Nifungue ipi kati ya NMB Bonus Account vs CRDB Saving Account

Grand Canyon

JF-Expert Member
Jan 2, 2020
525
1,132
Nina mpango wa kufungua akaunti ya akiba ili niwe nahifadhi pesa. Kisha baada ya mwaka ni draw zikiwa na interest nizifanyie wazo ambalo nitakuwa nimepanga.

Kwa wazoefu ipi ni nzuri zaidi, na je kuna tofauti gani kati ya hizo nilizotaja na Fixed Deposit Account?

Ahsante kwa msaada wenu.
 
Mkuu hapo hauna vikundi vya hisa?
Kwangu kuna kikundi kinazalisha sana.
unaweza wekeza 280 kwa miezi 6 na ukavuna 50's faida.
kila wiki unaingiza ten.
piga mara hisa unazonunua.....
Sisemi uje huku ila angalia vya namna hiyo
 
Tofauti ya bonas account na fixed diposit account ni

Bonus account rates zake ni ndogo lakini una uhuru wa kuongeza pesa kila baada ya muda fulani

Fixed deposit account, Rates zake n kubwa lakini hauna uhuru wa kuongeza pesa na huwa ukiweka hela Huna uwezo wa kuitoa mpaka muda maalumu uishe
 
sina hamu tena na fixed deposit account, niliweka tsh milioni 1 crdb kwa mkataba wa miezi3 baada ya miezi 3 kufika sikutoa pesa zangu nikaenda baada ya miezi 6 kupita nikakuta nimewekewa faida tsh3000/= nikabadilisha account kutoka fixed deposit account kuwa account ya kawaida siku nyingine nilipokwenda kuangalia salio nikakuta elfu3 nilizokuwa nimewekewa kama faida zimekombwa na kwenye milioni1 nako zimekombwa zimebaki laki tisa na kitu.
 
Hao CRDB Kiboko
 
Nina mpango wa kufungua akaunti ya akiba ili niwe nahifadhi pesa. Kisha baada ya mwaka ni draw zikiwa na interest nizifanyie wazo ambalo nitakuwa nimepanga.

Kwa wazoefu ipi ni nzuri zaidi, na je kuna tofauti gani kati ya hizo nilizotaja na Fixed Deposit Account?

Ahsante kwa msaada wenu.
Nipe interest rate za bank zote, pia na amount ya pesa utayo kuwa unawekeza kila mwezi. Nitakufanyia hesabu
 
  • Interest rate 1.5% nimeweka 500,000. crdb
Hi
Nakushauri nenda kafunguwe fixed deposit DTB bank. Interest aye ni 5.75% kwa mwaka. Baada ya withholding tax ni 5.175%(5.75*(1-10%)

Faida itakuwa Tshs 26,498/=
Untitled.png
 
Hi
Nakushauri nenda kafunguwe fixed deposit DTB bank. Interest aye ni 5.75% kwa mwaka. Baada ya withholding tax ni 5.175%(5.75*(1-10%)

Faida itakuwa Tshs 26,498/=View attachment 1766342
Ni savings zote ambazo huwa wanatoa Interests?
Mfano Kuna savings ambazo hukatwi Monthly Maintenance Fees Wala Bank Charges ambazo hazina Mpangilio labda Transaction Charges.

Nakuna zile saving account ambazo zimewezeshwa unaweza Kutuma/Kupokea/Kulipia Huduma Nje ya Nchi ambayo Wanakata Monthly Charge kama 2000 Kwa (CRDB) Tsh na Other Transaction Charges.

Hii imekaaje
 
Back
Top Bottom