Niliwahi kwenda kwa mganga kujitibu bila mafanikio lakini tatizo nililozoea la kuamka asubuhi na mikwaruzo liliisha, Je mikwaruzo ni uchawi?

gearbox

JF-Expert Member
Apr 20, 2024
244
706
Muhimu: Nilipelekwa huko ikiwa ni siri ya mimi na ndugu yangu ambae alishafariki, sehem tuliyofikia siikumbuki wala sina mawasiliano yoyote ya huko.

Kuna kipindi mwaka 2014 niliamini nina mikosi na nuksi kwa kuonaa maisha yangu yana utata, ndugu yangu wa karibu niliekuwa nikimshirikisha kwenye mambo yangu mengi aliniasa twende kwa mtaalam wa huko kijijini anakoishi.

huko tiba niliyopewa ni kufukizwa majani, nakumbuka nilifunikwa shuka, ghafla vijana kama wanne hivi walinishikilia kwa nguvu, ndani ya shuka kikaingizwa chungu kina mkaa, mtalam akaanza kuweka majani, moshi ulikuwa mzito sana niliijua thamani ya hewa safi, nilifukizwa karibu dakika 20 nilihisi kuzimia, kuna kijana moja milimgata pajani lile kovu haliji kufutika.


Kiufupi maisha yangu sikuona mabadiliko yoyote, maisha yalikuwa yale yale tu, ila ni hapo mbele kuanzia miaka ya 2017 nilivyoanza kuacha kampani za ovyo, kuwa na nidhamu ya pesa, kuchapa kazi, n.k. ndipo nikaja kugundua sikuwa na mikosi bali ni mtindo wa maisha niliyoyaishi ndio yalikuwa tatizo.

Lakini nilikuwa na tatizo la kuamka na mikwaruzo kwa miaka takribani nane, mimi nilishazoea kwa kuona labda najikwaruza kwa kucha, kwa mwezi naweza kuamka mara mbili mara nina miparuo begani, kwenye kifua, hata kwenye uso

Hilo tatizo liliisha kabisa baada ya kufukizwa kule kwa mtaalam na nikawa najiuliza sana kwamba limeisha sababu ya kufukizwa ? kuna chochote kilihusiana na ugonjwa huo kuwa wa kiroho ?
 
Nilipelekwa huko ikiwa ni siri ya mimi na ndugu yangu ambae alishafariki, sehem tuliyofikia siikumbuki wala sina mawasiliano yoyote ya huko.
Sawasawa mkuu, kwahiyo tatizo limeisha kabisa??? 🤒😎
 
Hakikisha unapuliza dawa ya mbu hapo geto kwako, pia KATA kucha mara kwa mara..

Mbu akikung'ata alafu ukajikuna lazima uache mikwaruzo na hivi mnakuka Ugali mkubwa usiku unalala kama Ng'ombe mjamzito.
 
Mmeona hamtupati kwenye simu mkaamua kuja JF. Nyinyi ndio wa hivi vi sms

666 KARIBU UJIUNGE NA CHAMA CHA FREE ,MASONI UMILIKI PESA ,NYUMBA,MAGARI NA BIASHARA> 0694620557

nitumie tu kwenye namba hii ya Airtel 0692979962 jina ni SALOME MWANJA

AU Nitumie Kwenye TIGOPESA Namba 0672677280 jina litakuja BRAISONI PATIRIKI SIMKONDA

au iyo ela nitumie asubuhi mapema kwenye AirtelMoney hii 0782772564 Jina litoke DAUDI SUMENO

Acheni wizi
 
"Kiufupi sikuwa na mikosi bali ni mimi mwenyewe tu mtindo wa maisha yangu ulichangia niwe na maisha magum, nilivyoweza kuacha kampani za ovyo, kuwa na nidhamu ya pesa, kuchapa kazi, mambo yalienda vizuri tu"

Nimekunukuu hicho kitu kiliwahi nisumbua pia nilivyogundua tu nilifanya kama hivyo hivyo ulivyofanya.
 
Hakikisha unapuliza dawa ya mbu hapo geto kwako, pia KATA kucha mara kwa mara..

Mbu akikung'ata alafu ukajikuna lazima uache mikwaruzo na hivi mnakuka Ugali mkubwa usiku unalala kama Ng'ombe mjamzito.
tatizo lilishaisha
 
Back
Top Bottom