Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
1. Tatizo kubwa la Tanzania ni uongozi mbaya. Huu ni uongozi usiojua nini muhimu kufanya kwanza na lipi liwe namba mbili. Baya zaidi wengine katika viongozi kwa kweli hawajui kabisa nini la kufanya.
2. Ili kuendelea lazima viongozi wengi katika serikali wawe na 'exposure' kuwa wameishi nje au wamefuatilia kwa muda mrefu yanayoendelea nje. Ukitazama Rwanda, viongozi wengi wako hivyo, na zaidi ya hayo, raia wengi wameishi nje na kurejea.
3. Weledi wa lugha nyingine. Hii imewasaidia sana Wanyarwanda. Ukifika Rwanda unaweza kuzungumza lugha yeyote ukafahamiwa, Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili.
Hii imeifanya nchi hiyo kuwa rafiki zaidi na wageni wanaomiminika kila siku kutaka kuishi. Hawa wamefanya maisha mjini Kigali yawe 'international' na siyo maisha ya 'kimkoa' kama Dar! Nini la kufanya? Wahimize wananchi wajifunze lugha kuu na wala usizibehue au kuwabehua wanaoweza kuzizungumza! Himiza na toa ruzuku ya kuanzishwa kwa Shule za lugha za jioni kufundisha Kiingereza, Kifaransa, Kichina, kwa bei nafuu. Vijana wengi watumia wakati huo kukaa bwete vigengeni kuzungumza Simba na Yanga tu! Lugha ni ajira.
4. Neno 'dikteta' linatumiwa vibaya Afrika. Mara nyingi katika Afrika dikteta ni kiongozi asiyetaka mchezo, mwenye nidhamu na anayeipenda nchi yake mno, kiasi kwamba wakati mwingine atauwa ili kutimiza nadharia ya maendeleo. Kwa kweli kama Kagame ni dikteta, huo ni udikteta ambao nausapoti. Alipoingia madarakani, miaka 30 tu iliyopita, pato binafsi la Mnyarwanda kwa mwaka lilikuwa dola 350.
Leo pato la Mnyarwanda ni dola 900 likifukuzana na la Tanzania dola 1200 (yategemea source unazozinukuu. Nimenukuu chanzo kinachoipa pato la juu zaidi, ama wengine wanasema ni dola 995).
Rwanda leo ni nchi ya pili rahisi zaidi mtu kufanya biashaa barani Afrika, baada ya Mauritius.
Matumizi ya neno 'dikteta' naona ni mbinu za wale wale watu wetu wasiolitakia bara hili mafanikio. Huwezi kuwasikia wakilalamika juu ya 'udikteta' wa Saudi Arabia, Misri au Bahrain.
Kwa vyovyote vile, hakuna nchi hata moja iliyoendelea kwa Demokrasia. Nchi zote zilizoendelea, ikiwemo Marekani, Uingereza, Japan, Ufaransa zilipitia na kuendelea kwa udikteta. Hapa napenda nifahamishe kuwa kuna tofauti baina ya 'Udikteta' na "ukatili" Ingawaje dikteta mara nyingine hutumia ukatili, hii huwa ni kwa sababu za msingi.
Katili anafanya ukatili bila ya sababu ya maana, na aghalabu hufanya hivyo dhidi ya maslahi yake mwenyewe na ya nchi.
Nchi ningi Afrika hazina 'Madikteta' zina watu makatili. Dikteta huchukizwa na hali waliyomo watu wake, ama katili huchukizwa na watu wake!