Nimesitisha rasmi kuchangia harusi

Very good umejibu vizuri
 
Yesu alihudhria harusi huko kana na waliopotindikiwa na divai alifanya muujiza kwa kuleta iliyo bora. Kumbuka kuwa suala la sherehe ni la kiutamaduni na kutegemea na daraja la mtu ktk jamii husika hivyo inategemea umezungukwa na watu wenye kipato gani maana alivyonavyo vingi kwake huyo vingi vitatakiwa hii ndio kanuni ya maisha. Wengi humu tunawatoto wadogo sana ngoja wakuwe wafikie kuoa na kuolewa ndio mtajua umuhimu wa kushiriki jambo hili. Na wengi wenu mmevutana hamjafunga Ndoa ndio maana mnapinga jambo hili.
 
Bahati mbaya sijaoa lkn nachangia sana harusi za watu lkn good news is bro zangu wameshaoa na hakuna aliyechangia harusi ilikua ni party ndogo lkn classic so sitegemei kuchangiwa na mtu.
 
Nishasahau hata arusi ni kitu gani, ila TBC kipindi cha chereko kimenikumbusha mbali sana.......enzi hizoooo
 
kuwa na formula katika maisha yako upande wa matumizi ili usijiumize wala usionekane mchoyo na mbinafsi maana ukweli ni kuwa maisha ni watu na watu ndo hao....unaweza fanya hivi kuwa ukatenga kila jumla ya kipato chako 10% ndio itakuwa mgao wakusaidia au kutoa mchango kwa watu...ikiisha wasubiri tena mzunguko mwingine,kwa kufanya hivyo utaepusha maumivu kwako na jamii inayokuzunguka...lakini zaidi pia toa fungu la kumi...
 
Bahati mbaya sijaoa lkn nachangia sana harusi za watu lkn good news is bro zangu wameshaoa na hakuna aliyechangia harusi ilikua ni party ndogo lkn classic so sitegemei kuchangiwa na mtu.
Bro zako watakuchangia na watashirikisha rafiki zao kukuchangia. Ndoa ni jambo la baraka na ni tukio muhimu sana linafanana na la msiba tofauti msiba hatuupeleki ukumbini ila gharama ni zilezile.
 
Siku hizi sio harusi tu. Michango ipo kwenye Ubatizo, Kipaimara, sijui mtoto "kafaulu" kutoka chekechea kuingia standard one na mambo luluki yasiyo na tija. Kina mama wengi ndio wanaotuingiza kwenye hii mitego.

Changia pale inapobidi na sema NO bila haya pale unapoona hii haijakaa sawa. Mtu atanuna siku 2 ila maisha yataendelea tu
 
Bro zako watakuchangia na watashirikisha rafiki zao kukuchangia. Ndoa ni jambo la baraka na ni tukio muhimu sana linafanana na la msiba tofauti msiba hatuupeleki ukumbini ila gharama ni zilezile.
Ndg usilazimishe mambo ya kuchangiwa na rafiki za bro zangu hayo hayapo, Kwny harusi zao tulijipanga kama familia tu.Baba, mama na watoto wa familia basi hakuna mchango nje ya hapo. Walipewa mwaliko watu wa karibu basi na kilikua hakuna mambo ya kitchen party, send off afu harusi. Sherehe ilikua ni harusi only.
 
Bro zako watakuchangia na watashirikisha rafiki zao kukuchangia. Ndoa ni jambo la baraka na ni tukio muhimu sana linafanana na la msiba tofauti msiba hatuupeleki ukumbini ila gharama ni zilezile.
Bro samahani wewe ni mc, au unakodisha vifaa vya mziki au unamiliki ukumbi wa harusi?
 
Mimi Huwa sichangii harusi ya mtu yoyote na wala sijawahi kuchanga harusi ya mtu yoyote, Nimeoa sikuhitaji mchango wa mtu yoyote niliwaalika watu tu kwenye harusi, na kuwaambia hakuna michango.

Nilichogundua kama unataka kuona basi ujipange kwa gharama za harusi yako sio kuwapa watu gharama au majukumu yasio wahusu.

Siipendi michanga ya Harusi na wala siisapoti michango ya kjinga kama hiyo. Natoa michango ya Mazishi tu sio harusi
 
Michango ya harusi mbali na kutufilisi, pia ina changia sana ndoa kuvunjika..... Maana kuoa ama kuolewa imekuwa jambo rahishi tu unachangiwa mradi sherehe iwepo hata kama mtu hana nia ya dhati ya kuoa ama kuolewa...... Miaka yetu kipimo cha ukweli kama mtu anataka kuoa kwanza utatafuta pesa, ili apate posa na mahali ya kulipa (Iwe pesa ama kitu kingine cha thamani kama ng'ombe nk) Na kwa muoaji wa dhati kabisa hata kama itachukua miaka 5 ama zaidi kutimiza hayo mambo atahakikisha anapata.......... Hicho kinakuwa kipindi tosha cha kujua kama mtu yupo serious ama anaigiza. Nilishaapa sitachangia ndoa kwasababu hata mimi nilihangaika mwenyewe binafsi kupata Posa na baadaye Mahali.....
Zaidi zaidi ninachoweza kufanya labda kukopesha mchango wa harusi lakini kutoa bure HAPANA KABSAAA!
 

Harusi nyingine za kifahari sana na mwenye harusi anategemea kianzio toka kwenu.......hatutaki kufanya kitu kuendana na hali yako.....unataka kufanya harusi kama ya fulani wakati mfukoni huna kitu.unategemea michango ya watu
 

Dear even me hautanichangia ? Mine it's only one wedding and I promise you I will be good to my husband so it can last ..aaaahhhhaaaaa... Pole sana ... Halafu Tz harusi zilivyokuwa big deal shurti competition and the end the marriage won't last .. Some wakoRadhi walipe michango ya harusi ili tuu waka party huku kids don't have school fees .. Ouch, haijaniingia yet .. Thanks ....
 
Huwa sitaki kusikia kabisa kuhusu michango hii. Tangu nikiwa shule miaka hiyo nilijiapiza kua sitachangia mtu hela yangu afanye starehe zake hizo za kuoana sijui na kwenda honeymoon
Sijawahi changa na sitakuja kumchangia yeyote. Mimi nilipoamua kuoa nilifanya kiparty kidogo kilicholingana na uwezo wangu nikawaalika ndugu na jamaa tukala tukanywa na tukafurahi pasipo kumchangisha yeyote
Sitaki na huwa sichangii harusi kabisa
 
Ukitaka kuacha kuchangia harusi sharti uzichukie kwanza moyoni mwako na usiwe unahudhuria harusi. Watanzania wamemajor sherehe na kuminor maendeleo
 
Mama you have said it all, what else can i say?
Stay blessed
 
Kwa nnavyoona ni bora michango iwekwe limit kulingana na idadi ya watu wanaohudhuria harusi itakuwa afadhali sana.
 



Kwani mume anachunga mbuzi si ameolewa mumewe afanye
 
Hivi kwa nini watu hupanga kufanya mambo ambayo hawana uwezo nayo na mwishowe wanaishia kuwa kero tu kwa wenzao?

Kwani hawawezi tu kufunga ndoa bila makeke kama uchumi hauruhusu?
 


Hili linawezekana kabisa. Nina mwaka wa pili sasa sijachangia harusi yoyote.

Nilichokifanya nimejitahidi kuwa mwaminifu kulipa fungu la kumi kanisani sawasawa na Malaki 3:8-12. Maamuzi ni ya kwako na kupanga ni kuchangua..... Linawezekana kabisa.

Malaki 3:8-12 Imeandikwa ....... 8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu.
9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote.
10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
11 Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.
12 Na mataifa yote watawaiteni heri; maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…