Nimetumika kwenye Tangazo la TV bika Malipo wala mkataba

srinavas

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,149
3,862
Habari zenu wanajamvi ,

Nakuja kwenu kwa heshima nikiomba msaada wenu wa kisheria baada ya kutumika kwenye tangazo la kibiashara kwenye televisheni bila ya kupewa pesa yoyote na pia bila mkataba au makubaliano yoyote ,

Kwenye tangazo hilo mm ndio mhusika mkuu , kwa maana ya kwamba mm ndio naonekana sana na mimi ndie niliyebeba ujumbe mzima.

Tangazo hilo mpaka sasa linarushwa kwenye televisheni mbali mbali na pia hata kwenye mitandao ya kijamii kama you tube ,twiter na facebook.

Ombi langu ni kwamba ningependa kujua kama naweza kufungua kesi mahakamani na nikapata haki zangu za msingi..

Tafadhali naomba wadau wenye ujuzi na uzoefu kwenye maswala ya kisheria na maswala ya masoko na matangazo wanisaidie au waniambie tu japo kuwa naweza kufanya fanya vipi nikafanikiwa.

Natanguliza shukran za dhati..
 
Liweke hapa hilo tangazo tuone
 
Hauwez kupata msaada wa kisheria hata uende mbinguni kwa sababu ulicheza tangazo bila mkataba! Angalau ungekuwa umejaza mkataba na malipo yako unayajua ingekuwa rahisi kuyadai sasa hapa unadai nini? Unadai hewa! Hakuna malipo bila maandishi! Tumia hiyo nafasi kujitangaza ili upate matangazo mengine na sio kuwasumbua ili ujibanie hata kama kuna wengine qamekuona
 
Hili nalo jipu...ilikuwaje hadi ukaonekana kwenye hilo tangazo inamaan ulikuwa hujitambui wakati mnapanga kufanya hilo tangazo au ndo elimu yako ndogo kama ulivosema....
 
Aisee...!
Wewe hukuwa unahitaji hela mkuu?
Ulikubalije kucheza bila kupatana bei?
Kwanini hata hamkuandikishana serikali za mtaa?
Basi tena endelea kujitazama kwenye kideo ufurahi na roho yako!
 
Waandikie barua ya madai ya kiasi cha hela unachoona ni haki yako huku ukilitaja hilo tangazo lako.
Hiyo barua mpe mwanasheria wako nakala ambaye atakusaidia kufuatilia huko mbele.

Tanzania imezoea kuwanyonya vijana wetu, wanazika haki za watu. Uzuri wa awamu hii ya tano ukienda ofisi yoyote unapokelewa na unasikilizwa. Dai haki yako utapata hata kwa kuchelewa.
 
ni PM ni tangazo gani nitakushauri since hutaki kulitaja hadharani!
 
Ulifanya makosa kutangaza bla mkataba nenda katangaze pia instagram page kama ya mrekebshatabia muombe akutangazie utaje na jina la kampun utasaidka haraka
 
Kwenye makubaliano yoyote ya kibiashara lazima kuwa na consideration. Mmoja anatoa, mwingine anapata. Kama mwenye tangazo sio ndugu yako(mke,dada, kaka), hata kama kulikuwa na makubaliano ya mdomo au hata kama hamkukubaliana, kisheria unastahili malipo fulani. Sema yanaweza kuwa kidogo maana kazi imeshafanyika hivyo huna nguvu ya kunegotiate. Contracts 101.
 
Kuna maswal hujajibu hum wakat una shoot tangazo hukujua? Kama ulijua ulishoot vp bila makubaliano?
 
Mkuu ukipata mwanasheria/wakili mjanja mbona hela yako unapata tu!as long as wewe umeshatoa huduma kweny hilo tangazo na wameikubali huduma yako na wanaitumia na pia kufaidika nayo, basi kisheria unayo haki,hapo tunaweza kutumia mlango wa kisheria wa either kulikuwa na oral contract,contract by conduct au quasi-contract(common law). Na pia ikumbukwe kwamba kwenye law of contract kuna common law principle inasema "no one should be benefited from the cost of another" kimsingi hao jamaa wananufaika bure na jasho lako of which unaweza kwenda kulilalamikia kwa mujibu wa sheria.
Na pia ikumbukwe pia si kila mkataba ni lazima uandikwe,kuna njia nyingi tu za kuingia mikataba mbali na kuandika isipokuwa kwa ile mikataba ambayo sheria inataka lazima iandikwe kama vile,mikataba ya kuuziana ardhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…