.

Jiltolee ukiwa na lengo la kutengeneza uzoefu na kupata hiyo ajira. Sasa kama lengo ni kupata uzoefu kuwa makini na sehemu unayojitolea, je wanaweza kukuajiri au hata kupendekeza uajiriwe? Kama umefanya utafiti na ukajua mfumo wao wa ajira basi utajua kama ajira zinatoka makao makuu au la, na kama ni makao makuu je pale unapojitolea wanaweza kupendekeza jina lako kuwa unafanya vizuri!
Pitia ile list yako ya kampuni uanzotaka zikuajiri, chambua zile ambazo ajira zake hutoka kwenye tawi, makao makuu, angalia ni zipi ambazo kama ukijitolea na ukafanya vizuri basi wanaweza kukuajri hapohapo. Anza na hizo, andika barua nyingi tu kwa kila kampuni ambayo unatamani ikuajiri, kuomba kujitolea, waambia kwanini uantaka kujitolea na sababu kubwa inapaswa kuwa ni kujifunza zaidi, kuchangia na kupata uzoefu, usitaje pesa katika kujitolea.

(5) Tafuta Kitu Chochote Cha Kufanya Popote; Kama umemua kuajriwa basi usikae tu nyumbani hakuna swali gumu kama kuulizwa kua miaka yote hiyo ulikua unafanya nini na ukasema ulikua tu nyumbani. Inawezekana katika zile kampunia ambazo ungependa wakuajiri ulikosa kazi, ukakosa kujitolea, basi angalia nyingine, angalia ambayo iko karibu, jitolee bila kujali ukubwa wake, wanweza kukuajiri au la.

Unapokua unafanya kazi tofauti na kukaa nyumbani tu, hata kama hulipwi lakini unakutana na watu ambao wanafanya kazi, ambao wanajuana na watu wanaofanya kazi, nirahisi kupata mtu wa kukuunganisha ukiwa kazini kuliko ukiwa nyumbani. Nyumbani utakutana na watu wale wale kila siku ambao washakuchoka lakini ukitafuta sehemu hata kama si ya hadhi yako utakutana na watu wapia watakupanua akili na kukufungulai njia nyingine.

(6) Tuma Maombi/Peleka CV Hata Bila Tangazo; Kuna watu wanasubiri matangazo ya ajira ndiyo watume barua, hapana, nilishasema unatakiwa kujua unataka kuajiriwa wapi, unataka nafasi gani hivyo kama uko kwenye soko la ajira hembu usisubirii kutangazwa kwa nafasi hasa katika mashirika binafsi. Hembu tuma CV yako, ishi katika mitandao kuangalia nafasi mpya kila siku na tuma CV zako.

Uzuri wa teknolojia nikua huhangaiki sana, ukishaandika barua yako moja kazi ni kuiedit tu anauani, naweza kuomba nafasi za kazi katika kampuni 100 ndani ya saa moja ukitumia email tu. Hivyo hembu tuma maombi kila sehemu bila kujali kama nafasi zipo au la, hii itawafanya waone CV zako na hata nafasi ikijtokeza wakutafute. Iko hivi kama nafasi hazijatangazwa ni watuwa chahe huomba kazi hivyo nirahisi barua yako kuonekana kuliko kusubiri nafasi zikishatangazwa kila mtu anaomba ndiyo uombe.

(7) Tafuta Watu Wa Kujuana Nao Kule Unapotaka Kuajiriwa; Kazi nyingi siku hizi kutolewa kwa kujuana, hivyo nilazima na wewe uwe na mtu wa kumjua katika sehemu unayotaka kuomba kazi. Katika zile kampuni zako, hasa zile ambazo unajua utaratibu wao wa kuajiri si mgumu sana hembu anza kutafuta mtu wa kumjua huko, anza kutafuta mtu yoyote bila kujali kama ni Bosi au mtu wa kawaida.

Anza na watu wa chini, wakati unapaleka barua yako ya maombi ongea vizuri na mlinzi, Dada wa mapokezi au mhudumu ambaye utakutana naye. Lakini pia tumia mitandao ya kijamii kutafuta watuwa naoafanya kazi sehemu unazotaka kuajiriwa hata kama hujatuma maombi na huu ndiyo umuhimu wa kujua mapema unataka nini. Kumbuka haijalishi kama wana nafasi za kukuajiri, hapana kuwa na mtu wa ndani ni muhimu kwa taarifa.

Lakini kuna barua nyingi huandikwa, nyingine hazizomwi kabisa hivyo kama unajuana na mlinzi mhudumu au mtu yeyote mbali na kukupa taarifa juu ya ushaili, kwmaba unakuaje, watu gani wanafnya na vitu kama hivyo anaweza kusaidia katika barua yako kuhakikisha inafika sehemu slaama, sheemua mabyo itasomwa na hata kuitwa katika ushaili na wewe kufanya kazi ya kuonyesha uwezo wako ili upate ajira.
Nimalizie kwa kusema, unapoingia katika soko la ajira usisubiri mpaka kuona tangazo ndiyo uanze kufanya maandalizi, hapana nilazima ufanye maamuzi, ujiandae na kubwa kabisa usiwe mtu wa kukaa tu kusubiri matokeo, pambana, changamka na angalia fursa, usikubali kukaa tu nyumbani, jitolee hata kama ni katika kataasisi kadogo ambako hakalipi lakini uwe tu unafanya kitu, nirahisi kuajirika ukiwa unafanya kazi kuliko ukiwa nyumbani.

21552098_2030473580556376_1413000172646590203_o.jpg

NOTE: ONGEZEA NA ZAKO KAMA UNAHISI ZITAKUWA MSAADA KWA WENGINE.
 
Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom