Nimenunua Unga wa sembe kilo 5 kwa Tsh 8500/= sawa na Tsh 1700/= kwa kilo. Je hii ndio bei au nimepigwa?

Huu mwaka ukiwa na mtaji utapga pesa mpaka basi kwnye nafaka
 
Week kama mbili zilizopita nimenunua 10kg kwa sh 16,000/= hapo Kawe mwisho sokoni. Nikamind sana yule muuzaji maana kabla ya hapo nilinunua elfu 12 kwa 10kg kwa mtu huyo huyo ila akajitetea kuwa bei zimebadilika, nikanunua zangu nikasepa. So, kupitia huu uzi sasa ndiyo napata picha maana mm mwenyewe nilihisi labda nimepigwa
 
Serikali yetu yadanganya kuhusu inflation rate, nina uhakika inflation Tz inafikia 10pc au zaidi
 
Huu mwaka tutanunua mpaka 2000 tutunze kilichopo hali in mbaya mashambani
Nilipanda mahindi heka 4,mvua ilivyonifanya we acha tu, mwaka huu na ujao ukiwa hivi hali itakuwa tete saana..

Na kwa mabadiliko ya tabia nchi, huu ndii uhalisia, hali itazidi kuwa mbaya siku kwa siku, navionea huruma vizazi vijavyo, ukame utatawala.
 
Back
Top Bottom