Ninavyoona hawa watoto wadogo wakirudi kwa kasi na kusumbua wananchi wa Dsm amani inapotea kiasi chake na kukumbuka tukio lilowahi kunitokea miaka ya nyuma, ilikuwa ni mwaka 2013.
Kipindi hiki kundi la panya road lilikuwa linatikisa maeneo mengi sana ya Dsm na hawa vijana kipindi hicho walikuwa wengi mno, na walikuwa wakivamia magari, maduka, vibanda na raia wa kawaida.
Sasa katika harakati zangu za maisha wakaniweka kati siku moja na kuanza kunivamia ili wanipore. Nakumbuka ilikuwa mida ya jioni kuelekea saa kumi na mbili hivi mitaa ya Tabata.
Basi nikiwa natembea nikiwa na jamaa yangu mmoja, ili tuelekee kwenye usafiri nikasikia makelele haoooo, haooo…!
Kutazama nyuma nikaona kundi la vijana kati ya 20-30 hivi, vitoto vidogo vinakuja kwa kasi na vijana wakubwa walikuwa wachache, wakiwa na majambia, mafimbo, manati na silaha nyingine ndogo za jadi.
Raia wakaanza kukimbia, hovyo huku wengine waliokuwa hawawezi kukimbia wakakamatwa na kuanza kuporwa na kupigwa.
Kwa kweli kitendo kile kiliniuma sana.
Nilipata ujasiri wa ghafla na sikuogopa chochote, jamaa yangu akakimbia wakamkimbiza wakampora simu na pesa, kwa upande wangu kwa sababu sikukimbia kidogo wakawa kama wamesita kunivamia. Mmoja wao akaniambia Broh, mbona unajiamini sana toa kila ulichonacho!
Nikaingiza mkono mfukoni kujifanya natii maagizo yake, lakini nilichofanya nilikunja ngumi na kumtandika ya uso akaenda chini, akagonga kichwa damu zikaanza kumtoka puani! Wenzake walivyoona hivyo wakapata taaruki wakataka kuja kunivamia kwa mkupuo basi mwenyewe kwa kuwa sikuwa na silaha yaoyote, nikaanza kupanga namna ya kumvamia mmoja wao ili nimyang’anye walao jambia au fimbo!
Kuna kadogo kamoja kalikuwa kanashangaa nikakavamia kwa kukatandika teke na kushika mkonno wake nikavuta jambia lake, kakakimbia maana alipigwa na butwaa zaidi.
Basi nilivyopata lile jambia, sikuwachekea kwa kweli maana nilipata ujasiri wa ajabu. Nikacharaza mmoja mgongoni, kilichofuata sijui nilimpiga nani na wapi, maana walikuja kwa kasi nikawa nadunda tu, kumbe wananchi waliokuwa eneo lile walivyoona napambana nao, wakaongeza nguvu tukawashinda, wakakimbia wengine wakiwa na majeraha.
Yule niliyemtandika ngumi mwanzoni pamoja na wengine wachache tuliowabananisha pale, raia walitaka kuwazimisha kabisa, bahati yao polisi walipata taarifa wakafika na kuwabeba.
Yule jamaa yangu niliyekuwa nae nilimkuta amebeba bonge la jiwe, anamtafuta aliyemkwapua simu na pesa.
Kwa upande wangu sikupoteza kitu, ila nguo nilizokuwa nimevaa zilichanika chanika, nilipata jeraha kidogo mkononi.
Kwa sasa sipo Dsm, ila niliposikia wamerudi nikakumbuka hili tukio.
Ninachoona kwa hawa panya road ni kwamba wananchi wengi ni waoga hawana ujasiri na pia mbinu za kupambana na hawa vibaka wa aina hii wengi hawana.
Hao watoto wengi wanavuta bangi na kutumia madawa ya kulevya, hicho ndio kinawapa kiburi!
Hivyo wanapopita mtaani na kuvamia raia, kama kukiwa na watu jasiri wenye mbinu, hawa watoto hata kama wakiwa 100, kati yao ni lazima 20 au 30 hivi wanaweza kuthibitiwa na kufundishwa adabu, hao wengine hata wakikmbia huko waendako nako kukiwa na watu majasiri, watawabananisha vile vile na kuwaadabisha tu.
Sambamba na hayo kama hujiamini vya kutosha na huna nguvu au mbinu za kupambana nao wewe ni bora ulindi usalama wako, maana kwa kweli nao wakikubana ni hatari sana, havina huruma hivyo vitoto! Halafu vinanuka hatari, haviogi wala kuswaki.
Nakumbuka pia wakati napambana navyo nilikuwa nasikia harufu kali ya uchafu, unaweza kuzimia