Mkuu, hiyo ni hatari sana, kumbuka kuwa ulikuwa umefunga milango/mlango na bado umjikuta umenyolewa, kwa maana rahisi ni kwamba mtu huyo anauwezo wa kuingia chumbani kwako ilhali mlango umefungwa. Unachotakiwa kufanya hapo ni kumshirikisha Kiongozi wako wa kiroho ili akushauri cha kufanya, ukitulia watakuja tena na safari hii wanaweza fanya makubwa zaidi kama kujikuta umelala nje ya nyumba au baharini.Habari wana JF
Leo asubuhi kimenitokea kitu kilichonipa maswali mengi sana kwa sababu sijawahi kutokewa na kitu kama hiki.
Mimi ninaishi pekeyangu kwenye nyumba hizi za kupanga, na kabla sijalala huwa ninahakikisha nimefunga mlango wa chumba changu.
Cha ajabu leo nilipoamka nimekuta nimeona nimenyolewa kidogo upande mmoja wa kichwa kitu kilichonishangaza sana (nivile tu ukristu wangu umenipa ujasiri) ni kama umeenda kwa kinyozi badala ya kukunyoa akakuchonga juujuu upande mmoja tu wa uso wako. Nimejaribu kutazama kwenye shuka sijaona nywele.
Hivi kimeshawahi kuwatokea hiki kitu? Nini hasa inaweza kuwa dhumuni la huyu mtu? au ni ushirikina tu? Maana mimi sidaiwi wala sina ugomvi na mtu..
wakimkuta na upara watazinyoa za ktk naniii.bora avae wigiDawa ni wewe kunyoa upara kote