Nimetembea kimapenzi na dada yangu wa damu, ninaomba ushauri

Njia pekee ni kutubu na kusema ukweli. Inaidi umuite mama na wazee wa heshima na sista upasue ukweli. Mficha maradhi kifo humuumbua
 
Laana zote zipo hapa mkuu. Soma kisha mlilie Mungu wako atakusamehe maana yeye ni mwingi wa rehema. Usirudie tena...

Kumbukumbu la Torati 27:1-26

1 Na Musa pamoja na wanaume wazee wa Israeli wakawaamuru watu, na kusema: “Kila amri ninayowaamuru ninyi leo, itashikwa.
2 Na itatukia kwamba katika siku ambayo mtavuka Yordani kuingia katika nchi ambayo Yehova Mungu wako anakupa wewe, utajiwekea pia mawe makubwa na kuyapaka chokaa.
3 Nawe utaandika juu yake maneno yote ya sheria hii utakapokuwa umevuka, ili uingie katika nchi ambayo Yehova Mungu wako anakupa wewe, nchi inayotiririka maziwa na asali, kulingana na yale ambayo Yehova Mungu wa mababu zako amesema nawe.
4 Na itatukia kwamba mtakapokuwa mmevuka Yordani, mtayasimamisha mawe hayo, kama ninavyowaamuru ninyi leo, katika Mlima Ebali,+ nawe utayapaka chokaa.
5 Pia utamjengea Yehova Mungu wako madhabahu huko, madhabahu ya mawe. Usitumie chombo cha chuma juu yake.
6 Kwa mawe mazima utaijenga madhabahu ya Yehova Mungu wako, nawe utamtolea Yehova Mungu wako matoleo ya kuteketezwa juu yake.
7 Nawe utatoa dhabihu za ushirika na kuzila huko, nawe utashangilia mbele za Yehova Mungu wako.
8 Nawe utaandika juu ya mawe hayo maneno yote ya sheria hii, na kuyafanya yawe wazi kabisa.”
9 Ndipo Musa na makuhani Walawi wakasema na Israeli wote, na kuwaambia: “Kaa kimya, usikilize, Ee Israeli. Leo umekuwa kikundi cha watu wa Yehova Mungu wako.
10 Nawe uisikilize sauti ya Yehova Mungu wako na kutimiza amri zake na masharti+ yake, ninayokuamuru leo.”
11 Naye Musa akaendelea kuwaamuru watu katika siku hiyo, na kusema:
12 “Wanaofuata ndio watakaosimama ili kuwabariki watu kwenye Mlima Gerizimu wakati ambapo mtakuwa mmevuka Yordani: Simeoni na Lawi na Yuda na Isakari na Yosefu na Benyamini.
13 Na wanaofuata ndio watakaosimama kwa ajili ya laana kwenye Mlima Ebali: Rubeni, Gadi na Asheri na Zabuloni, Dani na Naftali.
14 Nao Walawi watamjibu kila mtu wa Israeli na kusema kwa sauti iliyopaazwa:
15 “‘Amelaaniwa mtu ambaye anafanya sanamu ya kuchongwa au sanamu ya kuyeyushwa, kitu kinachochukiza kwa Yehova, kilichotengenezwa kwa mikono ya mfanyakazi wa mbao na chuma, na ambaye amekiweka mafichoni.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
16 “‘Amelaaniwa yule ambaye humtendea baba yake au mama yake kwa dharau.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
17 “‘Amelaaniwa yule ambaye huisogeza nyuma alama ya mpaka wa mwenzake.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
18 “‘Amelaaniwa yule ambaye humpotosha kipofu njiani.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
19 “‘Amelaaniwa yule ambaye hupotosha hukumu ya mkaaji mgeni, mvulana asiye na baba na mjane.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
20 “‘Amelaaniwa yule ambaye hulala na mke wa baba yake, kwa sababu ameufunua upindo wa nguo ya baba yake.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
21 “‘Amelaaniwa yule ambaye hulala na mnyama yeyote.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
22 “‘Amelaaniwa yule ambaye hulala na dada yake, binti ya baba yake au binti ya mama yake.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
23 “‘Amelaaniwa yule ambaye hulala na mama-mkwe wake.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
24 “‘Amelaaniwa yule ambaye kutoka mafichoni humpiga na kumuua mwenzake.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
25 “‘Amelaaniwa yule ambaye hukubali rushwa ili kuipiga na kuiua nafsi, wakati ambapo hiyo ni damu isiyo na hatia.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
26 “‘Amelaaniwa yule ambaye hatayatimiza maneno ya sheria hii kwa kuyafanya.’ (Nao watu wote watajibu na kusema, ‘Amina!’)
Kaini na abili watoto wa adam na hawa walioa wakina nani? Incest sex iliruhusiwa kipind hicho?
 
14 Kisha Walawi na wajibu, wawaambie watu wote wa Israeli kwa sauti kuu,
Kumbukumbu la Torati 27 :14

15 Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :15

16 Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :16

17 Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :17

18 Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :18

19 Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :19

20 Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :20

21 Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :21

22 Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :22

23 Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :23

24 Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :24

25 Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :25

26 Na alaaniwe asiyeyaweka imara maneno ya torati hii kwa kuyafanya. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27 :26
 
Wewe acha ujinga, muoe dada yako, si ushamzalisha watoto wawili au? Sasa unataka uende wapi?
 
Haya sasa ni mambo ya kina Dola Iddy

ila hii story nakumbuka kama nilishaisoma sehemu au humu humu kitambo sana.

Inafanana na Blue Logoon Movie
 
Hii hadithi yako ingelikuwa ni kweli ingelikuwa ni mkasa haswa...

Ila ndio hivyo tena changamsha genge...
 
Hilo linatoka kwenye biblia, ila kwa hicho unachotaka kujua Biblia ipo kimya labda uende kwa hisia.
kaini akamjua mkewe akamzaa henoko
Hisia zangu ni kwamba wakati mungu anawaumba adam na hawa kulikuwa na watu wengine jamii tofauti
Au lah huyo mke aliyezaa naye hakuwa specie moja na binadamu wa kawaida, sijui inakaaje hii kwenye genetics when two different species intersex

Hisia zako ni zipi?
 
kama mkristo tafuta ibada wewe na dada yak msaidiane aisee kumaliza hilo tatizo
 
kaini akamjua mkewe akamzaa henoko
Hisia zangu ni kwamba wakati mungu anawaumba adam na hawa kulikuwa na watu wengine jamii tofauti
Au lah huyo mke aliyezaa naye hakuwa specie moja na binadamu wa kawaida, sijui inakaaje hii kwenye genetics when two different species intersex

Hisia zako ni zipi?
Kwenye hilo la akina Kaini na Habil kuwajua wake zao na kuzaa, ya kwamba wake wametoka wapi sina hisia zozote na nimeliacha libaki kimya biblia ilivyoliacha kimya. Provided halina msaada kwenye wokovu wangu na kama lingekuwa na msaada lingeandikwa.
 
sikumbuki ni mara ya ngapi nakutana na story inayofanana na hii.nahisi mleta mada kaikopi sehemu,ila siyo habari mpya/ngeni kwangu.

all in all mahusiano ya kimapenzi kati ya ndugu wa damu moja ni laana katika ukoo.
Hizi stori wanatunga ili kupata wasomaji
 
Back
Top Bottom