Ninajuta kwa niliyoyafanya

Najuta kwanini nimechangia huu uzi wa mpuuzi mmoja

Mkuu unatamani kuwa "ke"?

uploadfromtaptalk1462359468695.png
 
Nimependa ID yako tu aiseeee.....
Kuhusu majuto anaitwa mjukuu.
Kubwa songa mbele na anza kama haujui kama uliwahi kukosea, songa mbele na kaza kwa bidii huku ukitafuta kazi na Mungu atakufungilia milango.
Bila shaka umepata funzo
 
Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 25, ni mhitimu wa shahada ya kwanza katika chuo kimoja hapa Tanzania, sijaolewa na kwa dini mimi ni mkristo wa kuzakliwa na kubatizwa.

Katika maisha yapo mengi ambayo mtu unaweza kuyafanya na baadae ukajutia kwa nini umeyafanya na akili gani imekutuma uyafanye, binafsi najuta kwani nimekuwa mpumbavu kiasi hiki, najuta kwa nini nilifanya haya yote na kwa akili gani ilinituma niyafanye haya, inawezekana May be it was not planned but why I did this?

Nakumbuka nikiwa secondary nilikutana na handsome boy mmoja ambaye namfahamu hadi kwao, sikujua intention yake by then but I think nilikuwa mtoto. huyu mkaka aliniita sehemu mbalimbali nilikubali kuwa nakutana nae and the guy was very decent til now the guy is decent, hakuwahi kunionesha kama ananitaka kimapenzi kwa kipindi chote ambacho nimekuwa naye, alikuwa ananisaidia sana by then na soon b aada ya kuingia chuo, aliniomba tuwe wapenzi, sikukubali wala sikukataa, nilibaki katikatikati ila nilikuwa naendeshwa na mkumbo wa shule sababu sikujua kama ule muda was right for to make a very huge decesion.

Nilikubali baadae lakini nilibadilishwa sana na upepo wa chuo sababu niliwekeza kwenye bata zaidi bila ya kuangalia mbele yangu, baadae niliamua kumkataa kabisa huyu kaka sababu hakuwa karibu na mimi na kingine nilipata watu wengine ambao walikuwa karibu na mimi na nilikuwa napewa pesa ya kutosha so to me life nililiona zuri sana. yule kaka hakutaka sana malumbano na mimi na baada ya kugundua aliamua kuendelea na maisha yake na naskia ameoa tayari.

Maisha yanaonekana magumu sana kwangu soon baada ya kumaliza chuo na kurudi nyumbani, ueklekeo umebadirika kabisa na sijui mwisho wake ni upi, kama kaka huyu atasoma haya maneno yangu na kuhisi machungu yangu naomba sana anisamehe kwa yote, I wish nirudishe wakati nyuma, kampani na wale wote walionidanganya hawapo tena karibu yangu, nimekaa nyumbani hata kazi sina, sina kitu na sina pakujishikiza, I feel so much pain.

Kitu kingine kinachoniumiza zaidi tena sana naskia yule kaka amefanikiwa sana kwa sasa, napata wakati mgumu sana kama nitapata mtu mwenye maisha ya upendo na mazuri kama yeye, marafiki zangu kila nikiomba ushauri wako wananisema na kunilaumu, najua nishakosea ila naomba ndugu zangu mnishauri nifanye nini? mimi sio wa kwanza kukosea, maisha najua yataendelea lakini je kwa style ipi?

Najuta sana na kila nikisikia mtu anamuongelea huyu kaka naskia kama nataka kupasuka, nikialikwa harusini nashindwa kwenda sababu nahisi nayeye atakuwepo kwani asilimia kubwa ya watu anaowafahamu nawajua pia, nina wakati mgumu sana naomba mnishauri


Wengi tulijuta hivo hivo, baada ya furaha ni majuto.
Hapo mwanzo ulimuona hakuwa na maisha mazuri na hukumtaka?
Kwahiyo sasa umemuona ana maisha mazuri ndio una muwaza na unamtaka?
Inawezekana huyo kama ana maisha mazuri kwa vile anae mke mwenye akili mzuri.

Mimi nilipenda maisha mazuri, ila nikagundua maisha mazuri inabidi uyatafute mwenyewe, sio utafutiwe na mwanaume au mtu.

Ndio maana wanakusema,
jitambue kwanza ukitoka hapo chapa kazi.
watu wenye tamaa ya kuishi maisha mazuri bila kutumia nguvu zao na akili zao wanaishi kwa pain sana tu bi dada.

Wengi yametukuta kama hayo, kweli ni utoto tu. Nilipofika miaka 30, ndio nilijigundua kuwa nilikuwa mpumbavu sana. Nilikuwa na watoto 2, sikua na pa kushika, nilikuwa nalia tu nikiwaza.

Ushauri wangu, kimbia mji, amia mbali na marafiki zako, jamaa na marafiki maneno yao yanaweza kukumiza zaidi na wakakufanya ujione mpumbavu zaidi, tafuta shule mbali na hapo ukaongeze elimu, na ukaanze maisha mapya na marafiki wapya. Husipende wakutembelee marafiki wa zamani. Huku unasoma azisha biashara, hata benki kakope pesa, ukiona mwanaume anakupenda na anataka kukuoa kubali, maisha mazuri munayatafuta wote kama haujui. Kama unataka uwe kula kulala, utaishi kwa pain hivo hivo, sababu wanaume watakukimbia
 
Ni kwamba unajuta kwasababu "boy" wako kafanikiwa na wewe huna mbele wala nyuma? Au unajuta kwasababu sasa unafeel kumpenda na yeye tayari ana mwingine? Nimeshindwa kuelewa. Pole!
Hili nelo "boy" linasound kama ni kijana chini ya miaka 18.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom