mose
JF-Expert Member
- Jun 5, 2009
- 387
- 378
NKNS...Nataka kujua kwanza,anayechambua hapa ni wewe simba au arsis?
Kwasababu aya inasema "yeye ndiye aliyewaumbia yote katika ardhi" iweje yawe hayo ni maandiko?
Unazungumzia samawati/tabaka iweje hizo tabaka ziwe za elimu?
Wakati kuna tabaka za ardhi na mbingu
Naona kuna kitu hakipo sawa hapa
Maandiko ya hivi vitabu vya Dini, yanahitaji wakati mwingine kurejea kwenye mambo ya kiufundi ya 'lugha ya asili' /chanzo chake--hili daima litashangaza wengi ambao wameyaishi 'maandiko' kwa mazoea ya juu juu...
Kwa hivyo unaweza kushangaa 'ardhi' inakuwaje kuja kuwa 'maandiko'? Japo hilo limeshafafanuliwa humuhumu...
'Tabaka' na 'Uelewa'-- Hili ni kati ya mambo ya msingi na kheri sana kuja kuyafahamu katika 'mwangaza bora'; kwa kuwa jambo hili hili litakuja kujitokeza siku za mbele kidogo kuhusu kile kwenye mapokeo Ukristo kuhusu 'Mbinguni/Mbingu'--Ukweli wake ni jambo tofauti na ambavyo wasomaji wa maandiko hayo 'hufikiri' ama hata 'kuachiwa kufikiri'!
Vivyo hivyo neno 'Maji'...
In Shaa Allah, kwa saburi na ustahimilivu 'Maarifa na Maarifu' yanatengemaa....
.