Nihilism ni nini?

Hii kitu naona hata Kiranga kaikataa
Watu wengi wanachanganya atheism na nihilism.

Atheist ni mtu anayekataa uwepo wa Mungu tu. Mtu anaweza kukataa uwepo wa Mungu halafu akaona anaweza kuyafanya maisha yawe na maana, akawa anafanya research ya kisayansi kugundua dawa ya kansa, kwa sababu haamini kuwa maombi kwa Mungu yatasaidia, kwa sababu Mungu hayupo.

Nihilist wa kweli haoni maana yoyote ya maisha, na hivyo kufanya research ya kupata dawa ya kansa kwake ni contradiction.
 
Ni kweli maisha hayana maana kwanini viumbe wote njia yetu ya kuondoka duniani iwe Moja ambayo ni kifo , kwanini isiwe Kila mtu aondoke duniani kwa namna anayoipenda yeye na isiwe kifo TU ? Ina maana nilizaliwa Ili nije kufa Tena , Sasa Kuna maana Gani ya Mimi kuzaliwa ?
 
Maisha hayana maana inherrently, ila wewe unaweza kuyapa maana maisha yako.

Mfano, hupendi kifo. Unaweza kusoma kujielimisha njia za kuzuia kifo kinachozuilika ukawa daktari wa watoto, ukaokoa maisha ya watoto wengi waliokuwa wanakufa kabla ya kumaliza siku moja duniani wakaishi zaidi ya miaka 100.

Ni kweli watakufa, lakini kifo cha mtoto wa siku moja na mzee wa miaka 101 si sawa. Ukiwa daktari na kusaidia hivyo, maisha yako yatakuwa na maana sana kwa hao watoto uliowasaidia.

Kifo ni matokeo ya the second law of thermodynamics si kwa watu tu, kila kitu kina mwisho wake, jua, nyota zingine, sayari hata ulimwengu utafikia the heat death of the universe kwa mujibu wa physics.

Halafu kifo ni njia ya ulimwengu ku recycle materials zilizomo ndani yako, usiwe selfish kutaka kuishi wewe tu, waachie wengine nao waishi, na hao wengine hawawezi kuishi bila wewe kufa. Kama wewe ulivyoweza kuishi baada ya wengine kufa. Ungeonaje kama isingewezekana wewe kuzaliwa kwa sababu babu zako wamekataa kufa?

Hivyo, ni vizuri kuangalia mambo katika muktadha sahihi.
 

Nimeichukua hii 🙏
 

Shujurani kwa mada nzuri. N8merudia kusoma na nina ma9ni ya ziada kuhusu kipande cha Nietzche.

Nietzche inawezekana alikuwa sawa kuwa ukiondoa dini na utamaduni wengi wanaweza kuishia kwenye nihilism. Lakini kufikiri kwamba hakuna tumaini kabisa la kuepuka nihilism ukiondoa dini na utamaduni ni kukosea. Kufikiri kwamba ukiondoa dini na utamaduni maisha yataishia kwenye nihilism ni makosa.

Kufanya kitu kwa sababu ya dini au utamaduni ni kufuata logical fallacies.

Kufanya kitu kwa sababu dini imesema ni logical fallacy ya appeal to authority, kufanya kitu kwa sababu ya utamaduni ni logical fallacy ya appeal to tradition.

Tunaweza kujiwekea moral framework zetu ambazo si lazima zitoke kwenye dini wala utamaduni na zikafanya maisha yawe na maana.
 
Halafu nimegundua kitu maisha ya binadamu yalipaswa kuwa kama yale mnyama yakuishi kiasili na kivyakevyake haya mambo ya serikali na vikorokoro vingine wameyatengeneza watu.Binadamu ni mnyama aliyechangamka
 
Ni kweli kabisa mpagani wewe
 
Nice one brother

Kitu ambacho kilikuwa kinamtatiza Nietzsche ni hatua mwanadamu wa kisasa anazopiga kila kukicha ambazo kwa namna moja zinapunguza utegemeo kwa Mungu katika kufafanua mambo. Mfano zamani watu walihusisha marathi na ghazabu ya Mungu kitu ambacho sasa watalamu wa afya wanajua si kweli na kutoa ufafanuzi usiohitaji Mungu. itafika siku mwanadamu hatakuwa na jambo lolote la kumwomba Mungu hapo ndipo Nihilism crisis inapoanzia.

Jinsi ya kukabiliana na changamoto zitokanazo na Nihilism philosopher wanne walitoa njia. Nietzsche, Schopenhauer, Camus, NA Kierkagaad.

Nietzsche - alitoa concept ya ubersmensch kwamba kila mtu atafute meaning inayomfaa yeye mwenyewe wala asibabaishwe na dogma za watu wengine, kila mtu atengeneze maana yake ya maisha.

Schopenhauer - world as will hapa duniani ni mateso mwanzo mwisho na hamna njia ya kuepuka, tupo kama kondoo tunasubiri kukutwa na jambo muda wowote sehemu yoyote. Hata hivyo kuna mda mfupi sana tunaweza enjoi music mzuri au picha nzuri alafu tunarudi mtingoni kwenye mtungo wa maisha.

Albert Camus - ubsurd mwanadamu anaubongo rational ulio katika ulimwengu ambao ni ubsurd. Kwa hiyo tukubali kila hali tunayokumbana nayo na hakuna point ya kulalamika.

Soren keirkergaad - huyo alikuja na kitu kina itwa leap of faith, kwamba muda mwingine inabidi uwe na imani tuu ili uepukane na Nihilism.
 
Mkuu wewe ni mtu makini mno humu jukwaani , ningependa kuona hata unaandika kitabu kwa vizazi vinavyokuja🤔🤔🤔
 
Mkuu wewe ni mtu makini mno humu jukwaani , ningependa kuona hata unaandika kitabu kwa vizazi vinavyokuja🤔🤔🤔
Shukurani kwa maneno yako.

Nimekuwa napata unyonge kila siku tukijadili mambo ya sayansi na falsafa kwa mfano, tunanukuu watu wa Marekani na Ulaya, kama vile Afrika haijatoa mchango kwenye haya mambo.

Tatizo kubwa ni kuwa hatuandiki. Mpaka historia yetu wenyewe mengi sana yameandikwa na wageni.

Kuna mpango wa kuandika vitu fulani sasa hivi.
 
Nashukuru sana mkuu nimekuelewa mno.🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…