Nimeishi Moshi, Bukoba, Lushoto aisee watanzania tuna ukarimu sana tofauti na tunavyoshambuliana kwa tofauti zetu

Tanzania sehemu nyingi Tu unaishi kama hutokuwa mjivuni na kiburi,

Na kama vijijini ndio rahisi, unawaonesha Tu kuwa umependa tamaduni zao na kuwanogesha zaidi unajitahidi kujifunza hata lugha yao. Watakupenda haswaaa

Ila Kuna wengine hasa wale born town, unaenda uhayani, uchagani, usukumani, ungonini au kabila yoyote ile maarufu. Kwa
fikra zako mbovu za kuskia, unaanza kuwakejeli na kuvimbia wenyeji,

Nikuambie tu, wakikukomesha unastahili
 
Nimebahatika kufanya kazi karibu wilaya zote Tanzania nzima Ila mkoa wa Tanga pamoja na wilaya zake zote toka kilindi, kwediboma, Handeni, Korogwe, Lushoto, muheza, tanga mjini Mpaka Mkinga kwa wadigo ndo the best place kwa kuishi na watu wakarimu. Nimetembea Tanzania nzima Ila hakuna sehemu nzuri unayoweza kuishi kwa Raha na amani kama Tanga.
Ukikaa Tanga huwezi kupachoka miaka 800 na usipokuwa makini unaweza amia mazima Kama ww ni mgeni.
 
Watu safi watanzania, mimi nimekaa kahama, nmefanya biashara huko mbeya ubaruku, nimekaa kidogo iringa, nna rafiki zangu toka arusha na moshi kama ndugu. Nina rafiki zangu wakurya, aisee ukiwa na rafiki mkurya kama anakukubali jua anakukubali kweli hata kupgana kwa ajili yako anaweza.
Tanzania ni sehemu safi kabisa kokote unaishi. Na saa nyingine wakijua wewe ni mgeni unakuwa mashuhuri kila mtu anakufahamu na kukurefer kwa jina la clan yako. Kama unafanya biashara utaskia, pale duka la flani utapata
Nenda pale saloni kwa mndengereko ukanyoe!!
 
Nipo Arusha sina ndugu hata mmoja ninaye mjua huu mkoa lakini najihisi nipo nyumbani.

🇹🇿❤️
Arusha ukiwa mgeni na haujaja kuleta competition na biashara/mbishe za watu utaishi fresh tu,yaani unatakiwa kua fala flani hivi ili uishi fresh.Lkn ukija Kama mpambanaji na umeleta competition ya maana utaukimbia huu mji.

Nimeongea Kama mzaliwa na mwenyeji wa hapa.
 
Unaposema mgeni unamaanisha nini?
Mtu asiye kabila la hapa ama mhamiaji yeyote?

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Aisee nimejifunza kitu kimoja kuhusu sisi watanzania baada ya kutembea mikoa tofauti na kuishi huko. Watanzania tunaweza kuwa tunatofautiana na kurushiana maneno mitandaoni juu ya sijui kabila fulani, hivi mkoa fulani hivi..ila kiuhalisia tunaishia kwa upendo sana.

Ok kiufupi, nimezunguka mikoa mingi..nimeishi Kagera aisee ilikua safi majirani na watu walikua na upendo sana japo sikua mwenyeji.

Nimeishi moshi big up sana kuna wajamaa waliiishi na mimi kama mdogo wao na hata kunisaidia naul kurudi Dar nilipokua hali tete braza George Mramba big up popote ulipo ulinisaidia first day kiuaminifu sana kama mdogo wako.

Unakaribishwa chakula tena unalizimishwa aosee wwtu wa mikoani big up sana ila na kiujumla watz safi sana.

Lushoto nimeishi lukozi napo ilikua safi sana watu walikua wakarimu vibaya mno kama wanakujua. Aisee watz sisi safi sana!
Ha ha ha wahaya walikuchangamkia bila shaka walikuwa after something.
 
Naunga mkono hoja yako pal, Zawadi kubwa tuliyopewa watanzania inawezekana kuliko hata waafrika wengine ni Upendo na ukarimu, Watanzania ni wakarimu mno nahisi ndio sababu ya umaskini wetu.

Mwanzo nikienda vijiji vya mkoa wetu jinsi majirani wanavyotupokea na kutupa vyakula nilikia najua ni mkoa wetu ndio wakarimu sana kumbe ni karibu mikoa yote. Mikoa yote niliyokua naishi nimeshuhudia upendo na ukarimu wa watanzania tena sehemu hizo unakuta hauna ndugu kabisa ila Unaishi kwa amani. Eg, Usukumani, Unyaturuni, Wandengereko, Wachaga/Masai nimekaa kwa raha sana, Wanyakyusa pia wakarimu sana asee..

Zanzíbar watu ni wakarimu sana ghalama ya kupata kitu chochote kwa Shamba ni kusema "naomba" Shida yao sometimes udini unawameza kiasi but nao wakarimu sana.

Dar ndio wwtu wanaishi kama magaidi ukipanda gari kila mtu anamuona mwenzake Mwizi, hata ukiulizia njia hasa maeneo ya Ubungo, kino,temeke, ilala Ndio kwanza mtu anakutafutia chance ya kukuibia/tapeli.
Hii ndio maana iliitwa bongo ukizubaa unapigwa chap kwa ukali😅
 
Aisee nimejifunza kitu kimoja kuhusu sisi watanzania baada ya kutembea mikoa tofauti na kuishi huko. Watanzania tunaweza kuwa tunatofautiana na kurushiana maneno mitandaoni juu ya sijui kabila fulani, hivi mkoa fulani hivi..ila kiuhalisia tunaishia kwa upendo sana.

Ok kiufupi, nimezunguka mikoa mingi..nimeishi Kagera aisee ilikua safi majirani na watu walikua na upendo sana japo sikua mwenyeji.

Nimeishi moshi big up sana kuna wajamaa waliiishi na mimi kama mdogo wao na hata kunisaidia naul kurudi Dar nilipokua hali tete braza George Mramba big up popote ulipo ulinisaidia first day kiuaminifu sana kama mdogo wako.

Unakaribishwa chakula tena unalazimishwa aisee watu wa mikoani big up sana ila na kiujumla watz safi sana.

Lushoto nimeishi Lukozi napo ilikuwa safi sana watu walikuwa wakarimu vibaya mno kama wanakujua. Aisee watz sisi safi sana!
Bukoba ulisha fanya nao kazi ofisini ukajua usemacho? Kilimanjaro pia changanya na waMeru. Sehemu pekee inakaribisha wageni pasi kuwabagua ni Kanda ya Usukumani na Kusini, kila mtu hua ana lake la kusema na tukitaka kusema hapa tutazua mjadala mkubwa usio na faida
 
Back
Top Bottom