malembeka18
JF-Expert Member
- Jan 26, 2018
- 3,122
- 3,437
Wakuu nimebangaiza nimefanikiwa kuweka Milioni 35 nataka kuingia katika biashara Kariakoo, nifanye biashara gani?
Michango ya wadau
Zaidi soma>>Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)
Michango ya wadau
Hayo mambo ya kununua nafaka na kuzitunza store, yalishapitwa na wakati, utakuja kulia!! Siku hizi unakuta karibia kila mwaka kuna mvua za kutosha, hivyo mavuno ni mengi, usitegemee bei kupanda ki vile!! Msimu huu waliotunza mahindi wanalia, walinunua gunia kwa sh.50,000 leo hii mtu anataka alinunue kwa 40,000!!! Kwa hiyo pesa yako huku huku kwenye mazao unaweza pata net profit ya hadi milioni 3/ kwa wiki!! Ni kujua chanels tu. Hutajutia
Habari Mkuu. Kwa mawazo yangu ingia kwenye biashara ya vyombo. Tafuta fremu mitaa ya sikukuu/aggrey (kodi 1-2m miezi 6 hapo 10m imeisha)
Shelves za kuwekea mzigo, feni, taa n.k kama 1 m.
Anza kujuana na supplier wa vitu vya nyumbani na vyombo. I.e ailyons, aborder, zunne, kenwood, west point, na wauzaji wa vyombo kwa jumla.
Fuatilia Tin na Lesen na mashine. Tafuta kijana wa kukusaidia kazi. Ingia mzigoni.
Hapo kwa siku unaweza make faida 70,000 - 200,000 na kuendelea.
Ukijiongeza ukafungua page social media, ukawa na group whatsapp utauza sana
Nauboresha huu ushauri...maana hapa nod kuna hela.
Mkuu kwa pesa yako hiyo fanya hivi.
Tafuta mji ambao ndo unaanza kukua au umekua ila huduma za afya bado hazijakua.
Tafuta nyumba kubwa tu kwa miji kama hiyo kodi unaweza kukuta kwa mwezi nyumba nzima haizidi laki 3.
Baada ya kulipa kodi labda ya mwaka mzima sawa labda na milioni 3.6(hapa lipa kishika uchumba kwanza labda laki 2 kabla ya kulipa kodi).
Nenda manispaa onana na DMO,afanya mpango akakague jengo na mazingira akipitisha.
Fanya ukarabati utakao ambiwa nafikiri kwa nyumba iliyokamilika hautamaliza 5M
Hakikisha mazingira yanavutia,nunua na vifaa sio lazima ununue vipya kuna used kibao vilivyo na hali nzuri kwa gharama nafuu..weka huduma ya dispensary yenye RCH ndani yake...huduma ziwe nzuri na bei ya kawaida...ukiwa na uwezo weka na meno na nunua Ultrasound ya bei poa hata ya milioni 10.
Tafuta wafanyakazi wachache wenye uzoefu kisha kaa mwenye golini wanapolipia ndani ya mwaka utakua mtu mwingine na huduma zikiwa bomba bro utapiga hela mpaka basi.
Mfano mdogo nakupa Dawa kama Doxcy boksi linauzwa 6400 ambao kila boksi linakaa na blister 10 na kila blister moja ina vidonge kumi sawa na vidonge 100.Kwahiyo kwenye boksi moja unatoa dozi 10 dispensary ninayofanya kazi dozi moja wanauza elfu 4 hivyo kwa kila boksi unatoa elfu 40.Drip unazoziona bei ya jumla unanunua 850-1000 ila mtu utamuwekea kwa elfu 10 hapo ukitoa giving set na scalp vein faida yako ni 8000.
Bado sikwambii kwenye kitengo cha Dental jino kung'oa ni elfu 10 ,mng'oaji anaweza chukua elfu 3 ,ukitoa gharama ya ganzi na syringe unakuta unabaki na faida ya elfu 6,,,bado kwemye ultrasound na RCH bado kuna kesi za Kusafisha ,kutahiri nk.
Bro biashara ya afya inalipa hasa ukiwa mjanja na akili nyingi inalipa sana.
Nb:ukishindwa Dispensary basi funguo maabara ya kisasa au pharmacy ule maisha.
Zaidi soma>>Baadhi ya njia unazoweza kutumia kupata wazo bora la biashara (Business Idea)