mwanga mweusi
JF-Expert Member
- Dec 21, 2020
- 267
- 441
Hata sielewi kwanini inanitokea hivi. Nilifanya kazi kwa jamaa mmoja akanidhulumu Tsh. 470,000/-. Nikafanya kazi kwa mwingine akanidhulumu Tsh. 70,000/-, mwingine Tsh. 35,000/-, nikauziwa tofali mbovu za Tsh. 200,000/-.
Nikakodi shamba la kulima nimefika kulima nakuta kuna mtu kaanza kulipa pale kwangu anasema nipewe sehemu nyingine!
Mimi sijawahi kula cha mtu, napambana nipate haki yangu ila nadhulumiwa tu hadi nimekata tamaa kabisa!
Sijui hata uelekeo wa kwenda polisi, maana sijawahi kanyaga toka nizaliwe. Nataka niende kwa mganga japo napo sijawahi kanyaga. Sasa naona ugumu kuanza haya mambo ya polisi na wapi huko wakati hata sijui nikifika nasemaje!
Naomba mwenye njia ya kunisaidia anisaidie.