Nimekutana na wanafunzi wamebeba fimbo na wameagizwa na mwalimu wao.

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Feb 26, 2024
5,853
11,930
Kwanza WAALIMU tunawapenda sana ndio maana tumewaamini kuwafundisha Watoto/wadogo zetu.

Lakini hii imekaaje unatoa oda zaidi ya wanafunzi wa 5 wakuletee fimbo za kuwaadhibu?

Hatukatai adhabu lkn mara kadhaa tumeshuhudia waalimu mkilemaza Watoto wetu na kuwatia kilema Cha maisha!

Wanafunzi wanasema Kila siku huagizwa fimbo 5 na wako Saba.
Tumewauliza hizo fimbo Huwa zinaisha Kila siku wamekubali.

Sijui malengo yenu zaidi lakini kama kufundisha tu mwe mnaagiza fimbo kiasi hiki Mimi kama mzazi napinga Kwa nguvu zote.

Zile fimbo nimezichukua nimehesabu ziko fimbo 17 na hizi ni wanafunzi watatu tu kati ya Saba ambao wao sikuwaona.

Nimewapa no zangu za simu na subiri Kwa hamu sana huyo mwalimu anipigie. Nimewambia pia wanafunzi jioni wakirudi wanipigie simu kama amewapiga kesho nimfate hapo hapo shuleni.

Nilichowaza ni hiki Kwa fimbo hizi kama mwalimu yuko na hasira Kali anaweza kuua wadogo zetu ama kuwajeruhi vibaya mno nikaadhimu Mimi na jamaa angu kuzichukua hizi fimbo kesho ama kesho kutwa zitakauka nipikiwe hata dagaa Nile.

Kwako mwalimu Mpwayungu Village
 

Attachments

  • IMG_20240918_074947_706.jpg
    IMG_20240918_074947_706.jpg
    246.9 KB · Views: 5
Kizazi cha Woga na Ulofa kinaandaliwa hivyo. Ni kama kilivyoandaliwa kizazi hiki tulichopo, kimezalisha products za uoga, uchawa, kusifu na mengi ya hovyo.
 
Karibu Tanzania 🇹🇿 huku Iringa wanatumwa Mianzi mibichi 😃
 
Ndugu mzazi hata kama wawapenda hao wanafunzi ila hukutumia busara shekh wangu!

Nenda shuleni, katoe maoni kwa mkuu wa shule! baada ya hapo kaa kwenye nafasi yako!

Walimu si wehu ndugu zangu.
 
Nilichowaza ni hiki Kwa fimbo hizi kama mwalimu yuko na hasira Kali anaweza kuua wadogo zetu ama kuwajeruhi vibaya mno
Mkuu unafanya judgment kwa hisia sana bila kutumia LOGIC. Hio itakuja kukuletea shida siku moja.

Yajue ya kuzingatia ili uachane na yasiyokuhusu. Na kama ukiona ni muhimu sana unahitaji kufahamu jambo basi nenda kwa wahusika ukahoji na upate majibu.

SHULENI viboko vinaruhusiwa kitaratibu na kisheria, na viboko huwa haviagizwi kwa mafundi seremala wala Serikali haipeleki viboko mashuleni.

Be a Man.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom