Nimekosa amani ya moyo ni Wiki ya pili sasa

Old Suspender

Senior Member
Feb 1, 2024
134
296
Habari za jioni wanaJF, kwanza nitangulie kusema sina mgogoro wowote wa kifamilia, kuhusu kazi sio mwajiriwa ni mchakalikaji wa mtaani, sina madeni ya kutisha ambayo may be yanaweza kunipa stress, ingawa nina hofu ya kutofikia lengo ifikapo 30 june mwaka huu hali ambayo nahisi itaniathiri sana na kufanya maisha yangu kuwa magumu sana kwa kipindi cha takribani miezi minne.

Kwa siku za hivi karibuni nimekuwa nikishikwa na wasiwasi sana hali ambayo inanipelekea kuwaza sana, nimekuwa mtu wa hasira na mawazo hata pindi ninapohitaji kuongea na familia yangu, nmejikuta mara nyingi nashikwa na hasira sana na sitamani waniambie chochote ukizingatia niko nao mbali kwa takribani miezi minane sasa, hii hali hata mimi binafsi inaniumiza sana, huwa natamani kuongea nao lakini pindi tu tunapoanza kuwasiliana najikuta nashikwa na hasira na kutamani kusitisha mawasiliano muda mwingine huwa nawakatia simu.

Wakuu sina amani moyoni, ninahisi nitapata magonjwa ya moyo, jana usiku niliwaza niondoke nirudi home niachane na hii project nayofanya labda nitapata unafuu lakini ukwel ni kwamba hii project ndio naitegema angalau kufikia end of june inipe angalau sent ya kuniweka mjini.
Wakuu naomba kama kuna mtu alishakutana na changamoto hii anisaidie namna ya kuitatua. Please naomba sana wakuu nisaidie sipo sawa kabisa.:4WeirdJam::4WeirdJam:
 
Umepatwq na janga gani
 
Kamuone msaikolojia....

Kutamani kuacha kazi ni dalili ya kuchoka kihisia(burnout)

Kukasirikia watu wako wa karibu, hiyo inaweza leta dysfunctional relationships pia ni dalili mbaya

Mimi sio mtaalam nimejaribu kuvaa viatu vyako tu.
 
Back
Top Bottom