Nimetumika kwenye Tangazo la TV bika Malipo wala mkataba

sasa mwanzo wakati unaigiza hukujua kama tangazo litatoka au ujinga tu kichwani ?
Niliahidiwa pesa ila ndio hivyo hatukusaini mkataba na kampuni iliyopewa kuandaa tangazo
 
Hili nalo jipu...ilikuwaje hadi ukaonekana kwenye hilo tangazo inamaan ulikuwa hujitambui wakati mnapanga kufanya hilo tangazo au ndo elimu yako ndogo kama ulivosema....
Elimu mdogo au kubwa sio tatizo ,

Na ofcoz kwenye swala la elimu nadhani nina elimu ya kutosha tu ,.. ila wakati nafanya tangazo tulikuwa na makubaliano ya mdomo. Hilo ndio tatizo
 
HILO TANGAZO LINAHUSIANA NA NINI? TUANZIE HAPO .. au utuambie linarushwa saa ngapi? nikufuatilie kama litatoa hela ndefu nifanye udalali kuna mwanasheria nikukabidhi atanipatia mimi 10%
Naomba nikutafute tu kama utanipa msaada , nisingependa ku publish hapa. Itaathiri kesi nzima.
 
Na wewe lipia Jamiiforums kwa hili tangazo... kwa sababu kila mtu atataka kujua ni nini hicho...
 
Habari zenu wanajamvi ,

Nakuja kwenu kwa heshima nikiomba msaada wenu wa kisheria baada ya kutumika kwenye tangazo la kibiashara kwenye televisheni bila ya kupewa pesa yoyote na pia bila mkataba au makubaliano yoyote ,

Kwenye tangazo hilo mm ndio mhusika mkuu , kwa maana ya kwamba mm ndio naonekana sana na mimi ndie niliyebeba ujumbe mzima.

Tangazo hilo mpaka sasa linarushwa kwenye televisheni mbali mbali na pia hata kwenye mitandao ya kijamii kama you tube ,twiter na facebook.

Ombi langu ni kwamba ningependa kujua kama naweza kufungua kesi mahakamani na nikapata haki zangu za msingi..

Tafadhali naomba wadau wenye ujuzi na uzoefu kwenye maswala ya kisheria na maswala ya masoko na matangazo wanisaidie au waniambie tu japo kuwa naweza kufanya fanya vipi nikafanikiwa.

Natanguliza shukran za dhati..
napenda kukutaarifu kuwa mahakamani utashindwa tu sababu hakuna maandishi yoyote,, mliyokubaliana
 
  • Thanks
Reactions: nao
...hahahahahaha..swali la kizushi,ulisaini karatasi yoyote?..una mkataba wowote na agency yoyote au agency model?
Sina chochote kati ya hivyo.. ila mimi si naonekana kwenye tangazo? Hiyo je haitoshi?
 
cha kufanya negotiate nao kwanza wakupe promise ya malipo kwa maandishi au mkataba u sign ili iwe mwanzo wa kila kitu
 
Back
Top Bottom