Nina mkosi wa kudhulumiwa

Nilifanya kazi mwezi mmoja na nusu jamaa akanidhulumisha laki 7 ivi...

laptop accessories yule mwamba 150,000 yangu mpaka Leo.

we Mzee wa makamo (50 years almost) niliekutumia elfu 20 kisa unadai gari Yako imepata hitilafu miezi mitatu iliopita nikusaidie hujalipa mpaka Leo ungejua navyoitafuta hela.

Ile kazi ya uviko na mliopita na hela zetu (150,000) fresh tu ....

Dogo hivyo viatu ulivyonidhulumu hiyo elfu 30 na Mpira wenyewe hutoboi shabbash ......

ndugu mtumishi , naww pia rafiki yangu Ile elfu 50 mpaka tusomeane Dua kweli ,miezi 4 sasa umejikausha ......

Ndugu Ile laki uliyosema unanirudishia soon Miaka mi 5 hii sasa ....

nk.

Namshukuru Mungu kwa wote mlionidhulumisha huwa sioni kilichopungua kwenye kile ninachopata hata kama ni kidogo. Ila mkae mkijua kama huko mbeleni kuna kulipana na bila shaka ipo , haki yangu mtailipa tu maana haki ya mtu haidhulumiwi.
Duhh coment yako imenipa moyo pesa tunatafuta kwa shida na haki ila mtu anaila hivihivi

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom