Nimetapeliwa na baba mzazi, naombeni ushauri jamani

Mzee wako mademu wanamponza ila anajua uwajibakaji wako, ongea nae kiutu uzima! akukopeshe hela kidoggo (usiombe mtaji omba mkopo) au mwambie wataka fungua biashara na yeye awe busness patner! Ongea nae kiutu uzima
Nimejaribu hii njia katosa kuhusu mademu sijui ila nachojua hakuwahitaka nikioa nikae nje nyumbani
 
Kwa uwezo ulio elezea wa kufanya biashara ulionao ni hazina tosha kaka.Usikate tamaa mapema kaka cha msingi jitahidi sana hata kuwatafuta miongoni mwa walokuwa wateja zako uwaelezee a real situation na kunapo uwezekano wa kumpata hata mmoja wa kukushika mkono amini unaweza utatusua tu brother.Remember what u see iz what u have bro.Struggle.
 
Wazazi wetu wakati mwingine sijui wanaingiwa na mapepo? Pole u r not alone in this. Saa ingine unawaza hadi unakufuru ila ndio alishakuwa mzazi wako. Jifute vumbi songa mbele kwa imani wala usiende kwake kuomba ushauri maana alipokifanyia hili alikuwa na akili timamu kabisa. Tafuta njia zako zingine utoke kivyako. Usirudie tena kufanya kitu na mzazi au ndugu labda umuachie asilimia zote lakini isiwe shirika.
 
Mkuu pambana uanze upya achana na makesi wala kumwazia mabaya pambana anza upya utafanikiwa wala usimchukie mpe heshima Yake kama kawaida ila kuhusu ela asikuzoee ata akija kujikomba au alitaka ushauri Wa biashara achana naye ilimradi usimvunjie heshima tu huyo Dogo wako Wa udom pambana amalizie huyo Wa india mshauri asimamishe ata mwaka mmoja mpaka uwe sawa
 
Mzee wako mademu wanamponza ila anajua uwajibakaji wako, ongea nae kiutu uzima! akukopeshe hela kidoggo (usiombe mtaji omba mkopo) au mwambie wataka fungua biashara na yeye awe busness patner! Ongea nae kiutu uzima

Mzee kamaliza hela itakuwa, I can't believe mpaka Leo kuna wazee hopeless namna hii!!!!! Mi naamini utainuka somehow. Usikate tamaa, ukikaa na wadogo zako na kusononekea majukumu hutawasaidi wala hutajisaidia, wake up and look up for business and capital, ukianza kurun regardless matatizo fedha ikiwepo hakuna kuchelewa
 
Nadhani kosa namba moja lilikuwa ni kukubali kuendesha biashara zako na mzee wako bila kuunda kampuni. Cha kwanza wewe kama msomi ulitakiwa umshauri baba yako muunde kampuni, wewe uwe CEO na yeye mwenyekiti wa Board ya wakurugenzi, ungehusisha watu wenu wa karibu kuunda board of directors. Kila tatizo ulilolipata lingekuwa na majibu hata baba yako angeogopa kabisa kumiss use hizo resources. Kinachoonekana baba yako ni mwingi wa habari, inaonekana alikuwaga na biashara nzuri sana alipokuwa na nguvu, na pia mtakuwa mlikuwa mnanyanyaswa kwa namna moja au nyingine, pia baba yako possibly alikuwa maarufu kiasi wanawake wengi walimpenda na yeye akaingia mtego wao, hivyo ulivyo rudi wewe na kuzifanya biashara kusimama baba yako alirudisha heshima mtaani. Ila baada ya kuona wewe unataka kujitegemea kaona biashara zake zitakufa akaamua bora akunyime. Cha kufanya, kaa na mzee wako, mwambie mtumie resource zilizopo chukueni mkopo bank, undeni kampuni, ingiza board member unaowajua, then utasimama. Achana na mambo ya kwenda kujitegemea wewe huyu huyo mzee mwambie tu baba tuliteleza tuanze upya ila muundo ndiyo huu, na hakika atakubali na mambo yako yatanyooka zaidi ya hapo!
 
Kwa uwezo ulio elezea wa kufanya biashara ulionao ni hazina tosha kaka.Usikate tamaa mapema kaka cha msingi jitahidi sana hata kuwatafuta miongoni mwa walokuwa wateja zako uwaelezee a real situation na kunapo uwezekano wa kumpata hata mmoja wa kukushika mkono amini unaweza utatusua tu brother.Remember what u see iz what u have bro.Struggle.
Nitajitahidi ingawa nimeshajaribu wengi wa waliokuwa wasupplier wangu wa mahind wamenielekeza nitafute eneo nisimike mashine ya kusaga na kukoboa then wenyewe watanikopa mahindi. Kuna mmoja aliahid kama nikiweza atanipa mpaka tani 200 za mahindi nimlipe baada ya miez mitatu. Ishu imekuja kuwa ngumu kupata mashine na kusindika. Pia mke kakomaa hataki nirudi nikae karibia na mzee wangu. Kuna mmoja aliahidi kunikopa 300000mts ila bahati mbaya yuko hospitali kalazwa anusumbuliwa na kisukari.
Naamini mungu yupo. Atleast nimepata ahueni kidogo baada ya kupata nasaha kidogo. Nilikuwa najifungia ndani tu nahuzunika naona aibu hata kuwaface marafiki zangu ila nimepata nguvu tena
 
He invested in you, you have paid him back, huo uwezo wa kufanya biashara ndiyo mtaji wako, komaa nao huo usihangaike na token songa mbele
And he probably had hard times...So don't let him down. Its time to show your wisdom...make him proud of you!! Wakati mwingine mtoto ukiegemea sana upande wa mzazi mmoja ni hatari mno. Pengine mzee ameona uko pamoja sana na mama yako hivyo akajihisi kuna jambo laweza kumkuta, anyway this is just my feelings and experiences.
 
Mzee kamaliza hela itakuwa, I can't believe mpaka Leo kuna wazee hopeless namna hii!!!!! Mi naamini utainuka somehow. Usikate tamaa, ukikaa na wadogo zako na kusononekea majukumu hutawasaidi wala hutajisaidia, wake up and look up for business and capital, ukianza kurun regardless matatizo fedha ikiwepo hakuna kuchelewa
Nashukuru Sana kaka. Ukiwa na wadogo watoto wa kike lazima uumize kichwa kama huyu wa udom nilikuwa naogopa kumpa situation iliyopo maana hachelewi
 
Unaweza kuanzisha na wewe kampuni yako kwa kukopa hela benki au mtu wa karibu akakukopesha mtaji,na kwa vile una wateja wanaokujua watumie hao hao.
 
GOOD.
Unajua huku uswahilini kuna msemo kwamba ukiona dhiki imezidi sana ujue neema inakaribia
So jipe moyo kwani hayo ni majaribu tu coz kila mtu huwa anapewa mitihani wa kulingana na uwezo wake so yakupasa uwe na misuli ya imani kaka.Wewe hilo kwako waweza ona zito/kubwa lkn akaja mwingine humu akaleta yanayomsibu hakika hata kama ulikuwa unalia utafuta machozi na kumtukuza MUNGU.Mimi kama mkiristo naamini MUNGU humpa mtu jaribu lkn pia humwandalia njia ya kutokea so dont be afraid fellow young man.Kila jaribu lina mlango wa kutokea kaka amini na Bibilia ina kataza na kusema MUNGU hampendi mtu anaenung'unika.
Songa mbele kuwa jasiri usiyumbe.
 
Acha kubwela wewe, kwa maelezo yako wewe unaonekana ni mfanyabiashara mzuri zaidi! Fanya mpango wakufanya hiyo business kivyako achana na mzee wako
Kuajiriwa kutakupotezea muda
MKUU UMENENA VEMA, BABA YAKE MTUMIAJI HUYO AACHANE NAYE.
 
Nadhani kosa namba moja lilikuwa ni kukubali kuendesha biashara zako na mzee wako bila kuunda kampuni. Cha kwanza wewe kama msomi ulitakiwa umshauri baba yako muunde kampuni, wewe uwe CEO na yeye mwenyekiti wa Board ya wakurugenzi, ungehusisha watu wenu wa karibu kuunda board of directors. Kila tatizo ulilolipata lingekuwa na majibu hata baba yako angeogopa kabisa kumiss use hizo resources. Kinachoonekana baba yako ni mwingi wa habari, inaonekana alikuwaga na biashara nzuri sana alipokuwa na nguvu, na pia mtakuwa mlikuwa mnanyanyaswa kwa namna moja au nyingine, pia baba yako possibly alikuwa maarufu kiasi wanawake wengi walimpenda na yeye akaingia mtego wao, hivyo ulivyo rudi wewe na kuzifanya biashara kusimama baba yako alirudisha heshima mtaani. Ila baada ya kuona wewe unataka kujitegemea kaona biashara zake zitakufa akaamua bora akunyime. Cha kufanya, kaa na mzee wako, mwambie mtumie resource zilizopo chukueni mkopo bank, undeni kampuni, ingiza board member unaowajua, then utasimama. Achana na mambo ya kwenda kujitegemea wewe huyu huyo mzee mwambie tu baba tuliteleza tuanze upya ila muundo ndiyo huu, na hakika atakubali na mambo yako yatanyooka zaidi ya hapo!
Nashukuru ni kama ulikuwepo. Hili ni kosa ambalo nililifanya kwa kutosajili ila idea yetu ilikuwa tufanye kazi ili tupate mtaji wa kufungua kiwanda cha Kati Tanzania badala ya msumbiji hata kabla ya harusi nilikuwa nishaanza negotiate na kampuni ya kichina ituuzie complete set ya flour mill without silos. Kilichonifanya nimuamini ni kwa sababu kwanza n mzazi wangu.
Pili alikuwa ananiamini Sana kuliko mtu yoyote. Idea ya kununua set nzima ilikuwa ili kumrahishia yeye ufanyaji kazi pia ukaguz hasa baada ya mimi kuondoka. Sikuwahi fikiria kama angenigeuka.
Kuhusu kurudi kusema kweli nimekuwa mvumilivu wa mambo mengi Sana ntaposema nianze nae tena ndo atazidi haribu. Hapa napoandika Kuna watu hawajalipwa pesa yao toka nilipoondoka. Nachohisi anafanya ni kutumia pesa akijua labda ntarud nianze kulipa tena. Kimechonishtua kukimbia kulipa Ada za watoto wake
 
Linawezekana pia hawa wazazi ni binadamu kama binadamu wengine. Ndio maana mahakama zimewekwa
Ushauri wako ni mzuri lakini sikubaliani nao hekima na busara zitawale mi nadhani yaliyopita si ndwele masuala ya sijui alikuwa na biashara ikaenda ikarudi aache nayo aanze hapo hapo fursa yoyote itakayojitokeza aitumie hawa wazazi ni kuwasamehe bure!Ubinafsi umewazidi japokuwa sio wote!
 
Mahindi unatoa wapi?
Kazi ilifanyikia Mozambique. Mimi sikuwa naenda shamba kurafuta mahindi ila Kuna watu ndo ilikuwa biashara yao pia nisingependa nitaje eneo maaba ni kampuni moja iliyopo hapo na Kuna raia wengi wanapita hapa for the sake of privancy naomba nisitaje hapa ili in private ntakuambia
 
Ushauri wako ni mzuri lakini sikubaliani nao hekima na busara zitawale mi nadhani yaliyopita si ndwele masuala ya sijui alikuwa na biashara ikaenda ikarudi aache nayo aanze hapo hapo fursa yoyote itakayojitokeza aitumie hawa wazazi ni kuwasamehe bure!Ubinafsi umewazidi japokuwa sio wote!
Thanks broo
 
Back
Top Bottom