Niliokoka baada ya kusikiliza Kwaya ya Makongoro na Uliyankulu!

Najua unachozungumza na ndio maana nimekuuliza

Kanisa la roma nalifahamu,lakini sijui ni msaada upi ambao wewe uliona huwezi kupewa hata kabla ya kuutafuta kwanza!

kumbuka pale juu nimeongea mambo ya rohoni zaidi,Roho mtakatifu anapochukua full control ya maisha atakupeleka popote ambapo anajua utapata msaada kwa muda unapokuwa na mahitaji hasa ya kiroho
 
Kuna kipindi nilisikia wengi wa waimbaji wa ulyankulu walikufa kwa ukimwi..naskia walikuwa wanaoana humo humo may be ndo ilichangia.

Nooo PLEASE! inahuzunisha sana kwa kweli,lakini kwa hakika kazi waliyofanya itakumbukwa milele
 
kumbuka pale juu nimeongea mambo ya rohoni zaidi,Roho mtakatifu anapochukua full control ya maisha atakupeleka popote ambapo anajua utapata msaada kwa muda unapokuwa na mahitaji hasa ya kiroho

Huko juu nimekuuliza kama roho mtakatifu ndio aliekuelekeza uende huko EAGT na hukunijibu

Lakini kwa mujibu wa Bibia roho mtakatifu mwenyewe ni msaada tosha,inakuwaje tena uwe nae uanze kudai anakuelekeza sijui wapi?

Roho mtakatifu ni mwalimu wa walimu wote wa maandiko,hahitaji kukupeleka kokote kule kwa msaada wa kiroho,sijakuelewa kabisa unapodai kuwa amekupeleka huko ....!
 
Ukisoma hayo maandiko hapo chini utapata mwanga wa utendaji wa Roho Mtakati

Matendo ya Mitume 9

Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu;
14 hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako.
15 Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.
16 Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.
17 Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
18 Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;
19 akala chakula, na kupata nguvu.
 
Weye umeona hizo kwaya mlizoimba hazina soko, sasa unakuja na gea mpya unajifanya zimekuokoa.

Siku hizi pamezuka magari ya kwaya zinapiga mitaani na kubembeleza watu kununua cd.

Pole sana, umepotea stepu.

umenichekesha sana
 
Ukisoma hayo maandiko hapo chini utapata mwanga wa utendaji wa Roho Mtakati

Matendo ya Mitume 9

Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu;
14 hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako.
15 Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.
16 Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.
17 Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.
18 Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa;
19 akala chakula, na kupata nguvu.

Ishu ya Paulo iko tofauti na wewe,kama ungesema kuwa baada ya kuamua kuokoka ulikwenda kwa kiongozi wako na kuwekewa mikono kisha ukatubu au ulikwenda kuungama kama ilivyo kwa taratibu za kanisa na Roma wala nisingekuuliza haya maswali

Wewe umekwenda kwenye nyumba ya ibada kitu ambacho kimenifanya nijiuize kama kweli unajua maana ya kuokoka au unafanya kimazoea tu,Paulo alikwenda huko kwaajili ya huduma ile na kuna sababu za msingi

1; Wakati ule hakukuwa na watumishi wa kutosha na hata namna ya kuomba kwa mujibu wa utaratibu wa Kikristo ulikuwa ni tofauti na vile ambavyo watu walikuwa wamezoea,hivyo ili uweze kuokoka kwa wakati ule ni lazima ulikuwa uwafuate watu ambao tayuri walikuwa wamejifunza na kumjua Mungu kwa mujibu wa Ukristo,Paulo hakuwa akijua chochote kuhusu Ukristo na ilikuwa ni lazima aende huko

2;Paulo alikuwa ni muuwaji wa wanafunzi wa Yesu,kitendo cha kuagizwa aende huko kilikuwa ni kitendo cha muhimu sana kwani kwanza kiliongeza imani ya mitume kwani hata mtu ambae walikuwa wakimuogopa sasa Mungu amemuokoa,pili ilikuwa akajitambulishe huko ili wanafunzi wa Yesu na Wakristo wa kwanza wasimuogope tena

Mazingira yanajieleza yenyewe kwa wakati ule,sasa wewe ni mazingira gani ambayo yalikufanya uende huko EAGT?
 
rosemarie

Nataka kujifunza kutoka kwako binafsi ulifanya nini kusikia sauti ya Mungu...umesema hakuna kitu kitatokea kwako usikijue..
 
Last edited by a moderator:
Huwezi kuona tatizo ambalo inazaliwa kila siku kwa watu ambao wanahama madhehebu

By the way,kimsingi hakuna sababu ya kuhama dhehebu pale ambapo unapoamua kuishi maisha ya Kikristo [kuokoka]

Kumbuka baada ya kufa na kufika kwa Mungu kutoa hesabu ya maisha yetu yalivyokuwa duniani hatutaulizwa tulikuwa tunasali dhehebu gani. Mungu anachoangalia ulikuwa ukiishi vipi ulipokuwa duniani. Maisha matakatifu yanakupa uhakika wa kuingia mbinguni. Maisha ya dhambi yanakupeleka Jehanamu. Hivyo watu hulazimika kuhama madhehebu au dini zao za awali kwa ajili ya kufuata MALISHO MAZURI YA NENO LA MUNGU. Madhehebu mengine hayaamini juu ya wokovu. Kifupi, wanapinga kuokoka. Hivyo kwa mtu aliyeokoka kuendelea kukaa mahali ambapo hata mchungaji ambaye anatakiwa kumsaidia anapinga wokovu, ni wazi kwamba atarudi nyuma. Yesu alisema kipofu hawezi kimwongoza kipofu mwenzake. Asomaye na afahamu
 
Upako unapatikana kwenye dhehebu?

Haya mambo hayana jibu moja.Kumbuka Mungu anakusudi kwa kila mtu kwa wakati na mahali fulani.Kuna mifano mingi katika bible ambapo Mungu aliwaamuru watu wake wahame nchi au wabadilishe majina.Kitu cha msingi hapa ni kumwabudu Mungu katika Roho na kweli .Hayo mengine hakuna mwenye haki ya kuhukumu
 
Kumbuka baada ya kufa na kufika kwa Mungu kutoa hesabu ya maisha yetu yalivyokuwa duniani hatutaulizwa tulikuwa tunasali dhehebu gani. Mungu anachoangalia ulikuwa ukiishi vipi ulipokuwa duniani. Maisha matakatifu yanakupa uhakika wa kuingia mbinguni. Maisha ya dhambi yanakupeleka Jehanamu. Hivyo watu hulazimika kuhama madhehebu au dini zao za awali kwa ajili ya kufuata MALISHO MAZURI YA NENO LA MUNGU. Madhehebu mengine hayaamini juu ya wokovu. Kifupi, wanapinga kuokoka. Hivyo kwa mtu aliyeokoka kuendelea kukaa mahali ambapo hata mchungaji ambaye anatakiwa kumsaidia anapinga wokovu, ni wazi kwamba atarudi nyuma. Yesu alisema kipofu hawezi kimwongoza kipofu mwenzake. Asomaye na afahamu

Umeandika mambo ya kufikirika sana. Mungu hatafutwi kwa Wachungaji au kwenye Makanisa. Kama alivyosema Eiyer Roho Mtakatifu haitaji kukusumbua na kukupelekapeleka hili umtambue Mungu. Mimi naona saa nyingine maisha yanawachanganya tu watu wanahangaika kila mahali kwa kisingizio cha kutafuta wokovu.
Ukikaa na kutulia mahali ulipo na kushikilia imani yako hakika Mungu atajifunua kwako.
 
Last edited by a moderator:
Nataka kujifunza kutoka kwako binafsi ulifanya nini kusikia sauti ya Mungu...umesema hakuna kitu kitatokea kwako usikijue..

Dear Zion Daughter,
mkristo yeyote aliyeokoka lazima ajifunze jinsi ya kusikia sauti ya Roho Mtakatifu,inaweza kuwa anakuonya au anakushauri kitu,baada ya kumpokea Kristo katika maisha nimekuwa nikisikia sauti kutoka moyoni mwangu,kwa mfano kuna kipindi nilikuwa nasafiri nilipofika bus stand nikasikia sauti kabisa inaniambia usipande hilo basi lakini ndiko nilikuwa naelekea kupanda the same basi,nilipanda basi lingine kwa sababu nimejifunza kusikiliza sauti ya Roho Mtakatifu,tulipofika Mikumi mbuga ya wanyawa ile basi iligongana na Lori la mafuta na kuua watu 38,kuna kipindi nilikuwa namtafuta mtu mmoja muhimu sana kwetu,anaishi kiwalani Dar,simfahamu wala sijawahi kufika kiwalani,nikaomba Mungu naomba nionyeshe huyu mtu,nilipofika Kiwalani nikasikia sauti inasema muulize huyo dada hapo mbele yako,cha ajabu kumuuliza kumbe ninamtafuta kaka yake kabisa,kuna umuhimu kujifunza jinsi ya kusikiliza sauti ya Roho Mtakatifu my Dear
 
unawezaje kuokoka huku bado unaishi?

Kuokoka ni kutubu na kuacha dhambi kwa kumwamini Yesu Kristo, na kumfanya kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. Soma Zaburi 16:3 "Watakatifu waliopo duniani, ndio walio bora, hao ndio niliopendezwa nao". Kwa hiyo utakatifu ni hapa hapa duniani. Kwa ufupi ni kwamba; KUOKOKA=UTAKATIFU
 
rosemarie, Bwana haangalii mwanzo mzuri, bali mwisho wenye ushuhuda.

Endelea kumkamata Yesu kwa nguvu, bidii na gharama yoyote.

Asante kwa ushuhuda huu wenye kujenga na kutia moyo. Bwana ayabariki na kuyainua maisha yako.
 
Last edited by a moderator:
Dear Zion Daughter,
mkristo yeyote aliyeokoka lazima ajifunze jinsi ya kusikia sauti ya Roho Mtakatifu,inaweza kuwa anakuonya au anakushauri kitu,baada ya kumpokea Kristo katika maisha nimekuwa nikisikia sauti kutoka moyoni mwangu,kwa mfano kuna kipindi nilikuwa nasafiri nilipofika bus stand nikasikia sauti kabisa inaniambia usipande hilo basi lakini ndiko nilikuwa naelekea kupanda the same basi,nilipanda basi lingine kwa sababu nimejifunza kusikiliza sauti ya Roho Mtakatifu,tulipofika Mikumi mbuga ya wanyawa ile basi iligongana na Lori la mafuta na kuua watu 38,kuna kipindi nilikuwa namtafuta mtu mmoja muhimu sana kwetu,anaishi kiwalani Dar,simfahamu wala sijawahi kufika kiwalani,nikaomba Mungu naomba nionyeshe huyu mtu,nilipofika Kiwalani nikasikia sauti inasema muulize huyo dada hapo mbele yako,cha ajabu kumuuliza kumbe ninamtafuta kaka yake kabisa,kuna umuhimu kujifunza jinsi ya kusikiliza sauti ya Roho Mtakatifu my Dear

Inaitwa intuition kila mtu anayo hata wa "Mataifa"
Omba hiyo sauti ikuongoze upende kujifunza vitu uongeze ufahamu wako, usipende kupelekwa huku una uwezo na maarifa mbele yako
 
Inaitwa intuition kila mtu anayo hata wa "Mataifa"
Omba hiyo sauti ikuongoze upende kujifunza vitu uongeze ufahamu wako, usipendwe kupelekwa huku una uwezo na maarifa mbele yako
naomba nikuulize swali my Dear,je umeokoka?nimeuliza ili tuweze kwenda sawa
 
Back
Top Bottom