Nimesoma nimerudia kusoma na kusoma ila nimeshindwa kuielewa hii habari ya US Dola na mafuta

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,916
6,662
Dola 747 milioni zahitajika ununuzi wa mafuta
Dar es Salaam. Mjadala wa kunusuru mkwamo wa waagizaji wa mafuta huenda ukafikia ukomo endapo Serikali itawezesha upatikanaji wa Dola 747 milioni (Sh1.9 trilioni) kwa ajili ya kufuta malipo ya bidhaa za petroli zilizoingizwa nchini kati ya Machi na Julai mwaka huu.

Kampuni za biashara ya mafuta jana zilisema zinahitaji jumla ya dola hizo, huku Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kampuni za Uuzaji wa Mafuta Tanzania (Taomac), Raphael Mgaya akisema, “Hadi kufikia Julai 21, 2023 mahitaji yote yalikuwa dola milioni 747 (Sh1.9 trilioni).

Kiasi hiki kinahitajika ili kuondoa mrundikano unaohusisha pia nyaraka za dhamana ya malipo ya dola, ubadilishaji na mikopo ya posta kutoka nje," alisema Mgaya, aliyefanya mazungumzo na gazeti la The Citizen.

"Ni muhimu kutambua kwamba bila kukamilisha mahitaji ya dola milioni 747, kampuni nyingi hazina njia za ziada za kufadhili uagizaji wa bidhaa za petroli siku zijazo,” alisema Mgaya.

Kwa mujibu wa Taomac, uagizaji wa petroli na dizeli ulipungua kwa asilimia 24.2 kati ya Januari na Agosti mwaka huu, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Aidha, uagizaji wa bidhaa hiyo ulipungua hadi tani milioni 1.43, ikilinganishwa na tani milioni 1.89 katika kipindi kama hicho.

Mgaya alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku tano zimepita baada ya Taomac kupitia kikao cha maja diliano kutoa angalizo mbele ya Waziri wa Nishati, Januari Makamba kwamba hali inaweza kuzidi kuwa mbaya iwapo changamoto ya upatikanaji wa dola haitatatuliwa haraka.

Kabla ya kuibuka kwa mjadala huo, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), wiki iliyopita ilitangaza ongezeko la Sh463 kwa lita moja ya petroli katika jiji la Dar es Salaam, baadhi ya waagizaji wakidai kutokuwa na akiba ya kutosha ya mafuta kutokana na uhaba wa Dola.

Katika kikao hicho kilichofanyika jijini hapa kwa lengo la kutafuta mwarobani wa changamoto zake, waagizaji hao walisema uhaba huo unaongeza gharama za uendeshaji wa biashara na kuathiri bei ya mafuta kwa mteja wa mwisho.

Msingi wa tatizo
Msingi wa changamoto hiyo unachagizwa na uhaba wa Dola katika mzunguko wa uchumi duniani uliosababisha kupanda kwa thamani ya sarafu hiyo inayotumika katika miamala ya kimataifa kwa zaidi ya asilimia 85.

Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), thamani ya Dola dhidi ya Shilingi iliongezeka kwa kasi kutoka wastani wa Dola 2,309 Januari 2 hadi Dola 2,409 Agosti mwaka huu.

Akilifafanua hilo, Mgaya alisema uzoefu umeonyesha kuwa sasa ni changamoto kupata kiasi hicho cha Dola 747 milioni kutoka kwenye masoko ambayo ni pamoja na benki za biashara na maduka ya kubadilishia fedha.

Pamoja na hatua hizo, waagizaji wanahitaji karibu Dola 250 milioni (kama Sh625 bilioni) kila mwezi, kwa ajili ya kufadhili uagizaji wa bidhaa za petroli katika soko la ndani.

Alisema kiasi hicho kinatosheleza uagizaji wa takribani tani 250,000 za mafuta.

Hatua za udhibiti
Akijibu malalamiko kuhusu uhaba wa Dola, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba alisema benki hiyo huingilia soko kila inapowezekana kwa kusambaza dola zaidi, pamoja na kuanzisha mpango wa dhamana ya mikopo ya nje.

Kwa mujibu wa BoT, akiba ya nje inafikia Dola bilioni 5.5 inayoweza kugharamia takribani miezi mitano ya uagizaji bidhaa nje, ikiwa juu ya ndani ya kigezo cha angalau mahitaji ya miezi minne.

Tutuba aliliambia The Citizen, BoT iliuza Dola milioni sita (takribani Sh15 bilioni) kwa kampuni za uuzaji wa mafuta zilizoomba dhamana ya mikopo benki.

Hatua nyingine zilizochukuliwa na BoT ni pamoja na kununua dhahabu na kuuza nje ya nchi ili kupata Dola za Marekani, pamoja na kupiga marufuku matumizi ya dola katika miamala ya ndani.

Mwananchi
 
Zinaletewa wa huni waje kuzipiga kupitia very weak presdent
 
It can be worse...😂😂

Sidhan kama Mwigulu alivo mpenda sifa atakubal kuangukia pua kirahisi hivi....

Shida kubwa naiona Nishati
 
Twende pole pole shida ni kuwa na fedha za Tanzania lakini hawawezi kupata dola au hawana vyote?

Dola haipo, ili waweze kyagiza mafuta hao taomac wanahitaji hizo dola million mia 6 na ushee, sasa kuzipata ndio mziki ndio maana bot nao wajaribu ku intervin ili hiyo kitu ipatikane
 
Dola 747 milioni zahitajika ununuzi wa mafuta
Dar es Salaam. Mjadala wa kunusuru mkwamo wa waagizaji wa mafuta huenda ukafikia ukomo endapo Serikali itawezesha upatikanaji wa Dola 747 milioni (Sh1.9 trilioni) kwa ajili ya kufuta malipo ya bidhaa za petroli zilizoingizwa nchini kati ya Machi na Julai mwaka huu.

Kampuni za biashara ya mafuta jana zilisema zinahitaji jumla ya dola hizo, huku Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kampuni za Uuzaji wa Mafuta Tanzania (Taomac), Raphael Mgaya akisema, “Hadi kufikia Julai 21, 2023 mahitaji yote yalikuwa dola milioni 747 (Sh1.9 trilioni).

Kiasi hiki kinahitajika ili kuondoa mrundikano unaohusisha pia nyaraka za dhamana ya malipo ya dola, ubadilishaji na mikopo ya posta kutoka nje," alisema Mgaya, aliyefanya mazungumzo na gazeti la The Citizen.

"Ni muhimu kutambua kwamba bila kukamilisha mahitaji ya dola milioni 747, kampuni nyingi hazina njia za ziada za kufadhili uagizaji wa bidhaa za petroli siku zijazo,” alisema Mgaya.

Kwa mujibu wa Taomac, uagizaji wa petroli na dizeli ulipungua kwa asilimia 24.2 kati ya Januari na Agosti mwaka huu, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Aidha, uagizaji wa bidhaa hiyo ulipungua hadi tani milioni 1.43, ikilinganishwa na tani milioni 1.89 katika kipindi kama hicho.

Mgaya alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku tano zimepita baada ya Taomac kupitia kikao cha maja diliano kutoa angalizo mbele ya Waziri wa Nishati, Januari Makamba kwamba hali inaweza kuzidi kuwa mbaya iwapo changamoto ya upatikanaji wa dola haitatatuliwa haraka.

Kabla ya kuibuka kwa mjadala huo, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), wiki iliyopita ilitangaza ongezeko la Sh463 kwa lita moja ya petroli katika jiji la Dar es Salaam, baadhi ya waagizaji wakidai kutokuwa na akiba ya kutosha ya mafuta kutokana na uhaba wa Dola.

Katika kikao hicho kilichofanyika jijini hapa kwa lengo la kutafuta mwarobani wa changamoto zake, waagizaji hao walisema uhaba huo unaongeza gharama za uendeshaji wa biashara na kuathiri bei ya mafuta kwa mteja wa mwisho.

Msingi wa tatizo
Msingi wa changamoto hiyo unachagizwa na uhaba wa Dola katika mzunguko wa uchumi duniani uliosababisha kupanda kwa thamani ya sarafu hiyo inayotumika katika miamala ya kimataifa kwa zaidi ya asilimia 85.

Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), thamani ya Dola dhidi ya Shilingi iliongezeka kwa kasi kutoka wastani wa Dola 2,309 Januari 2 hadi Dola 2,409 Agosti mwaka huu.

Akilifafanua hilo, Mgaya alisema uzoefu umeonyesha kuwa sasa ni changamoto kupata kiasi hicho cha Dola 747 milioni kutoka kwenye masoko ambayo ni pamoja na benki za biashara na maduka ya kubadilishia fedha.

Pamoja na hatua hizo, waagizaji wanahitaji karibu Dola 250 milioni (kama Sh625 bilioni) kila mwezi, kwa ajili ya kufadhili uagizaji wa bidhaa za petroli katika soko la ndani.

Alisema kiasi hicho kinatosheleza uagizaji wa takribani tani 250,000 za mafuta.

Hatua za udhibiti
Akijibu malalamiko kuhusu uhaba wa Dola, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba alisema benki hiyo huingilia soko kila inapowezekana kwa kusambaza dola zaidi, pamoja na kuanzisha mpango wa dhamana ya mikopo ya nje.

Kwa mujibu wa BoT, akiba ya nje inafikia Dola bilioni 5.5 inayoweza kugharamia takribani miezi mitano ya uagizaji bidhaa nje, ikiwa juu ya ndani ya kigezo cha angalau mahitaji ya miezi minne.

Tutuba aliliambia The Citizen, BoT iliuza Dola milioni sita (takribani Sh15 bilioni) kwa kampuni za uuzaji wa mafuta zilizoomba dhamana ya mikopo benki.

Hatua nyingine zilizochukuliwa na BoT ni pamoja na kununua dhahabu na kuuza nje ya nchi ili kupata Dola za Marekani, pamoja na kupiga marufuku matumizi ya dola katika miamala ya ndani.

Mwananchi
Nasikiaga Tanzania kuna wachumi wamesomea Harvard na Yale etc etc, vipi wako wapi? Kwa nini watu kama hawa huwa hawatumiwi?
 
Back
Top Bottom