Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,067
Mkuu ni wapi unapoweza kupata kontela la futi 40 kwa 1.5M?? Kwa bei hiyo hata la futi 20 hupati.Nunua kontena za kusafirishia mizigo 2 za futi 40.
Kontena moja unapata hata kwa 1.5 m kwa sasa so jumla itakuwa ni 3M.
Kontena kama kontena tayari ni nyumba inayojitegemea ila huwa na matatizo matatu tu ambayo huyafanya kontena lisiwe zuri kwa matumizi ya nyumba.
Matatizo hayo ni:
1.joto- hali ya hewa ya joto huathiri kontena sana mana lile huwa ni kama box ambalo limefungwa pande zote.
So kontena likitobolewa na kuweka milango,madirisha na ceiling basi huweza kuzuia joto la nje na kufanya kuwa sehemu nzuri ya kuishi.
2.upepo- ikitokea kuna upepo nje basi kontena huwa linalia kama ngoma so huwa sio sehemu nzuri ya kuishi.
Unaweza kuzuia upepo huo kwa mbao nyepesi kuzunguka kontena na hivyo likawa zuri tu kwa kuishi.
3.baridi- baridi huweza kuzuiwa na mbao pia.
Ukishafanya mambo hayo 3 basi kontena linabadilika na kuwa sehemu nzuri ya kuishi ambao inaamishika pia.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuniinbox.