rosemarie
JF-Expert Member
- Mar 22, 2011
- 6,887
- 3,416
Wapendwa katika Bwana
Leo ni jumapili na nimeona ni vema nitoe ushuhuda wangu jinsi nilivyokata shauri kumfata Yesu!
Nilikuwa msikilizaji mzuri wa nyimbo za Kwaya maarufu ya Makongoro na kwaya ya Ulyankulu nafikiri kutoka Tabora samahani kama nimekosea spelling,
Nilichogundua ni kila nikisikiliza nyimbo zao hasa kama nipo peke yangu machozi yalikuwa yakinitoka na nilikuwa nikilia sana.
Nilienda moja kwa moja kwenye kanisa la Evangelistic Assemblies of God wakanipokea na kuniongoza sala ya toba.
Kuanzia pale nilianza kujifunza neno la Mungu kwa undani na kugundua kumbe Biblia ni kitabu cha ajabu mno na kina mambo mengi ambayo pamoja na kwamba mimi ni mtu mzima na Mkristo niliyekuwa nasali kila jumapili nilikuwa siyajui.
Mungu alianza kujidhiirisha ndani yangu na nikajiukuta nipo karibu sana na Mungu kiasi kwamba hakuna jambo lolote linaloweza kunitokea ambalo silijui,
Pongezi zangu za dhati naomba ziwaendee popote pale walipo waimbaji wote wa kwaya hizo na viongozi wao na kanisa lao,kwa kweli kazi yenu ni kubwa mno japo siwajui lakini ujumbe wenu umejaa upako mkubwa mno.
Nimemwomba Mungu anisaidie niwatembelee siku moja popote pale mlipo,vile vile natamani niwe mmoja wa wadhamini wenu,naomba ujumbe huu uwafikie popote pale mlipo,Mungu awabariki kwani kazi yenu mnayofanya mtalipwa hapa hapa Duniani!