Nina mashaka na ujauzito wa mpenzi wangu

Mimba huhesabiwa toka mzunguko wa mwisho wa mwanamke. Yaani ile tarehe yake ya mwisho ya period, alipomaliza period, kesho yake ndo tarehe ya kwanza ya mimba.

Piga hesabu zako vizuri mkuu usije bambikiziwa kiumbe ambacho sio chako kisa tu amekuona wewe mnyonge.
 
Ikiwa mlifanya tendo la ndoa na mpenzi wako wiki tatu zilizopita na kipimo cha ultrasound kinaonyesha kuwa ana ujauzito wa wiki 5 na siku 2, inawezekana kwamba mtoto ni wako. Kipimo cha ultrasound kawaida hupima muda wa ujauzito kuanzia siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho ya mwanamke (LMP), ambayo ni takriban wiki mbili kabla ya yai kuachiliwa (ovulation) na mimba kutungwa. Hii inamaanisha kuwa ujauzito wa wiki 5 na siku 2 ungehusishwa na kutungwa kwa mimba takriban wiki 3 zilizopita.
Kwa maana hio huenda hedhi yake ya mwisho ilikua wiki 5 zilizopita, na tumekutana wiki 3 zilizopita.. kwahio ultrasound imeanzia kuhesab kunzia hedhi yake ya mwsho! Km ni hvo bas ntafatilia nijue hedhi yake ya mwsho ilikua lini ili ni confirm..
 
Habari, nipo kwenye mahusiano na binti fulani hivi kwa muda wa mwaka, sasa mara ya mwisho kukutana nae kimapenzi ni wiki tatu zilizopita na kabla ya hapo sijakutana nae kimapenz zaid ya miez mi3.. sasa juzi kaniambia anahisi ana mimba maana hajazion siku zake..
Nikamtumia pesa aende hosptal kupima.. baada ya kupima akanitumia ultrasound inasoma mimba ipo na ina week 5 na sku 2.
Nimepiga hesabu zangu naona zinagoma nilitegemea angalau iwe na wiki 3 au zisizid 4.
Ila yeye sijamueleza hiki nachohisi kama mimba sio yang.

SWali langu je hizi ultrasound zinaonesha uhalisia au ni makadirio?

Na kama ni makadirio, je mimba ya wiki 3 inaweza kweny ultrasound ikasoma 5weeks?
Hatari sana.
 
Mimba huhesabiwa toka mzunguko wa mwisho wa mwanamke. Yaani ile tarehe yake ya mwisho ya period, alipomaliza period, kesho yake ndo tarehe ya kwanza ya mimba.

Piga hesabu zako vizuri mkuu usije bambikiziwa kiumbe ambacho sio chako kisa tu amekuona wewe mnyonge.
Thnks, nitafuatilia hili nijue kiundan period yake ya mwsho
 
Ikiwa mlifanya tendo la ndoa na mpenzi wako wiki tatu zilizopita na kipimo cha ultrasound kinaonyesha kuwa ana ujauzito wa wiki 5 na siku 2, inawezekana kwamba mtoto ni wako. Kipimo cha ultrasound kawaida hupima muda wa ujauzito kuanzia siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho ya mwanamke (LMP), ambayo ni takriban wiki mbili kabla ya yai kuachiliwa (ovulation) na mimba kutungwa. Hii inamaanisha kuwa ujauzito wa wiki 5 na siku 2 ungehusishwa na kutungwa kwa mimba takriban wiki 3 zilizopita.
Bora umemwelewesha mi naona uvivu kuandika,watu wengi hawajui kuhesabu umri wa mimba wao wanadhani siku ya kudo ndo umri wa mimba
 
Ukute hana mimbaa, ni mpango kautega akupigee maokotoo.

Nimekumbukaa shost angu alivyompiga jamaa ake mapenee, kupitia mimba uchwara, mwsho kudanganya imeharibikaa. Lol

Shtukaa mjinii hapaaa.
 
Back
Top Bottom