Nimenunua Hisense mpya Ila sometimes volume inajishusha yenyewe mpaka 0

Nilinunuaga hisense 43 mtumba aliniagizia mpemba mmoja ni brand ya UK 4k asee ile chombo ni balaa hizi zinazouzwa kkoo nyingi feki aliniuzia bei kubwa ila ile tv ni nzuri kuanzia picha sauti mwonekano nk
 
SAMSUNG, LG, SONY hizo zingine kulia muda wote!!!
Binafsi natumia LG muda mwingi iko "on" asubuhi- usiku, na haijawahi hata kununa😄😄
 
Wakuu Msaada pls,

Nimenunua Hisense dukani, nakuja home nimenotice kila baada ya muda flani sauti inajishusha mpk 0..na pia kuna kaujumbe kanaanzia na REVERT. Nisipobonyeza any button TV inajizima na kurestart.

Msaada Please.

Sent from my SM-N960U using JamiiForums mobile app
Chief-Mkwawa
Inawezekana ipo store mode mkuu, ama mode yoyote ambayo sio kwa ajili ya mtu wa kawaida kutumia.
Sababu ni mpya ireset ianze upya pia kwenye setting kama ipo store mode itoe.
 
Hii haina maana kuwa ni feki, TV za siku hizi ni complicated kama simu au computer so kuna vitu vingi vinaweza "kuharibika" hasa katika software.

Kwanza jaribu kutoa betri kwenye remote uone kama inaendelea kuleta shida inaweza ikawa button ya volume imenasa.

Kama haujaconnect TV na internet jaribu kufanya hivyo, kisha update firmware, hii inaweza ikarekebisha tatizo lako. Unaweza kutumia hotspot ya simu.

Kama yote hayo hayajatatua tatizo fanya factory reset.

Nakili ujumbe mzima unaosema Revert..
 
Inawezekana ipo store mode mkuu, ama mode yoyote ambayo sio kwa ajili ya mtu wa kawaida kutumia.
Sababu ni mpya ireset ianze upya pia kwenye setting kama ipo store mode itoe.
Kiongozi wapi wanauza Hisense Og na nitaijuaje?
 
Kiongozi wapi wanauza Hisense Og na nitaijuaje?
Kuna wakala wengi sana, Mjini pale karibu na pizza hut kulikua na official shop sema bei zimechangamka mno, kkoo huku unapata bei rahisi zaidi.

Hisense wana software yao vidaa ni proprietary. Angalia tu software ukikuta vidaa ni hisense yenyewe.
 
Back
Top Bottom