Niliamini yoyote anaweza kutapeliwa baada ya kunasa kwenye mtego wa tapeli huyu

Miaka mitatu iliyopita majira ya usiku mida ya saa tatu baada ya kutoka chuoni nimepoa katika kibanda kimoja cha vinywaji baridi nikipiga stori mbili tatu na Mwanangu Tambwe.

Ghafla anatokea jamaa mmoja mrefu kiasi, mweusi sana na amevalia mavazi ya heshima na kunin'giniza kitambulisho kifuani, akanunua maji na kukaa kando yangu.

Akaniuliza kama mimi ni mwanafunzi wa chuo, nikamjibu ndiyo na hapa nimetoka chuo muda si mrefu. Akasema yeye anafanya kazi katika warehouse ambayo wanashusha mizigo kwenye makontena yaliyotoka kwenye meli.

Anasema siku hiyo wameshusha Laptop nyingi sana na amefanikiwa kubaki (kuiba) kadhaa, ameziweka sehemu na yupo tayari kuziuza. Nikamuuliza anauza bei gani, akasema kwanza anatafuta mtu wa kukaa nazo mpaka kesho kwasababu yeye usiku ule alikuwa shift ya usiku hivyo akitoka asubuhi ndipo atakutana na mtu atakaye kaa nazo then watafute wateja.

Akaniuliza kama nipo tayari kukaa nazo kwa usiku ule then asubuhi akitoka tukutane tutafute mteja tuuze, nikamwambia nipo tayari twende tukachukue... Hapo akili yangu inawaza anipe Laptop usiku ule alafu mimi niingie nazo mitini kesho hanipati.

Basi tukaanza safari kuelekea katika yard yao, safari ya miguu tukaanza kuitafuta TRH, tukaacha njia ya kigamboni kisha kukunja uelekeo wa bandarini au kurasini. Wakati tupo njiani jamaa alikuwa analalamika kwamba anahofu zile laptop endapo zikilala mule kesho hatoweza kutoa tena, nikamwambia tuwahi tukachukue mzigo mapema.

Wakati tupo njiani nasikia jamaa anaongea na simu anamwambia boss wake ametoka kidogo anarudi, kumbe alikuwa haongei ila anazuga tu ili niamini kweli anafanya kazi.

Hatimaye tukafika maeneo ya yard, akaniambia nisubiri aende ndani akaongee na walinzi ajue ni namna gani atatoa mzigo, akaelekea mbele kidogo ambapo niliona anaingia kwenye geti kabisa, ghafla akarudi akisema walinzi wanataka Elfu sabini ili waruhusu jamaa atoe mzigo, nikaona sio hasara nikampa hiyo pesa nikijua akinipa hizo laptop napotea nazo na kesho hanipati.

Nilimsubiri yule jamaa kwa zaidi ya nusu saa simuoni, nikaamua kwenda kwenye lile geti na kujaribu kuingia ndani ndipo nikagundua ile ni parking tu ya malori, na kwa ndani kuna mageti mengine ambayo mtu anaweza kutokea upande wa pili.

Nilijua tayari nimepigwa, mwili ulipata ganzi ghafla maana ile pesa ilikuwa ya matumizi ya kujikimu, nikaondoka maeneo yale nikiwa siamini kilicho tokea.

Nikarudi uhasibu kwa mwanangu Tambwe japo sikumueleza kilicho tokea, nikamuagiza K vant ndogo moja ninywe, akashangaa maana anajua mimi situmii pombe.

Basi nikanywa ile pombe kwa hasira sana, nikaanza safari ya kurudi geto, kufika geto nimelewa sana acha nianze kutapika, kumbe nilisahau kwamba jioni nilikula wali na maharage sasa na ile pombe cha moto nilikiona siku hiyo.

Kuanzia siku hiyo nimejifunza hapa mjini kutapeliwa ni kwa yoyote na haijalishi wewe ni mjanja kiasi gani ila siku ukiingia kwenye mifumo ya watu hutoki.
Ulitapeliwa kizembe mno mno. Hili wala huhitaji kutumia akili kujua ulizembea. Hivi mtu asiyekujua anawezaje kukupa laptop akuachie?
 
Epuka kuwa na tamaa,
Epuka kuwa na huruma
Jitahidi kutoamini chochote kwa haraka haraka.
HUTATAPELIWA.
 
Any Slight change na unnecessary Dodge za swali ni wazi Alikuwa anapausha na kukuficha ukweli ulio wazi ila ulizongwa na imagination zako aKakununua kama uduvi alipokuambia anatafuta wakukaa nazo.
Hiyo mbinu aliyo tumia ni matata sana hasa ukizingatia alikuwa anatafuta mwanafunzi wa chuo akijua kabisa hawa wana njaa kali
 
Mwizi aibe halafu aje kubwabwaja kwa mtu asiyemjua kuhusu kuhifadhi mzigo wa wizi?

Umetapeliwa kiboya. Tujenge utaratibu wa kujiuliza maswali kwenye kila situation.

Kingine, kuwa makini na mtu mwenye maneno mengi kuanzia kina Mwijaku, Baba Levo na wengine ambao maneno hayakauki mdomo.

Mi ukishakuwa muongeaji sana kengele ya hatari inalia kichwani kwangu.
 
Mkuu haina haja ya kunipa ushauri wote huo kwani sijaomba ushauri popote, ila makosa husababisha mtu kujifunza na nimejifunza hasa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom