Dialogist
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 1,121
- 1,815
Heshima kwenu Wakuu,
Nimetafakari kama raia wa kawaida tu, na raia namba 53,398,487 wa Jamhuri yetu.
Kuna hii saga au mvutano unaoendelea ndani ya Chadema katika madhira ya kugombea uongozi baina ya timu ya Mwenyekiti wa sasa Ndugu FREEMAN AIKAEL MBOWE (STU) na Makamu wake Ndugu TUNDU ANTIPAS LISSU (LLB). Na mvutano huu unachagizwa zaidi na wapambe wa kila mmoja hasa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia na mahojiano yao wahusika wakuu kupitia media mbalimbali.
Katika muktadha huo, na kwa kuzingatia hali ya kisiasa iliyokua nayo Chadema baada ya uchaguzi wa Serikali za mitaa, na kwa kuzingatia kutokuwepo kwa wale wabunge COVID 19 ambao walikua na nguvu na ushawishi chamani, sasa kwa hayo na mengine machache in any how hiki chama kilikua kinaenda kujifia taratibu mwakani.
MBOWE na LISSU ni very tricky people. Kwa uchunguzi wangu usio rasmi sana kupitia vyanzo vyangu binafsi, ni kwamba hawa jamaa wamekaa kikao wao na wengine wachache sana na kutengeneza "MASSIVE PUBLIC ATTENTION" ili kurudisha chama kwenye ramani.
Ambapo katika hilo wamekana hadi nafsi zao mradi tu kutengeneza uhai wa chama. Hawa wote mnaowaona sijui Boni Mayai, Matobi na Nyerere ni vipindi tu vimetengenezwa. Trust me huu uchaguzi umesukwa hasa. Na baada ya uchaguzi haijalishi atashinda nani kwenye sanduku la kura lakini atatangazwa MBOWE, na LISSU atakubali katika mfumo wa maridhiano ili kukinusuru chama.
Lissu atagombea Urais wa JMT na watawasamehe COVID 19 wote katika muktadha huo huo wa maridhiano ili kwenda kupambana majimboni. Move ya hawa jamaa ni kupata wabunge angalau 45% na madiwani 52%... wakijua urais hawatapata.
Kwa hayo na mengine mengi, muda utaongea. Na ningependa hii post iwe STICKY in Moods discretion..
Tukutane FEBRUARY 15.
..Ni hayo tu!!!