Nimetambua lengo kuu la kuwepo duniani ni kutafuta uhuru/haki

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Aug 1, 2014
2,765
3,335
Abadni sitapingana na vitabu vitakatifu ambavyo vinaamini uwepo wetu katika dunia ni wenye lengo la kumuabudu mungu,quran inasema sikuwaumba majini na binadamu isipokuwa waniabudu.

Binafsi nimetambua dhamira ya uwepo wetu katika hii dunia ni kutafuta namna ya kupambana na mazingira ili kupata uhuru na haki,ndiyo maana kila eneo katika hii dunia inazungumzia haki pamoja na uhuru.

Lakini, hii haki na uhuru tunayoitafuta ni asili ni kwamba unakuwa na mipaka ndani yake siyo haki nyengine ambazo haziendani na nature,kuna nadharia za akina thomas hobbes na john locke ambazo zinaelezea asili ya binadamu kabla ya kuwepo state, watu walikuwa wanachinjana ili kupata haki,wanapigana ili kupata uhuru(uhuru wa kimazingira,kufikiri na hata kazi).

Ndiyo maana utaona tuna nchi,vyama,mahakama na taasisi kibao ambazo zinazojitegemea hii ni uhalisia wa nature inavyotaka ila kwa bahati mbaya zaidi mifumo huwekwa ili kuvunja baadhi ya lengo, lakini pia hakuna ubaya kwa kuwa tungelikuwa tunaishi katika uhuru basi dunia ingelikuwa ni chungu kwa kila mmoja wetu.
 
Back
Top Bottom