Nimwombe Rais Samia awaondoe haraka wanajeshi wetu kule DRC Congo. Mnapigana na nchi ya EAC

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,902
2,155
Hii inaenda kuwa kashfa kama ile ya Biafra tulisapoti wrong side katika History badala kujikita kwenye kupatanisha.

Col. Ojukwu hivi aliwahi hata kuja Nchini kutembelea makaburi ya Askari wetu kweli?

Au alikuwa anakaa kwenye Mahoteli ya hali ya juu na kubadilisha Wasichana Warembo huko Abidjan?
 
sijajua wanajeshi wetu wanafia nini kule DR congo wakati sasa imejulikana bila shaka kwamba wanapigana na wanajeshi wa Rwanda ambayo ni nchi mwanachama wa EAC.

SOLUHISHO ya vita ile ni kuiwekea vikwazo RWANDA na kuifukuza EAC haraka iwezekanavyo.

Mama yetu mpendwa nakuomba uwaondoe haraka watoto wa taifa letu wanaopigana na M23 kule DRC.damu yao inamwagika kwa sababu gani?


View: https://www.youtube.com/watch?v=HHtxvhSPgAQ&t=124s&pp=ygUWdGhlIHBlb3BsZSAgd2hvIGFzayBtZQ%3D%3D

Kuna magari zaidi ya 300 kutoka Rwanda yanabeba Mchanga uliokuja na meli kupitia bandari ya Kigoma kutoka Congo yanapita Kigoma -Kasulu - Kibondo- Kakonko -Nyakanazi. Itakuwa Nchi wanachama tunafiadika siyo bure.
 
Hiyo vita sio ya kuisha leo wala kesho provided M23 wana support ya nchi jirani. Adui (makundi yote ya waasi) wakizidiwa wanauwezo wa kupotea haraka kama walivyo na uwezo ku-mobilise jeshi haraka hali ikitulia na kulianzisha tena.

Tanzania na wasaidizi wengine waipe Congo ultimatum msaada wa kijeshi uende sambamba na serikali ya Congo kuwekeza heavily kwenye jeshi lao kulinda mipaka yao na kuli-control hilo eneo. Awawezi kuli-control hilo eneo ifike wakati tuache fate ichukue mkondo wake kama ni annexation ya eneo let it be aitokuwa nchi ya kwanza kumegwa kwa sababu ya serikali kushindwa ku-control eneo.

Bila ya Congo kutoa road map ya adhma yao ya kuli-control hilo eneo miaka 20 baadae bado tutakuwa tunapeleka askari wakati wenyewe huko Kinshasa wako busy kuboresha mikorogo na kukata mauno.

Ifike hatua lazima Tanzania ione seriousness ya Congo kutaka kulinda himaya zake yenyewe kabla ya kuji-commit kuwasaidia miaka zaidi ya 20 ya kuwasaidia inatosha kama wenyewe hawana mpango wa kuweka strong military presence huko. Kwani sisi nani alitusaidia Amini alipoitaka Kagera si wenyewe tulilinda eneo letu.

Let them annex it kama wa-Congo wameshindwa kulilinda eneo lao inatosha, watasaidiwa mpaka lini.

Iła M23 lazima nae atiwe adabu kipindi hiki kwa kuuwa askari wa Tanzania, lazima ajue sumu aionjwi.
 
Bahima Empire,Plundering and piracy ya resources ndio msingi mkubwa wa mauaji ya raia wasio na hatia..

Hatuwezi kuwa salama kama nchi ikiwa tutabariki uharamia wa rasilimali kwa wenzetu (DRC) wenye impact kubwa kwenye uchumi wetu..Logistics infrustructure and trade.

Tukizembea na kujizima data ipo siku M24 wataingia Ngara,Geita,Kahama,Biharamulo..
 
Back
Top Bottom