Uchunjuba Punjubi
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 799
- 622
Habari yenu wakuu, bila kupoteza muda naomba kwenda moja kwa moja kwenye lengo la kuanzisha uzi huu, naomba sana ushauri wenu kuliko kejeli na kunicheka, maana kiukweli napitia kipindi kigumu sana, baada ya mchumba wangu au mke wangu mtarajiwa, kuniambia kitu ambacho kimeniumiza sana katika moyo wangu.
Ni hivi, mimi na huyu binti tulikutana yapata mwaka mmoja na nusu hivi, tulipendana na kuheshimiana sana, kiukweli alikuwa chaguo sahihi sana kwangu, katika nyanja zoote. Mzuri, ameshika dini, haniombi pesa mpaka nimpe mwenyewe hana makuuu.....na sifa nyingi kem kem za kuitwa wife material.
Kutokana hali hii nilijikuta naingia gharama nyingi sana sababu yake hasa ukizingatia nilikuwa namuamini sana huyu mwanamke, na pia niliona ni wajibu wangu kumhudumia kwa sababu ni mwanamke wangu, na kutokana na jinsi tulivyoishi hatuwahi kabisa kufanya mapenzi, alidai ye ni bikira, sikuweza kuwa na uhakika lakini kutokana na jinsi alivyo na tunavyoishi kwa asilimia kubwa niliamini hilo.
Sasa ilitokea kuna kipindi mimi nikahamishwa kikazi toka sehemu tulipokuwa tunaishi pamoja na huyo mchumba wangu, hivyo tukabaki tunawasiliana tu na kupanga mipango kabambe juu ya maisha yetu yajayo, nilikuwa nina furauha sana juu ya huyu mwanamke.
Lakini kuna kipindi alinipigia simu akadai anaumwa sana, nikimuuliza nini shida akawa hanielezei ukweli, anaficha ficha, kadri muda unavyoenda kuna kipindi akawa hapatikani kabisa hewani, muda ukaenda lakini baadaye akaja kuwa hewani kwa namba nyingine alisema alipoteza simu ndio maana alikuwa hawezi kuwasiliana na mimi, nilikubali na mawasiliano yakaendelea kama kawaida. Mapema mwakani nilikuwa nina mpango wa kumuoa, na tulishaanza kuandaa mipango yetu itakavyokuwa lakini.
Wiki iliyopita kumetokea shida, kwake anachukulia ni ndogo lakini kwangu ni shida kubwa na kiukweli japo kaniomba msamaha na nikatamka kwa mdomo kwamba nimemsamehe, lakini moyo umegoma, pamoja na kumpenda koote lakini kwa hiki alichofanya Nimeshindwa kabisa Kumsamehe.
Anadai kautoa kafara usichana wake ili aweze kupona, kile alichokuwa anaumwa. Anadai ndugu zake walitaka kumtoa kafara wamuue, sababu kuna mipango yao alikuwa kashaijua hivyo walikuwa wanaenda kummaliza kabisa na atoweke katika ulimwengu huu.
Kile kipindi alikuwa anaumwa kumbe shida ndio ilikuwa hao ndugu zake walikuwa wanamsumbua, na alishauriwa na rafiki zake waende kwa mganga ambaye anatibu kwa majini, na huyo mganga alichomwambia tiba yake ni kuutia huo usichana wake kwa mwanaume ili wale ndugu zake wasiweze kumtoa kafara.
Anachosema ilibidi mimi ndio niende nikafanye hiyo kazi, lakini alishindwa kuwasiliana na mimi sababu hakuwa na simu na alikuwa hoi sana, na yule mganga ni mwanamke hivyo ilibidi atafutwe jamaa ya huyo mganga ndio aifanye kazi hiyo.
Ya kumbikiri Mke wangu mtarajiwa . Niliumia sana, zaidi ya Sana kiukweli nilimwambia, zama hizi akili yako inafikiria vitu kama hivyo? Ulishindwa kutafuta japo simu au kumpa mtu namba anitafute tupeane japo ushauri? Maana shida zake nyingi sana nilimtatulia lakini sijui kwa nini hili hakutaka nimsaidie?
Nimejitolea vingi sana kwa huyu mwanamke, nimepoteza muda, na moja ya vitu nilivyokuwa natarajia toka kwake na nilimsisitiza ni kuutunza usichana wake kwa ajili yangu, sababu katika maisha yangu sijawahi kumbikiri mwanamke, na nilikuwa natarajia hapa, me sio mtu wa wanawake, ni mtu najiheshimu sana. Nilikuwa namuamini na kaniomba sana msamaha lakini nimeshindwa kumsamehe japo mdomoni nilimwambia yameisha.
Anasema kama angeamua kunificha kuhusu hili asingeshindwa kabisa kwani amefundishwa jinsi ya kuurudisha usichana wake,na mimi hata ningekuja kumuoa nisingegundua chochote, ila ameamua tu kusema ili kuniweka wazi. Nilimpenda lakini ameniangusha sana kwanza kuamini Ushirikina na pili kuugawa usichana wake kwa mtu tu, mpita njia.
Alilia sana na kunisihi nimsamehe maana hakuwa na jinsi zaidi ya kufanya hivyo ili kuokoa maisha yake, yuko tayari nimuoe hata awe mke wa pili lakini sio kumuacha, nilimkubalia, lakini kiukweli nafsi imegoma kabisa kumsamehe, tunawasiliana lakini hayupo tena moyoni mwangu.
Najua wapo wanaume Wenzangu, wanaooa wanawake ambao walishazalishwa, au waliofanya matukioa zaidi ya huyu wangu lakini kwangu imekuwa ngumu kumsamehe, nataka kumfanya awe rafiki tu na sio Mke kama ambavyo tulipanga.
Ushauri wenu tafadhali, mwenzenu nimekwama najipanga kutafuta mchumba mwingine, nioe haraka.