Nilimruhusu msaidizi auze bidhaa zake ndogo ila zinamlipa kuzidi mshahara wake. Je, nifanye maamuzi gani?

Uzi huu nimeweka jukwaa la biashara nategemea michango yenye tija. Tujue kutofautisha biashara na vituo vya kutoa misaada bure, msikiti, kanisa, n.k, THIS IS BUSINESS

Kuna kaduka nilifungua, kwakuwa utumishi umenibana niliweka msaidizi anisaidie.

nikitoa gharama za frame, mshahara, allowance, umeme, usafi, Tra, leseni, n.k. Duka linaingiza faida ya laki 3 hadi 4

msaidizii aliwahi kuniomba aanze kuweka bdhaa zake, Nilichukulia poa kwasababu niliona bidhaa anazouza ni ndogo na ni nje ya biashara nayofanya, Nikamruhusu.

Mshahara naomlipa ni 150,000 kwa mwezi, allowance ya matumizi yake elf 70, jumla 220,000

Leo nilifika dukani hayupo kafunga, nina ufunguo wangu nikaingia, kuna kidaftari nilikiona kwenye draw.

Kapangiliaia vizuri sana hesabu zake, kila siku anafunga hesabu kwa faida ya elf 6 hadi 7, sometmes elf 8

Nilipiga picha fasta, nimefika home nimepiga hesabu, mwezi uliopita kaingiza faida 168,500, Mwezi huu hadi leo kaingiza 87,000 probably anaweza kuingiza 180k mwisho wa mwezi

Kuna maamuzi kadhaa nataka nichukue

  • Nimwambie awe anachukua faida asilimia kadhaa kwa biashara yoyote atayoifanya dukani kwangu
  • Nisimlipe mshahara wake niwe nampa aloowance pekee, ajilipe mshahara kwenye faida
  • Nimpe miezi kadhaa auze, baada ya hapo iwe biashara yangu

Ni jambo liliilonfanya nitafakari sana, nichukue maamuz yapi.
Wivu mbaya. Biashara itakushinda hiyo. Hakikisha unamtumia ipasavyo. Ongeza bidhaa zingine ili faida iongezeke. Hayo maamuzi unayotaka yatakughalimu . Utampata anayekuibia usirudi kuomba ushauri
 
Una weza ukaanza kuziuza wew na zisitoke hata kidogo ukaishia kupata hasara usio itegemea kabisa, hatujaumbwa kufanya kila kitu maishani kila mtu kuna kile amepewa na mungu regardless ata fanya kwa njia gani au kupitia nn mkuu. Em chukulia kama sehem ya kumotivate yeye afanye kaz kwa bidii na uaminifu bila kuwaza kukuibia,
 
Uliishaamua tulia kwanza isije onekana una wivu.

Chunguza nini kimefanya biashara yako ishuke.

Unaweza kukuta hata huko nje anaweka bidhaa kama za dukani kwako na kufanya wateja waishie hapo nje.

Mwisho duka lako litafilisika yeye atafungua duka lake mtaa wa pili.
 
Muite muweke chini, umueleze kikubwa biashara yako kaiona imedrop, gharama za frem, mshahara na vitu vingine biashara haiendi, yeye anaonaje.. Msikilize kwanza.
Muulize kwake biashara ikoje, kama inalipa vizuri, umuongezee posho, mshahara muuvunje mpaka pale biashara itakapokaa sawa.

Kama kweli anapata faida atakubali.

Lakini mkuu faida ya 180k ndio ya kukutoa roho?
 
Unavyosema biashara yako imeshuka umejiuliza huu ni msimu wake wa pesa (high season)? Ulivyoona imeshuka kuna ubunifu wowote umeufanya ili kwenda sawa na hali? Kwa mfano kama ni duka la nguo huwezi kulazimisha kipindi cha baridi uuze Tshirt. Lazima utauza masweta na makoti. Je, kuna dalili zozote dada anachangia kuzorota kwa biashara yako? Kama dada hahusiki basi tazama kwa makini tatizo ni nini. Ila kama anachangia biashara yako kuzorota kwa kuweka nguvu kubwa kwenye biashara yake huna budi kumpiga chini na kutafuta mdada mwingine asiye na mambo mengi.

Lakini pia naungana na wadau wengine waliokulaumu kuwa una roho ya kichawi. Haina ubishi kuwa uko hivyo.
 
Hii roho yako mleta mada ndio wabongo wengi wapo hivyo,

Huruma inakuwa mwanzoni ili mtu ajihisi yupo huru kufanya chochote ili tu awe comfortable.

Najua huko kumwambia ajiongeze kwa vitu vidogo vidogo dukani kwako ilikuwa ni kumfanya awe huru na asijutue kufanya kazi kwako.

Lakini matokeo ya uhuru huo ndio wabongo wengi hawapendi na roho mbaya na chuki juu ya mtu ndio inapo anzia.

Hapo cha kufanya ni umuache aendelee na kazi yake na usimuingilie kwa chochote as long as anakufanyia kazi na anakuingizia pesa kama inavyotakiwa.

Akikuza msingi wake na akiamua kuondoka kufungua biashara yake pia unatakiwa umuache aende .
 
Wewe ni Ke au Me, maana kama mwanaume lazima usimamie maamuzi yako. Hiyo laki na 80, nilidhani labda anapata milioni mbili kumbe ki laki tu. Labda kama na wewe biashara yako ni vilaki ndio unaweza kuwa na ghubu.

Anyway Kuna mtu hapo juu kashasema uamuzi ni wako.
 
Back
Top Bottom