Hii ina maana gani pale mtu unapoota ndoto kama hii;
Siku moja tulikuwa watatu, mimi na wasichana wawili katika ghorofa fulani floor namba 7. Wale wasichana waliniaga wanapanda lift wanakwenda floor 1, kwani wanawahi harusini. Dakika 1 baadaye nikawaona wakitembea kule chini ikimaanisha kuwa walishashuka katika lift ile.
Nami nikapata wazo nishuke Ground hivyo nikapanda katika lift ile. Kama ilivyo ada nikapress G, lakini kama dk 5 lift haikusimama ni kama ilikua na kasafari karefu. Baada ya hapo nilipoteza fahamu, nilikuja kuzinduka naskia sauti ikisema "TOKA NJE".
Nilivyotoka nilistaajabu kuona mji uliojaa majengo mazuri, nikaangalia simu yangu inaonesha saa 7 mchana tarehe 14, Wakati memory yangu nilipokuwa na wale wadada ilikuwa tarehe 13.
Wakati nawaza alitokea jamaa flan nikamuuliza hapa ni wapi, akasema hapa ni KUZIMU, duniani ni floor namba 1, nikaamka kutoka usingizini.
NINI TAFSIRI YA NDOTO HII?