tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,388
- 21,280
Sitaki salamu, ninaingia kwenye mada moja kwa moja. Wazungu wanasema experience is the best teacher. Ajali ya kuanguka ghorofa la Kariakoo imenipa mafunzo mengi. Bila kupoteza muda, ajali hii imenifundisha mambo mengi sana, yakiwemo haya hapa:
1. Watawala wa nchi hii hawana huruma kwa wanyonge
Wakati taifa limeingia kwenye simanzi kwa kuondokewa na wapendwa wao, tena ambao wamekufa kikatili huku wakiomba msaada bila mafanikio, kiongozi mkuu wa nchi yupo Amerika Kusini anakula bata na Bashite yupo busy kule ALUSHA anafanya sherehe ya kula bata kwa miezi 6. Kwao, kufa kwa raia wasiokuwa na hatia haiwahusu.

Siku chache zilizopita tumeshuhudia Rais Biden anaondoka kwenye mkutano muhimu anarudi nchini kwake baada ya nchi yake kukumbwa na kimbunga lakini Rais Samia ameendelea kukomaa huko mpaka mkutano uishe wakati kuna janga nchini kwake. Pili, tumeshuhudia watawala waliobaki nyumbani wakienda mbio Kariakoo kuhalalisha malipo ya perdiem wakati kuna wananchi chini ya kifusi wanakufa kimyakimya. Taifa hili lina watawala katili na wenye roho mbaya sana. Kama wangefanya jitihadi angalau kidogo tu tungepunguza idadi ya wapendwa wetu waliopoteza maisha.
2. Tuna taifa la watu wajinga sana
Wakati nchi inaingia kwenye simamzi ya kuondokewa na ndugu zao, mmiliki wa jengo aliyesababisha vifo vya raia bado amejificha huku polisi wakiwa wamekaa kimya bila kumtafuta aje kujibu makosa ya mauaji yanayomkabili. Pia yule mpuuzi aliyetoa idhini ya kutoboa ghorofa kwa chini ili apate maduka zaidi ya kupanga, bado yupo uraiani anakula bata bila kuchukuliwa hatua. Kibaya zaidi, wananchi waliopoteza ndugu zao kwa uzembe wa serikali wamekubali kupokea 'rushwa' ya gharama za maziko ya wapendwa wao badala ya kuibana serikali iwalipe fidia na kukubali kuwajibika kwa upotevu wa roho za ndugu zao.
3. Mateja ni watu na nusu
Wakati ajali hii inatokea, wavuja jasho na hustlers wa Kariakoo, ambao mnawaita mateja, ndio walikuwa mstari wa mbele kufanya uokoaji huku jeshi lenu la zimamoto na uokoaji likiwa limeketi pembeni likishuhudia. Nimejifunza kwamba mafunzo ya uokoaji hutolewa kwa uwatu wasiokuwa sahihi. Mafunzo hutolewa kwa jeshi la uokoaji lakini watu wanaofanya uokoaji ni raia wasiokuwa na mafunzo ya uokoaji. Ipo haja ya serikali kuelekeza mafunzo hayokwa waokoaji sahihi badala ya kuwafunza waigizaji wasiokuwa na faida yoyote kwenye suala la uokoaji
4. Rushwa ni adui wa uhai
Maofisa wa serikali wanaotoa vibali vya ujenzi kwenye maeneo yasiyofaa kwa sababu tu za kula mlungula sijui huwa wanajisikiaje wanapoona makosa yao yakiondoa uhai wa mamia ya raia wasiokuwa na hatia. Hawa jamaa wachukuliwe kama wahaini wengine.. Mtu akiua kwa kukusudia, hunyongwa hadi kufa. Serikali inasubiri nini kuwanyonga hawa wauaji walioua halaiki ya raia wasiokuwa na hatia? Inauama sana.
5. CCM wanachezea kamari maisha ya wananchi
Katibu mkuu wa CCM, bwana Nchimbi amesikika akisema eti chama cha mapinduzi kimehudhunishwa na vifo vya raia waliopoteza maisha. He cant be serious. Uzembe wa CCM ndio umesababisha haya majanga kutokea halafu huyu kiumbe anajitokeza hadharani kuwakejeli watanzania bila aibu, woga au soni? Yakhe, hana khaya!
Kwa hali ilivyo na ikiwa majanga ya namna hii yataendelea kutokea, tutarajie vifo vingi vya wahanga. Tuombe Mungu aepushie mbali majanga ya aina hii yasitokee ktk nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki wananchi wa kawaida katika nchi hii. Amina