Franky Samuel
JF-Expert Member
- Oct 10, 2018
- 5,180
- 13,719
Msimbazi hiyo ndo haina yao ya wizi unashangaa mtu anakuvaa alafu anakwambia umemkanyaga, mimi imewai kunitokea mala 2 ila hawajawai kuniibia sababu mimi mwenyew borntownMtoa mada atakua sahihi.
Kwasababu pia nakumbuka nikiwa kidato cha sita pugu sekondari nilienda kariakoo kuzurula. Nilikutana na kitu kama hiki lakini wao walikua mateja.
Kimsingi ilikua pale msimbazi. Mwenzenu nimetoka zangu mitaa ya karume sokoni kule narudi kituo cha kupandia daladala za kuelekea sinza kupitia shekilango.
Nilipofika pale, jamaa bana si ikawa kama vile nimemkanyaga bahati mbaya. Kiungwana nikajishusha nikamwambia samahani.
Kumbe lilikua kosa la kiufundi. Ndani ya dakika nilizungukwa na wadau kama saba hivi, mimi nilikua around miaka kumi na 19, nikawa sijui hili wala lile.
Bana wee, nikaskia mkono mmoja unaelekea mfuko wa nyuma. Akili ikanirudi. Nilizunguka mara moja kwa hasiri nikiwa nimeweka viwiko.
Dakika moja si kubwa wote waliamsha. Kucheki simu ninayo na elfu kumi na sita ninayo, yani hawakuchukua hata mia.
Nilivyomuona yule mdau mbele, aliezuga nimemkanyaga, nikamfata, kwa ujasiri, nikamwambia mpumbavu wewe, nikatoa simu na hela nikamwambia njoo uchukue, njoo, huku namfata, nimeisha iva kweli.
Jamaa akarudi kinyume nyume, nilimfata kama mita 3 hivi. Akatimua akaondoka uchochoroni huko.
Wanaume wa dar sasa/ yaani k/koo
Eti, kinafiki wananiuliza , mwanangu umejaa? Hawajakupiga tukio?
Nikawaambia wajinga nyie. Saa nane mchana yote hata kumsaidia mtu hakuna? Alafu mnatafuta umbea?
Nikaepa.
Kwaiyo wale wana ni wepesi kama tishu pepa.