txyz
Member
- Apr 3, 2014
- 89
- 48
Bila shaka ni umasikini wa fikra tu kufikiri Kuzungumza lugha yako ni ujinga.Nawashangaa watanzania wenye wrong vision km hii.wakati tunalilia kuitangaza lugha yetu kimataifa,wanataka Rais wetu azungumze English wakati yeye ndo mtanzania namba moja anayepaswa kuitangaza lugha yake .Lini Obama akatumia lugha isiyo yake.Rais wa china alipokuja Tanzania alizungumza lugha gani?Mwacheni Rais wetu adumishe Utamaduni wetu.Wataalamu wa lugha wanasema"There is no superior language".Lengo la lugha ni kuwasiliana.Umesikia wanyarwanda wamelalamika hawajamwelewa Nyerere Junior!Lengo la lugha ni kufikisha ujumbe. Watanzania tumwunge mkono Rais wetu,tusimkatishe tamaa. Kiingereza si lugha yetu,ni ya wakoloni. Magu ongea hicho kikoloni inapobidi,mradi ujumbe ufike.