Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,038
- 4,752
Kama tunasoma vyuo vilevile bila kujali vyama vya siasa tunavyotoka, kwanini CHADEMA wawe na timu inayoweza kufanya uchambuzi wa kina na usio na upendeleo (biasness) kwa kiwango hiki?
Kwa uchambuzi huu waliofanya, naamini hakuna maoni yaliyochambuliwa kama ya hawa watu. Taasisi na mashirika mbalimbali ikiwemo vyama vya siasa wamewasilisha maoni. Tofauti ya maoni ya makundi mengine ni kwamba hawa wenzetu walikaa wakachambua nakuandika kitaalamu na kwa lugha ambayo kila mtu akisoma anapata mantiki na anaona vision yao kuhusu mfumo wa uchaguzi nchini
Sina uhakika kama waajiriwa wa CHADEMA wanalipwa kiasi gani ila naamini wanalipwa kidogo kulinganisha na chama tawala.
Je, wanapata wapi wasomi wazuri kiasi hiki wasiopenda maslahi makubwa bali wanapenda itikadi yao? Wanawezaje kusajili watu wenye akili timamu kwa miaka zaidi ya 30 mfululizo?
Viongozi wengi wazuri ndani ya chama cha mapinduzi na wanaokubali mjadala japo kwa kiasi kidogo waliwahi kuwa chadema , viongozi wa vyama vya upinzani karibia wote waliwahi kuwa chadema. Lakini hakuna mwana CCM mwenye nafasi ya uongozi chadema kwa maana hiyo chadema imeweza sana kuwaandaa watu makini na wenye akili timamu ikilinganishwa na taasisi nyingine.
Swali la nyongeza, ni kweli kwamba haya maoni yameandikwa na wana chadema au wamelipwa washauri kutoka Mataifa na vyuo vikubwa Duniani? Kama wameandika wenzetu watanzania ; tunaweza kufahamu majina yao? Itatusaidia sana kuwapa mchongo wa kazi za uandishi lakini pia hata waliopo madarakani wanaweza wakawa chukua kuwasaidia kazi.
Huu uchambuzi unanipa moyo kwamba hatuna umuhimu wakutumia makampuni ya kigeni kwenye kesi zetu; tuandae watanzania na kwa kuanza tujifunze kutoka mfumo wa chadema.
Hongereni kwa hatua hii, niwaombe na taasisi nyingine vikiwemo vyama vya siasa waweke wazi maoni yao waliyowasilisha kwa maandishi jamii ione. Tusiwe kama Joseph Selasini ajaandika chochote cha taasisi anakwenda kutoa maoni binafsi kwa niaba ya NCCR.