Nimekua Tabora, pazuri ila nimelishwa vumbi, Afrika tusichekane

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
32,238
50,413
Barabara ya kuanzia Manyoni kwenda Tabora ukiacha ile ya kupitia Singida, nusu yake nakisia kama kilomita 150km (equivalent of Nairobi to Nakuru) haijatiwa lami, ni vumbi tupu. Na kuna maeneo yenye makazi ya watu pembezoni. Hapo vumbi balaa, kiasi kwamba unatamani kuona hata ishara ya lami.

Lakini yote tisa, Tabora pazuri watu wa pale wakarimu na hawana hulka za kibaguzi, wageni tukifika tunafanya biashara zetu kwa amani na kugeuza bila matatizo. Hali ya hewa nzuri, vyakula vitamu maana vinatokea moja kwa moja shambani. Japo maji kwenye mabomba hotelini ni tatizo kama ilivyo mikoa mingine kama Morogoro.

Japo nilipata raha pale Isevia na Oxygen, watu wa Tabora humu JF watanielewa nikitaja Isevia.



 
Wewe ni dereva wa basi kumbe? Au ni lorry hilo
Na biashara gani unaenda kufanya Tabora? Umelipa kodi stahiki?
Umeingia Tanzania kihalali? Do you have all papers?
 
Sehemu pekee iliyo baki nyuma ni Hili eneo
yaani hii mikoa ya Magharibi
kigoma na Tabora
lakini kwa sasa kazi inaendelea,
Hiyo barabara ina mkandarasi tayari
Hata kenya kuna barabara bado zina vumbi

Ndio maana nikasema kwenye title yangu kwamba Afrika tusichekane, najua kuna maeneo Kenya yenye barabara ya vumbi hususan kaskazini ambapo kuna watu wachache huko. Japo hiyo yenu niliona kama ni 'National Trunk Road' au type B. Sidhani kama Kenya tuna type A, B na C ambazo bado ni murram, I stand to be corrected.
Nilikua najua ile ya Kitale-Lokichar lakini imeshughulikiwa kwa ajili ya mafuta ya Turkana.

Anyway tutafika tu.
 

Hiyo barabara wameigawa vipande vipande
80% Imesha jegwa kwa lami
Kipande kirefu nihicho kutoka kigoma au kwenda Kigoma
Ukifika Tabora mjini
Hiyo barabara unapiga Lami 200km
Then kuna vumbi tena 30km
unapiga lami mpaka Kigoma
na maeneo hayo yoote kama ulitoa macho nje
uliona Wakandarasi wakiendelea
 
I use to think Nairobi-Nakuru is very far.. kumbe Kenya ni ndogo sana.. wakati mwingine huwa nasahau Tanzania ni 52% ya East Africa ukiitoa South Sudan.
 
I use to think Nairobi-Nakuru is very far.. kumbe Kenya ni ndogo sana.. wakati mwingine huwa nasahau Tanzania ni 52% ya East Africa ukiitoa South Sudan.

Kuna watu wanaishi Nakuru na wanafanya kazi Nairobi, yaani gari ukiichezea kwenye 100km/h halafu bararabara yenyewe imenyooka mbona Nairobi unafika ndani ya muda mchache sana.

Aisei Tanzania ni kubwa, binafsi nimetembelea mikoa yenu mingi, yaani nalala na kuamka na kulala mara kadhaa na hatufiki, madereva wenu wa mabasi wana nguvu sana, halafu huwa naona kuna polisi wana zile radar za kukamata taarifa za kasi, hivyo inabidi dereva asafiri taratibu kwenye chini ya 80km/h.
 
Ndio maana tunatamani sana reli ikamilike.. maana safari ya kigoma itakuwa unaondoka Dar na kufika kabla jua halijazama..
 
Ni pale mtu anapotoka nje ya main highway na kuongelea dust road! Swali rahisi ni je Dodoma-Singida ipo paved ama hapana? Na Tabora-Mwanza je?
Tabora Mwanza kuna 278km na hakuna vumbi ni lami kwenda mbele
Hata barabara hii anayo zungumzia yeye
Ipo inajengwa
 
Wewe ni mwongo nahisi hujafika huko umesimuliwa,
Hicho kipande ni km80, halafu sio kuanzia manyoni, ni mbele ya Itigi ndio hicho kipande kimeanzia,
Halafu kama hutaki vumbi ungepita Singida-Nzega-Tabora, ungefurahia mkeka saaafi kabisa.
Uachage majungu.
 
Wewe ni mwongo nahisi hujafika huko umesimuliwa,
Hicho kipande ni km80, halafu sio kuanzia manyoni, ni mbele ya Itigi ndio hicho kipande kimeanzia,
Halafu kama huftaki vumbi ungepita Singida-Nzega-Tabora, ungefurahia mkeka saaafi kabisa.
Uachage majungu.
 
 

Tatizo unasoma kwa mihemko hadi unakosa kuwa makini ili uelewe nimesema nini. Rudia vizuri nilichoandika utaelewa.
Nimetumia neno 'nakisia'
Halafu nimesema nakisia nusu yake, hivyo sikusema vumbi limeanzia wapi.
Ukianza hapo Manyoni, unakwenda kwa lami, kunazo signs pembeni zinazokuonyesha Tabora ni KM ngapi. Unatiririka kwa raha zako maana lami yenyewe tamu, hadi ghafla unazinduliwa kutoka usingizini maana mnaingia kwenye sehemu ya murram na vumbi.
Sasa hapo kwa murram inabidi kukisia maana hakuna hizo signs za kuonyesha umbali, baada ya kusafiri kwa muda hadi kukata tamaa kwamba hamna lami tena, ndio hatimaye ghafla unaunga kwenye lami na kupiga kilomita kadhaa hadi Tabora.
Halafu huko mnanitajia Mwanza na kwengine sijui mnataja vya nini maana sijaongea kuvihusu. Mbona kutokea Dar-Dodoma-Manyoni pako freshi tu hadi nililala bila matatizo.
Hehehe halafu hilo la majungu sijui umelitoa wapi .... Mwangaluka
 
Ajabu sana.....kwani kuna nini kinaendelea?

Mbona MK254 amekuwa mstaarabu sana Leo? There must be something wrong going on somewhere...

Anyway MC254 una.....feel......aje...mazee?

Hehehehe!! Mbona mimi mstaarabu siku zote...
Tatizo mkitembelewa na mgeni mnataka ataje mazuri yote bila doa hata moja, nikitaja doa mnatiririka povu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…